Tukubali yaishe?

Kitila,

Ngoja nijitoe pia tena sio kuchangia tu hata kusoma, nisije nikapata mafunza pia kichwani!
 
unajieleza kichwa kilivyochoka? rudi bongo kijana kama kichwa kimejaa mafunza! nilifikiri umeota sugu! teh teh teeee tehhhhh

Pole sana, siwezi kukusaidia na frustration zako za maisha!

Nani kakuomba msaada....mbona unajipendekeza hivyo? Eti frustration za maisha...nadhani ungependa iwe hivyo lakini ndio kinyume chake. Halafu usiongee tu mambo bila kujua. Nani kakuambia mimi siko bongo...? P********. Hao funza wamekudhuru vibaya sana wewe
 
Haya its a beautiful new day, a cloudy and cold dear.. ya jana yalikuwa ya jana na ya leo yatakuwa ya leo.. life moves on! Kitila umejibu swali jingine muhimu... Thanks everybody who contributed to this thread michango yenu imefungua mawazo yangu kwa kiasi kikubwa kuliko mnavyoweza kufikiri, na mmenifanya kuelewa mambo fulani ambayo huwa yamekuwa yakinisumbua...
 
Mwanakijiji,

Fasihi yako nimeielewa, ila sina uhakika kama niko sahihi. Kwamba unayoyataka (na wananchi walio wengi kwa ujumla wake) serikali hii iyafanye, haiyafanyi. Hata kama inayafanya, inayafanya kwa kiwango kisichoridhirisha na kwa taratibu sana! Pia kupiga kelele tokea nje ya CCM kunawafanya wasisikilize kwa sababu "they can not swallow their own pride".

That means you are in a dialemma as to whether you join them so that they can listen to you or just keep shouting from outside the ruling party. Yeah!, it is really a political dialemma because once you jump into CCM and realise that they are still not listening to you, you will either be more frustrated or just decide to become greedy are they are.

Had I been you, I would have just kept on shouting from outside, and to be on a better side from a non-political organisation. Just like HAKI ELIMU, TAMWA and the likes do. Shouting from an opposition political party sometimes makes things even worse. The government of the ruling party ignores all the recommendations, however good they might be. Take an example of this year's alternative budget from the opposition parties, it was professionally prepared and had there been any efforts to merge it with the gorverment one, we would be having a better budget today. That is my opinion anyway.
But the gorvenment wouldn't do anything with it because it would mean giving credit to the opposition.

I like Kitila Mkumbo signature on this forum.."Evil flourishes when good men (and women)do nothing". Mwanakijiji, I suppose you are one of the good men and you should not keep quite.
 
Masaki, well put! Na by extension naangalia dilemma ya wale walioko ndani ya CCM pia na ambao wamekuwa wakipiga kelele na hawasikiki na kama mtu mmoja alivyosema humu wamejikuta wamebadilishwa na CCM. Watu hao kutoka hawawezi na kuendelea kukaa wanaungua.. Ukilinganisha dilemma ya wale tulio nje na ambao hatuna uwezo wa kusikika na wale walioko ndani wana uwezo wa kusikika lakini wanapuuzwa basi utaona kuwa dilemma yetu ni ndogo kuliko ya kwao.

Inawezekana hili linaelezea gharama kubwa ambayo mtu aliyeipinga serikali inabidi alipe kwa kurudi "kundini". Leo kina Dr. Kabourou, na wengine wao wako wapi? Hata hivyo tunaweza kuwaona watu kama kina Butiku, Salim, na leo Malecela wana uwezo wa kuikemea CCM na viongozi wakiwa nje zaidi kuliko wakiwa ndani.

Swali kubwa ambalo bado najaribu kuliexplore ni jinsi gani CCM inaweza kufungua milango ya hoja mbadala ndani yake pasipo kulazimisha wanachama wake wajipange mstari! Suala la Buzwagi ni mfano mzuri na lile la Richmond pia. Kama CCM ingekuwa na utaratibu mzuri wa kukubali mavericks politicians ndani yake ingekuwa imechangamka mno. Ndio maana watu kama kine Selelii walipojaribu kuzungumza kwa nguvu wakazimwa kama kijiti kiwakacho kinapomwagiwa maji! Kwa watu kama hao uchaguzi wa kusuka au kunyoa unaonekana kwa urahisi zaidi na wapinzani kuliko walio ndani ya CCM.
 
...1000's of countless post against mafisadi & injustice,at the end this is what u get from traitors like Mwanakijiji,kama unafikiri ulichokuwa unaandika hapa kilikuwa utani kuna watu kimewa affect big time na mmoja wa victim wako ni msolla...swali moja tuu kabla sijamalizana na wewe is this reconciliation or surrender?
 
neither!! ni Msolla na mafisadi wenzake yamewakuta yaliyowakuta! na huko tunakokwenda mapambano ya kifikra yataletwa kwenye malango yao!
 
Kwanini msisalimu amri tu na kukubali kushindwa? Wakati huu ndio wakati muhimu kuamua kama mapambano haya tunayaweza au tuseme tumeshindwa. Mapambano haya ni ya fikra na mioyo ya Watanzania. Nani atashinda inategemea nani anapigana. Leo zamu ya Kikwete kucheza chess yake and he surely made his move. Do we have a counter move au ndio katuambia "check mate"? na wote tumebakia na moyo wa kukata tamaa?
 
Mzee Mwanakijiji,

Mie nilishakubali siku nyingi sana,i happen to talk with one of the most prominent person ,who was also a senior officer by then Mkapa ni Rais.

He told me a lots of thing about how the system works,system inaongozwa na watu ambo ni viziwi,wenye kiburi na wanaopenda mawazo yao yaheshimiwe tu.

unakumbuka kauli za Mramba,Hata wananchi wale nyasi ila ndege ya rais itanunuliwa?

unakumbuka kauli za Sumaye,Kwamba kama wewe siyo CCM ni vigumu kufanya biashara zako?

wewe unadhani ni kwanini watu kama Mgonja na maneno yote hawang'oki?

Brother and siters,tusikate tamaa sababu sasa nimepata nguvu mpya..nadhani we need to participate in these changes rather than monitoring serikali ikifanya kazi siyo onekana.

tuingie ndani na tulete mabadiliko,kama John Githongo aliweza kuseamyale waliyoshindwa wengine ,i think we can..
 
JK kweli ameprove failure. JK Kama alithubutu ku freeze Account ya Kighoma A Malima Mwaka 1995 akiwa waziri wa fedha inakuwaje mafisadi wanamshinda, au anataka amwachie rais wa awamu ya Tano aje kuwashitaki mafisadi kina Chenge, Mkapa,na Yeye atakuwa kwenye list wakati huo?.
 
Goli ndiyo hiyo limeingia, nyavu zinatikisika, refa anasema "mpira kati"... dakika 90 ndiyo hizo zimepita, mnarudi uwanjani kufanya nini!? tukubali yaishe tusubiri mechi nyingine... ?
 
Mzunguko wa pili....timu ile ile refa yule yule dakika zile zile....kuna haja ya kujipanga upya?. .au matokeo yanajulikana?
 
cha kushangaza licha ya watu kujua kuwa refa atawabeba jamaa, lakini bado watu wanaenda uwanjani!

Lakini na timu siinaingia uwanjani, au mashabiki wawe wa timu moja tuu, na timu isipoingia uwanjani mashabiki watakasirika kwa kuwa wana imani na timu yao lakini kuna mambo hawayajui, hawa ni mashabiki tuu..
 
Nimeamka leo na mawazo ya ajabu sana! Maajabu kiasi cha kunishangaza mimi mwenyewe, na siyo tu kunishangaza bali kunistaajabisha kwa kunishangaza jinsi ninavyoshangaa! Hata hivyo ni mawazo ambayo kwa hakika ni ya mtu aliyefikia ukingoni... Tumepiga kelele hawakushtuka, tumeimba hawakucheza, na tumewaita hawakuitika! Wameamua kuendelea kufanya wafanyalo, kulinda walindalo, na kuendeleza kile kinachoitwa "libeneke".

Hata kama mtu ni shabiki wa timu ya mpira wa soka, kuna wakati ule ushabiki unakutoka hasa timu yako inapobugizwa magoli utadhani mchezo wa mpira wa kikapu. Ukifungwa goli moja unaweza kusikitika lakini bado ukaendelea kuishangalia timu, lakini goli la tatu, la nne, la tano, hata kama ni shabiki wa kuzaliwa inabidi uvue jezi na kuishangalia timu ya upinzani au kuamua kujing'atua uwanjani pole pole!

Bila ya shaka hadi hivi sasa hakuna shaka ni serikali gani tunayo mkononi, tunafahamu kwa hakika kuwa sera yao ya kulindana bado inaendelea, wako pole pole kushughulikia masuala ya mustakabali wa Taifa, na kwa hakika hadi hivi sasa hawana kipaumbele cha utendaji! Serikali haiwezi kufanya kila kitu kwa kiasi kikubwa ndani ya muda ule ule isipokuwa mpaka ichague kipaumbele na kipi kitangulie. Kama ni miundo mbinu, elimu, afya, madini n.k serikali makini ni lazima ijue inataka kuweka msisitizo wapi. Haiwezekani hata kidogo kumridisha kila mtu kwani matokeo yake hakuna atakayeridhika.

Waswahili walisema "panya wengi hawachimbi shimo refu". Maana ya msemo huo inashabihiana kabisa na ile "law of diminishing returns" ambapo inafika mahali faida inazidi kupungua pale vitu fulani (variables) vinazidi kuongezwa. Kwa kuongeza wakulima zaidi kwenye shamba la ekari moja haina maana mavuno yataleta faida zaidi! Kwa jinsi serikali yetu inavyokwenda nina uhakika tumefikia mahali pa diminishing returns na hatuna budi kupunguza vitu fulani.

Tupunguze vitu vya kufanya ndani ya miaka mitano ya mwanzo (sasa mitatu iliyosalia). Rais Kikwete na timu yake wake chini na kuingalia Ilani ya CCM na waamue kwa dhati ndani ya miaka mitatu iliyobakia ni nini kitatiliwa kipaumbele ili ifikapo 2010 angalau vitu hivyo viwe vimefikiwa angalau asilimia 95 ya malengo yake. Kwa kufanya hivi napendekeza kuwa na vipaumbele vya aina mbili.

a. Vipaumbele vya Msingi. Hivi ni vipaumbele ambavyo ni lazima serikali yoyote ihakikishe vinaendelezwa kila mwaka. Vipaumbele hivi vinahusu huduma za jamii (afya, elimu, na maji); vipaumbele vya Usalama (majeshi, ulinzi n.k) na vipaumbele vya miundo mbinu (barabara, umeme, simu n.k).

b. Vipaumbele vya Kati: Hivi ni vipaumbele ambavyo kila serikali inafanyia kazi kwa kadiri ya inavyochaguliwa. Mara nyingi vipaumbele hivi vinafuata sekta maalumu au eneo maalumu la kiuchumi. Lengo la vipaumbele hivi vya kati ni kufikia vipaumbele vya msingi. Maeneo ambayo serikali inaweza kuyatilia maanani katika sehemu hii ni vitu kama : Ubadilishaji wa sheria, utungaji wa taratibu, usimamizi na uchunguzi wa mambo fulani n.k Hivyo masuala kama ya mikataba n.k yangeweza kutiliwa maanani mara moja kwa kubadilisha taratibu na sheria na kufanya uchunguzi ili vipaumbele vya msingi viweze kufanikiwa pasipo matatizo.

Tatizo tulilonalo sasa ni kuwa watawala wetu wanajaribu kufanya mambo mengi kwa muda mfupi kwa kutumia watu wengi zaidi. Hili kwa hakika itakapofika 2010 tutajikuta hatujafanya mengi. Kwa vile watawala wetu wanajaribu kuridhisha kila mtu na kwa maneno yao mengi wanajaribu kufanya kila wawezalo kuonesha wako ontop of everything, na kwa sababu siamini hata kidogo kuwa wataweza kufanya yote waliyoyasema na kuyaahidi, nimeamua kuweka manyanga chini hasa katika suala la kuikosoa serikali.

Nimeamua na mimi kuungana na wale watafutao yale mazuri ya serikali na kuyapigia mbiu na kuyatangaza! Nimekubali yaishe... Nimekubali kuwa wao ndio watawala na walichaguliwa kwa asilimia 80, wanapendwa na wananchi na wanakubalika kutawala miaka mingine hamsini ijayo... kama walivyosema wengine "kama huwezi kuwashinda, jiunge nao".

CCM here I come, naomba kadi au ukada wa aina fulani....

Nilipata kusikia kwamba Mh manji anahusika na KAGODA, kisha baada ya hapo nikasikia kwamba Manji kapatwa na ugonjwa wa kichaa, kisha kutibiwa nairobi, hivi ni kweli kwamba Manji ni mfadhili wa Muungwana a.k.a Kikwete?

Miaka Hamsini?!! mimi nimeshindwa kuelewa una maana gani hasa!, kwamba tukubali yaishe!! ( hizo ni kauli za mfa maji ! )

sababu unatapotamka sentensi kama hiyo kuna baadhi ya watu wanashindwa kuelewa msimamo wako,

hili suala la kuomba kadi ya uanachama CCM ( Chama Cha Mafisadi ) sababu haujaanza leo kiasi kwamba sisi wengine tusiojua lolote (ama kutokuwa na Chama) unatuacha njia panda hasa hasa unaposema kwamba kama hauwezi kushindana nao basi jiunge nao!

Kujiunga na mtu ama kikundi inamaanisha kujihusisha katika shughuli (iwe mbaya ama nzuri ), na inajulikana kabisa kwamba kila mtu ana matakwa yake, na kila chama kina kauli mbiu yake, mfano hicho chama ulichokitaja hapo juu , kina kauli yake ( Maalumu kabisa! ) ambayo inasema " Chukua chako Mapema "

Unajua wazi kabisa sera ya vyama vingi ilianza miaka ya 90, na kabla ya hapo tulikuwa na chama dume, katika kipindi kama hicho tuliona watu wengi walioitwa mikia ya fisi ( walikuwa wakihama chama kimoja mpaka kingine, siku moja mpaka nyingine ),inajulikana wazi kabisa kwamba katika kipindi kama hicho tulikuwa tukipigwa changa la macho na wale waliojiita wanamapinduzi a.k.a wanaharakati ambao hakuna walichokuwa wakipigania zaidi ya kufanya mambo yawe magumu, ( njaa na manufaa yao binafsi! )

sina uhakika kama jamaa hao wameisha , kama wapo, basi nina uhakika bado wapo kwa ajili ya kuuwa Demokrasia ( the so called! ) .

Pia kuna uandishi unaoitwa "Ukanjanja" , ninadhani hata Muungwana alishawahi kuzungumzia kuhusu hili sababu mawakala wa RA na wenzake ni wengi tu na wanajulikana.

sasa ni kipi ambacho tunaweza kutegemea kutoka kwa mtu kama wewe ambaye unapaswa kuwa mstari wa mbele ,mfano wewe m.kijiji umekuwa nguzo ama daraja muhimu kwetu sisi ambao tuko mbali na habari za uhakika ( ama za kushtukiza ) katika namna moja ama nyingine.
Mbali na hilo inafahamika wazi kwamba JF ni jukwaa ambalo tunapata habari mapema na zilizo na uhakika.
kitu ambacho ninaweza kusema ni kwamba upepo ndani ya jukwaa umebadilika ghafla tangu kipindi Jakaya alipolihutubia bunge na kisha kugusia kuhusu EPA.

Bila kusahau , kuna mtu alishawahi kuzungumzia kuhusu hili ( kwamba upepo ndani ya JF umechafuka ) na kisha baada ya hapo mtu huyo alisisitiza kwamba ni bora watu watu wakahamia katika majukwaa mengine kwani humu hapakaliki tena!.

vile vile kulitokea fununu kabla ya hapo kwamba JF inatishiwa kufungiwa!, lakini kuna baadhi ya watu wakawa " assure " kuhusu hili na kwamba mambo yote yatakuwa sawa, baadhi ya watu wengine kidogo wanakuwa na wasiwasi kuhusu hili.

imefikia kipindi wanachama wa jukwaa hili wakawa na msimamo na nia moja ( hii inamaanisha jambo linafanyika na kutekelezwa ) , na pia jukwaa kwa ujumla kuwa na Lengo maalumu, badala ya kulalamika kila siku na kuishia kuwa watu wa kulalamika tu pasipo kuchukukua hatua yeyote ile.

Mwanakijiji na wengine naomba msikubali kwamba kulalamika tu ndio suluhisho la tatizo, pia usisahau suluhisho la tatizo si kulikimbia!.
 
ushabiki wangu wa Kikwete haukuwa na kificho na mapenzi yangu kwa CCM sijawahi kuyaficha. Hata hivyo muda huo wote SIKUWA MWANACHAMA nilikuwa shabiki tu hasa ukizingatia nililelewa ndani ya CCM na kunyweshwa maji ya bendera. Na kwa muda wote sijawahi kuwa na kadi yoyote ile isipokuwa ya CCM niliyopewa miaka ileeeeee wakati natakiwa kwenda mafunzo ya Mgambo!(ila ilishaexpire baada ya kuukimbia mwenge 1984).

Niliomba kujiunga na CCM mapema mwaka huu lakini wakanipa masharti magumu gumu hivi ya kucompromise some of principles nikagoma tu. Ila sasa wataka au wasitake nitajiunga nao humo humo... kwani naamini ninatimiza masharti yote ya kuwa mwanachama.
Kumbe wenzetu waliombaga kuwa wanachama wa CCM?!, angalau sasa ndio nimeanza kuelewa!, na kiuk
weli jambo ukiishalielewa, halikupi taabu!.

Nakutakia kazi njema, October ama tutapongezana ama tutapeana pole!.

Pasco
 
Kumbe wenzetu waliombaga kuwa wanachama wa CCM?!, angalau sasa ndio nimeanza kuelewa!, na kiukweli jambo ukiishalielewa, halikupi taabu!.

Nakutakia kazi njema, October ama tutapongezana ama tutapeana pole!.

Pasco

Pasco this is too low for you, yaani unatafuta link za ajabu ajabu, ngoja niishie hapa
 
Back
Top Bottom