Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,693
- 40,700
Nimeamka leo na mawazo ya ajabu sana! Maajabu kiasi cha kunishangaza mimi mwenyewe, na siyo tu kunishangaza bali kunistaajabisha kwa kunishangaza jinsi ninavyoshangaa! Hata hivyo ni mawazo ambayo kwa hakika ni ya mtu aliyefikia ukingoni... Tumepiga kelele hawakushtuka, tumeimba hawakucheza, na tumewaita hawakuitika! Wameamua kuendelea kufanya wafanyalo, kulinda walindalo, na kuendeleza kile kinachoitwa "libeneke".
Hata kama mtu ni shabiki wa timu ya mpira wa soka, kuna wakati ule ushabiki unakutoka hasa timu yako inapobugizwa magoli utadhani mchezo wa mpira wa kikapu. Ukifungwa goli moja unaweza kusikitika lakini bado ukaendelea kuishangalia timu, lakini goli la tatu, la nne, la tano, hata kama ni shabiki wa kuzaliwa inabidi uvue jezi na kuishangalia timu ya upinzani au kuamua kujing'atua uwanjani pole pole!
Bila ya shaka hadi hivi sasa hakuna shaka ni serikali gani tunayo mkononi, tunafahamu kwa hakika kuwa sera yao ya kulindana bado inaendelea, wako pole pole kushughulikia masuala ya mustakabali wa Taifa, na kwa hakika hadi hivi sasa hawana kipaumbele cha utendaji! Serikali haiwezi kufanya kila kitu kwa kiasi kikubwa ndani ya muda ule ule isipokuwa mpaka ichague kipaumbele na kipi kitangulie. Kama ni miundo mbinu, elimu, afya, madini n.k serikali makini ni lazima ijue inataka kuweka msisitizo wapi. Haiwezekani hata kidogo kumridisha kila mtu kwani matokeo yake hakuna atakayeridhika.
Waswahili walisema "panya wengi hawachimbi shimo refu". Maana ya msemo huo inashabihiana kabisa na ile "law of diminishing returns" ambapo inafika mahali faida inazidi kupungua pale vitu fulani (variables) vinazidi kuongezwa. Kwa kuongeza wakulima zaidi kwenye shamba la ekari moja haina maana mavuno yataleta faida zaidi! Kwa jinsi serikali yetu inavyokwenda nina uhakika tumefikia mahali pa diminishing returns na hatuna budi kupunguza vitu fulani.
Tupunguze vitu vya kufanya ndani ya miaka mitano ya mwanzo (sasa mitatu iliyosalia). Rais Kikwete na timu yake wake chini na kuingalia Ilani ya CCM na waamue kwa dhati ndani ya miaka mitatu iliyobakia ni nini kitatiliwa kipaumbele ili ifikapo 2010 angalau vitu hivyo viwe vimefikiwa angalau asilimia 95 ya malengo yake. Kwa kufanya hivi napendekeza kuwa na vipaumbele vya aina mbili.
a. Vipaumbele vya Msingi. Hivi ni vipaumbele ambavyo ni lazima serikali yoyote ihakikishe vinaendelezwa kila mwaka. Vipaumbele hivi vinahusu huduma za jamii (afya, elimu, na maji); vipaumbele vya Usalama (majeshi, ulinzi n.k) na vipaumbele vya miundo mbinu (barabara, umeme, simu n.k).
b. Vipaumbele vya Kati: Hivi ni vipaumbele ambavyo kila serikali inafanyia kazi kwa kadiri ya inavyochaguliwa. Mara nyingi vipaumbele hivi vinafuata sekta maalumu au eneo maalumu la kiuchumi. Lengo la vipaumbele hivi vya kati ni kufikia vipaumbele vya msingi. Maeneo ambayo serikali inaweza kuyatilia maanani katika sehemu hii ni vitu kama : Ubadilishaji wa sheria, utungaji wa taratibu, usimamizi na uchunguzi wa mambo fulani n.k Hivyo masuala kama ya mikataba n.k yangeweza kutiliwa maanani mara moja kwa kubadilisha taratibu na sheria na kufanya uchunguzi ili vipaumbele vya msingi viweze kufanikiwa pasipo matatizo.
Tatizo tulilonalo sasa ni kuwa watawala wetu wanajaribu kufanya mambo mengi kwa muda mfupi kwa kutumia watu wengi zaidi. Hili kwa hakika itakapofika 2010 tutajikuta hatujafanya mengi. Kwa vile watawala wetu wanajaribu kuridhisha kila mtu na kwa maneno yao mengi wanajaribu kufanya kila wawezalo kuonesha wako ontop of everything, na kwa sababu siamini hata kidogo kuwa wataweza kufanya yote waliyoyasema na kuyaahidi, nimeamua kuweka manyanga chini hasa katika suala la kuikosoa serikali.
Nimeamua na mimi kuungana na wale watafutao yale mazuri ya serikali na kuyapigia mbiu na kuyatangaza! Nimekubali yaishe... Nimekubali kuwa wao ndio watawala na walichaguliwa kwa asilimia 80, wanapendwa na wananchi na wanakubalika kutawala miaka mingine hamsini ijayo... kama walivyosema wengine "kama huwezi kuwashinda, jiunge nao".
CCM here I come, naomba kadi au ukada wa aina fulani....