Tukitaka kodi ya SIMcard ifutwe tufanye hivi

Tukitaka kodi ya SIMcard ifutwe tufanye hivi

wakuu,

naona tunatumia muda mwingi kusign hizi petition ambazo hazina athari zinazotakiwa. Nilipokuwa masomoni marekani, nilifundishwa mbinu moja nzuri ya uanaharakati, lakini nawamegeeni hizi mbili, muweze kuzitumia kufanikisha lengo kuu.


hit your enemy where it hurts the most: His pockets!

tafsiri yake ni kwamba "mpige adui yako mahali ambapo ataumia zaidi: Kwenye mifuko yake." tafsiri fupi ni kwamba, kama ana mapato, tafuta njia ya kumnyima mapato, kumtia hasara kubwa, ikiwezekana, mfilisi kabisa. Kwa hili tufanyeje? Badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari na kusign petition, tunachopaswa kufanya ni kuendesha mgomo baridi wa hata saa 24, kwa kuzima simu zetu za mkononi. Matumizi ya simu hizi, kisheria, na kibiashara, ni kwamba, mteja anaponunua line ya simu (sim card) na kupewa namba ya simu ya mtandao wowote ule, anakuwa na hiari ya kutumia au kutotumia simu yake hiyo, na wala hapangiwi kiasi cha fedha anachopaswa kutumia. Kutumia aku kutotumia ni hiari yake; halazimishwi.

Hebu fikirieni, iwapo wakazi wa jiji la dar es salaam, tena wale ambao wana kipato cha chini ambao ndio wenye matumizi makubwa zaidi, kwani mapato ya hizi kampuni za simu hupatikana zaidi kwenye sms, na watumiaji hawa ni wengi zaidi kuliko matajiri, waamue kusitisha kutumia simu zao kwa saa 24 hadi 48, hasara watakayoipata wamiliki wa kampuni za simu itakuwa kubwa namna gani? Kampuni hizi zimeingia ubia haramu na serikali yetu wa kuwanyonya watanzania ambao wengi wao tayari ni maskini, ambao wengi wao kipato chao hakitoshi hata mlo mmoja wa siku. Ni ajabu walidunduliza miaka ngapi hadi kupata uwezo wa kununua hizo simu zao za mkononi, kisha kununua line, na leo serikali inakuja na kodi ya kinyemela kuwatoza shs. 1,000 kwa mwezi? Dharau iliyoje? Basi na sisi (najua nitaitwa mchochezi lakini hizi ni harakati) tuwagomee huduma yao hii, kwa hizo saa 24 hadi 48. Najua wataleta vitisho kwamba kila atakayezima simu yake atafungiwa line yake hiyo, lakini hizo zitakuwa ni nguvu ya soda, kwani hakuna kampuni ya simu hata moja ya kuifungia line yoyote ile iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria, epoca, kwani sasa line hiyo ni chanzo cha mapato kwa serikali.

Kampuni hizo haziwezi kukiuka mkataba wake na serikali; tuzitie adabu, tuzitie hasara. Adabu isipotosha, mgomo huo (boycott) unarudiwa, mpaka serikali na wabia wake haramu washike adabu, na waiondoe kodi hiyo haramu. Kwani wamiliki halali wa nchi hii ni nani kama sio sisi watanzania, tena wanyonge, masikini, tulio wengi? Kwani viongozi wetu wanaolilia kututawala huja kuomba kura kwa nani wakati wa uchaguzi, kama sio kwetu sisi, ambao ndio tunaowapa dhamana hiyo ya kutwaa madaraka? Sasa cha kuogopa ni nini? Tukijipanga vizuri, tutafanikiwa. Hakuna kuogopa, zama hizo zimepitwa na wakati. Hata hivyo, kususia kutumia huduma hii ya simu sio kosa la jinai! Ni hiari! Tujipange! Inawezekana!



put his dirty laundry out in the open!
tafsiri ya mbinu hii ya pili ni "anika nguo zake chafu hadharani!" tafsiri fupi ni "anika siri zake za uhalifu/ufisadi hadharani". Kwa lugha ya kiingereza, "dirty laundry" ina maana ya "uhalifu/ufisadi". Tukubali ukweli. Hakuna asiye na siri. Kampuni hizi za mawasiliano ya mkononi zimekuwa zikiwaibia (pasi na kuwa na ushahidi wa jinsi wanavyoibiwa) wateja wake kuwa miaka lukuki. Waajiriwa kwenye kampuni hizo, ambao ni watanzania wenzetu, wamekuwa (kutokana na njaa zao) wakirubuniwa kushiriki kwenye wizi huu, pasi na kujua kwamba huu ni unyonyaji mkubwa kwa watanzania, wengi wao ambao ni maskini.

Watanzania wengi wamekuwa wakilalamika jinsi pesa zao zinavyokatwa kinyemela pasi na kuwa na maelezo kwa sababu gani mambo haya yanafanyika. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watendaji katika vyombo husika vya kusimamia sheria husika nao wameingizwa mtegoni, kwa kupewa ruzuku lukuki (bahasha za khaki), ambapo, kwa mfano, wanaposafiri nje ya nchi, hupangiwa masurufu makubwa ambayo kampuni hizi huhesabu kuwa "gharama ya uendeshaji kampuni ya ziada", au "overhead"/ hapa tunahitaji kuwabembeleza watanzania wenzetu wanaofanya kazi kwenye kampuni hizi kuwa wazalendo zaidi, na kutufunulia uchafu wote unaofanywa na kampuni hizi, kama ilivyofanyika kwa kampuni ambayo imekuwa ikiliibia taifa kwenye mapato ya matumizi ya umeme kwenye minara yake ya kurushia mawimbi, zaidi ya 1,700, na kusababisha hasara ya zaidi ya bilioni 119 kwa mwezi! Sasa harakati na ziendelee.

Tuanike nguo zao chafu hadharani, kila mtu azione: Tuifanye thamani ya kampuni zao iwe ndogo kabisa, kiasi kwamba wezi hawa washitakiwe kwa mujibu wa sheria, ikishindikana, wauze kampuni zao kwa wafanyabiashara wengine ambao wataogopa kutuibia, kwani watatambua kwamba, kwanza, wamenunua kampuni hizo kwa bei ya "kutupa", lakini pili, watatuheshimu watanzania na kuogopa kurudia makosa ya wenzao.


Mbinu hizi mbili zinatosha. Acheni kuhangaika na hizo petition. Hazisaidii chochote. Mkitaka ushauri wa jinsi ya kuratibu harakati hizi, nitawapa, lakini msinipm. Sitapokea pm ya mtu yeyote kuhusu hili, kwani najua miongoni mwetu humu wamo mandumilakuwili wengi tu. Siko tayari kumwamini mtu yeyote nisiyemjua kuhusu hili. Nitaweka mambo hadharani.

Kila la heri.

A luta continua!

p.s.: moderators, nalazimika kuirudia post hii kwenye uzi wake, baada ya kuiweka chini ya post nyingine, kwa kuwa naona hata hao walioanzisha post hiyo ya kukusanya saini kupitia petition wameichoka. Nadhani wameelewa kwamba wanachokifanya hakina tija kwao.

hii imekaa kisasa zaidi ile ya petition ni siasa hainaga impact
 
Naunga mkono hoja na napendekeza tuzime simu zote kuanzia 1/8/2013 hadi 8/8/2013 kwa kuanzia. Haiwezekani waachie kodi migodini na watoze kodi laini za simu. CCM mbulula 100%.
 
Tatizo sisi watanzania bado hatujafikia ule moyo wa kujitoa na kujitolea, kuna mtu atakumbuka hajaongea na demu wake tu, basi zoezi kwisha, tuna vibaraka watakaoshabikia nk

the bottom line (at least to me) ni kwamba makampuni ya simu yameishinda serikali, hayalipi kodi na sisi tunaadhibiwa kwa kuwa na simu

TRA and other law enforcement agencies zimeshindwa kutimiza wajibu na sasa tunakamua maskini
 
wizara zifuatazo ya fedha, habari, pamoja mawasiliano lazima wafikiri upya namna ya kuwaelimisha watu kuhusiana na kodi hii mpya ili wananchi wawe wameandaliwa na sio kukurupushwa kulipa ili kuepusha uchochezi ulioanza kufanywa na watu wenye mlengo wa kujenga chuki na jazba miongoni mwa watu na mamlaka halali
 
kuwaelimisha ili wakubali kuzilipa au kuziondoa, sijaelewa!
 
pole sana mleta mada, walioipitisha wenyewe waanza kuipinga, sasa wewe ushaanza kuushambulia upinzani. Pole sana.
 
Elimu tumeshaipata itakua ni kuanzia agosti 19 ni kuzima simu zote za mkononi Tanzania
 
Elimu tumeshaipata itakua ni kuanzia agosti 19 ni kuzima simu zote za mkononi Tanzania

Tuwaonyeshe kwamba tunaweza na tunastahili kuheshimiwa kama wananchi wa nchi hii! Nchi hii si mali ya watawala pekee bali ni ya watanzania wote na kile ambacho watawala wanakifanya ni lazima kiwe na manufaa kwa wananchi.
 
wizara zifuatazo ya fedha, habari, pamoja mawasiliano lazima wafikiri upya namna ya kuwaelimisha watu kuhusiana na kodi hii mpya ili wananchi wawe wameandaliwa na sio kukurupushwa kulipa ili kuepusha uchochezi ulioanza kufanywa na watu wenye mlengo wa kujenga chuki na jazba miongoni mwa watu na mamlaka halali

Nafikiri wangeanza na Nape Nnauye kwa sababu na yeye nasikia amesema hazifai.
 
Last edited by a moderator:
Msisahau kwenda kutupoa sahihi zenu hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...la-mwezi-kufuatia-mabadiliko-ya-sheria-8.html ili tunalize kesi kwa njia zote

Petition ni kupoteza muda mkuu! Inamtia nani hasara? Ukimnyima mtu mapato unamtia hasara, unamfunza adabu, heshima inarudi! Au hujui msingi wa biashara ni mapato? Si wanafanya biashara? Basi tuwaoneshe UCHUNGU watakaoupata baada ya kupoteza mapato, hata kama ni kwa siku moja tu.

Ngoja nikudadavulie kidogo jinsi watakavyokula hasara:

1. Watakosa mapato kwenye ujumbe mfupi (SMS)
2. Watakosa mapato kwenye miito ya simu (caller tunes)
3. Watakosa mapato kwenye makato (commissions and service charges) ya utumaji na upokeaji wa pesa
4. Watakosa mapato kwenye upigaji wa simu (voice calls)
5. Watakosa mapato kwenye makato (percentage) ya Shs. 1,000 ya kodi ya serikali ya umiliki wa SIMcard
6. Serikali itakosa mapato kwenye makato mengine ya kodi, kwa mfano, kodi ya mapato (Income Tax) pamoja na Kodi ya Nyongeza ya Thamani (VAT) ambazo zinatozwa na Serikali. (Kama mtu hanywi soda, Serikali haikusanyi mapato. Kwa hiyo, kama mtu kazima simu, hivyo hivyo!)


Usiudharau muda. Japokuwa saa 24 zaonekana kuwa chache, hiyo ni SIKU NZIMA. Hebu fikiria kama watu wangegoma kwenda kutumia huduma za benki, kwa muda huo, nchi nzima? Ni biashara kiasi gani ambazo benki zingekosa kwa muda huo? Mgomo wa aina ya "kususia" (boycott) hauna madhara ya kutafutwa na askari polisi, kwani hauvunji sheria. Unapokataa kutumia huduma au bidhaa fulani, unapoisusua, kwa kuwa UNAILIPIA huduma, SI KOSA LA JINAI wala MADAI kwa kuwa ni HIARI YAKO kwa 100%, kuchagua kutumia au kutotumia huduma na/au bidhaa hiyo.

Kumbuka, kutatokea vitisho na vishawishi vingi sana. Tayari kampuni moja ya simu imeanzisha kishawishi cha kuwafanya Watanzania waamini kwamba wanaweza kushinda Bajaj mpya kila siku, kama mpango wa kukabiliana na harakati hizi. Tujiulize: Ziko Bajaj ngapi, na je, shindano/promosheni hiyo itaendeshwa kwa muda gani? Kisha tujiulize: Washiriki wa mgomo huu wako wangapi? Je, washiriki wote hawa wanaweza kupewa/kushinda hizo Bajaj wasishiriki kwenye harakati hizi? Sasa unajua kwamba, hata kabla ya tarehe husika kufika, WALENGWA wa harakati hizi wameanza KUOGOPA SANA, kiasi kwamba wanakuja na mipango yao ya danganyatoto. Unapoingia kwenye harakati lazima ujifunze kutambua vishawishi na vipingamizi vinavyoweza kukukatisha tamaa usifanikiwe kwenye harakati zao.

Sisi tuna mpango wa kufanya harakati za amani, ambapo walengwa ni watu ambao HAWANA HATA CHEMBE YA HURUMA kwetu sisi wateja wao, na halikadhalika, kama wateja, HAWATUHESHIMU. Tunaibiwa kwa kukatwa pesa tunazotumia bila mpango. Ukiona kwamba bidhaa/huduma unayonunua inakuumiza, kwa nini uendelee kuumia TENA KWA PESA YAKO MWENYEWE?

Nadhani sasa umenielewa!
 
Mnachekesha kweli nyie.

Mnaijua 80-20 rule?

Kwa taarifa yenu mapato ya kampuni za simu kama Zantel, Airtel na Voda 80% ni kutoka kwa Corporate clients wao na sie wengine akila baba Zabosi ndio tunachangia hiyo 20% sasa hata tukizima sisi simu sitegemei kama mabenki yatazima simu zao, au ofisi za serikali watazima simu zao, wabunge watazima simu zao, makampuni makubwa yatazima simu zao. Na mtu yeyote mwenye shughuli za kumpatia kipato lazima anahitaji mawasiliano hawezi kusima simu yake hata kwa dakika 30.

Sana sana huo mgomo wenu utawaumiza wakina mangi wanauza vocha na kutoa huduma za Tigo/M-pesa

Hayo mabenki nayo kama yanatuletea ujinga tutapitisha azimio la kuto kwenda benki na pesa zetu tutaweka mchagoni kama wazee wetu walivyofanya huko nyuma potelea mbali liwalo na liwe tu bwana.Tumechoka sasa na tozo hizo.
 
Mbona kama hapo una sound kama kirusi? ungeomba tu kwamba isiunganishwe, kwanza njia yako unajua ni ngumu kutekelezeka ivyo unafanya JOKES ya mambo muhimu, watu watazima vipi simu na ndio maisha yenyewe ?
Halafu hata ujapiga mahesabu kwa welezi kwa kampuni za simu zinapata pesa wakati wa ununuzi wa vocha au wakati wa matumizi?
sio kwamba ukinunua vocha tu hela yao ina clock? sasa ukizima simu wao inawaumiza vipi na vocha umeshanunua? na wao watasaidia vipi kuondoa hii sheria? dawa ni kusaini hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...la-mwezi-kufuatia-mabadiliko-ya-sheria-8.html kisha wabunge wazalendo wafanye kazi, na hakuna sababu za kupingana kama unavyotaka kufanya as if njia inatakiwa iwe moja tu
POSHO MAVYEO


Naona hujaelewa vizuri ni lengo kuu la harakati hizi, haswa lengo la kuwanyima mapato wawekezaji uchwara hawa. Sasa kabla ya kukudadavulia kuhusu suala la “mapato”, ngoja nikudadavulie jinsi ambavyo “wawekezaji uchwara” hawa wanavyotuibia (LAKINI MAJIBU HAYA NI KWA FAIDA YA WANAHARAKATI WENZANGU):


  1. Kwa mujibu wa sheria, kila kampuni inayomiliki mtandao wa simu za mkononi inatakiwa kuweka wazi viwango vya tozo zake, kwa sekunde na/au dakika, kwa kila simu inayopigwa, na pia gharama ya kila ujumbe mfupi wa simu unaotumwa.
  2. Tozo hizi zinatakiwa kutangazwa kwa hali ya uwazi, na zinatakiwa kutangazwa zikionesha ni kiasi gani kinatozwa kwa huduma ya ndani na nje ya nchi.
  3. Lakini kwa sasa, kama mbinu ya kuzificha, kampuni hizi zimekuja na kampeni za “bundles”, ambapo mtumiaji wa huduma hizi anawekewa kiwango ambacho hakiainishi wazi ni kiasi gani cha fedha kinakatwa, kwa sekunde au dakika. Unaambiwa kwa kiasi fulani cha fedha unapata dakika kadhaa, SMS kadhaa na MB kadhaa za Internet. Lakini umeshawahi kujiuliza ni wamiliki wangapi wa simu za mkononi wenye simu zenye uwezo wa kutumika kwenye Internet? Sote tunajua kwamba ukitaka kutumia huduma ya Internet kwenye simu yako, lazima uwe na “smart phone”, na wamiliki wengi wa simu ni wenye uwezo mdogo wa kifedha, ambao wananunua simu za Kichina, ambazo nyingi – kutokana na kuwa na gharama ndogo – hazina uwezo huo. Sasa hapo kumwambia mteja anapata MB kadhaa za Internet wakati hazitumii ni sawa na kumwibia. Huwezi kumwuzia mtu huduma ambayo haitumii.
  4. Sisi wateja HATUNA UWEZO wa kufuatilia iwapo kweli kile ambacho kinatangazwa kuwa tozo za huduma hizi ndicho haswa tunachokatwa. HATUNA!
  5. Wakala wa Kudhibiti Mawasiliano (TCRA) ilitangaza zabuni ya kimataifa, ambapo kampuni yenye teknolojia hiyo ingepaswa kuja kufunga mitambo ya kufuatilia kiwango halisi kinachokatwa na kampuni hizi kwa wateja wao. Lakini kwa kuwa kampuni hizi zina “ushawishi” mkubwa kwa watendaji wa TCRA, zabuni hii – kama mipango mingine mizuri inayopangwa hapa nchini – ilitoweka katika mazingira ya kutatanisha. Wenzetu nchini Uingereza wanayo huduma hii; hakuna kampuni inayothubutu, wala yenye uwezo wa kuwaibia wateja wake.
  6. Kwenye suala la utumaji na upokeaji pesa, hapa ndipo KILIO KIKUBWA cha wananchi kinapotoka. Wengi wamepoteza pesa nyingi katika utumaji, upokeaji na hata uhamishaji wa pesa kutoka kwenye akaunti zao za benki kwenda kwenye akaunti zao za simu.
  7. Utakuta mtu ana dharura, kutokana na muda au mahali anapokuwa kwa wakati huo, hawezi kwenda benki aku kwenye mashine ya ATM. Pengine kuna mgonjwa anahitaji kupelekwa hospitali – ugonjwa huwa hautoi taarifa – yeye mwenyewe yuko mbali na nyumbani, kwa hiyo anahitaji kutuma fedha hizo haraka nyumbani. Anahitaji kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti yake ya benki, kwenda kwenye akaunti yake ya simu, kwa mfano, kutoka SIMbanking ya CRDB kwenda M-PESA ya Vodacom. Anaingia kwenye sehemu ya SIMbanking kwenye simu yake, inamuunganisha na akaunti yake, anahamisha kiasi cha pesa kutoka kwenye akaunti yake ya CRDB kwenda kwenye akaunti yake ya M-PESA. Taarifa ya muamala huo inamwambia kwamba amefanikiwa kuhamisha kiasi alichotaka cha fedha; anahakiki salio lake kwenye akaunti, linamthibitishia kwamba pesa hizo zimekatwa.
  8. Sasa kilichobaki ni kusubiri taarifa kwenye simu yake kwamba pesa zimeingia kwenye akaunti yake ya M-PESA; anakuwa na uvumilivu, wa kusubiri, dakika tano… nusu saa… saa moja… saa mbili… siku nzima (hali ya mgonjwa ilipozidi kuwa mbaya, nyumbani walikopa pesa kwa jirani)! Pesa hazikuhamishwa kutoka kwenye akaunti ya benki kwenda kwenye akaunti ya simu; na matukio kama haya yametokea kwa watu wengi. Wanapofuatilia kwa kupiga simu kwa kitengo cha Huduma kwa Wateja (Customer Service), wanaopokea wanatupa mpira kwa wahusika wa benki. Wakiongea na benki, wanawarudisha huko kwenye mtandao… ili mradi hakuna anayekubali kuwajibika. Wakati huo, hakuna mwenye maelezo fedha zimekwenda wapi.
  9. Sasa hebu fanya hesabu; kama, kwa mfano, watu 100,000 wamepoteza kati ya Shs. 20,000 hadi 100,000 na zaidi, kila mwaka, kwa miaka kumi iliyopita, je, ni kiasi gani cha pesa kimepotea katika mazingira haya, ambayo dhahiri ni wizi?
  10. Sasa umenielewa kuhusu jinsi ambavyo tunaibiwa; sasa tuongee suala la mapato.

Kampuni hizi zinapataje mapato yake?


  1. Kila unapopiga simu, unakutana na mlio wa simu tofauti upande wa pili, wakati simu ikiita kabla ya kupokelewa. Mlio huu unaitwa “caller tune” au “mwito wa simu”. Mmiliki wa simu unayoipiga anakuwa amelipia huduma hii, ambayo, wakati mwingi, bila ya yeye mwenyewe kujua, anakatwa malipo ya takriban Shs. 30-50 kila siku, jambo ambalo mara nyingi haliwekwi wazi na kampuni hizi. Kutokana na matangazo ya huduma hii, watu wengi “huingia mkenge” na kujiunga, na hushtuka pindi wanapogundua kwamba wameingia kwenye mkataba ambao hawakutaka, na inawachukua muda mrefu kujiondoa kwenye huduma hiyo. Hiki ni chanzo kimojawapo cha mapato.
  2. Kila unapofanikiwa kuunganisha mawasiliano yako unapopiga simu, unalipishwa huduma hiyo kwa sekunde au dakika, na huna uwezo wa kujua KWA UHALISI ni kiasi gani umelipwa. Wakati mwingine unaweza kuongeza salio na kutaka kujiunga na mojawapo ya huduma za “bundle”. Unaweka kiasi cha pesa unachotaka, unalipia “bundle”, unapata ujumbe kwamba umefanikiwa kununua muda wa sekunde 600 (ambazo ni sawa na dakika 10). Lakini unapojaribu kupiga simu unaambiwa, huna salio la kutosha. Dakika ulizolipia zimekwenda wapi? Hiki ni chanzo kingine cha mapato.
  3. Kila unapofanikiwa kutuma ujumbe mfupi wa simu, unakatwa kiasi Fulani cha fedha, iwe umejiunga na “bundle” au la; tena unakatwa bila taarifa yako. Hiki ni chanzo kingine cha mapato.
  4. Kila unapotuma fedha kupitia akaunti yako ya fedha ya simu yako unakatwa kiasi Fulani cha fedha. Kwa mfano, ukituma Shs. 10,000 unakatwa Shs. 1,000 kama ada ya huduma ya kutuma fedha kwa kiasi hicho; hii ni kwa mtandao wa Vodacom kupitia huduma ya M-PESA. Hiki ni chanzo kingine cha mapato.
  5. Kila unapolipia huduma yoyote ile unayoitumia, kwa mfano, Ankara ya Maji, Ankara ya Kisambuzi (Startimes, ZUKU, etc.), Tiketi ya Ndege, Ada ya Shule, n.k., unakatwa kiasi Fulani cha fedha, ikiwa ni ada ya huduma hiyo. Hiki ni chanzo kingine cha fedha.

Mpaka sasa nimekudadavulia vyanzo 5 vya makato na mifano kama hiyo ya jinsi tunavyoibiwa.

Sasa nakujibu hoja zako moja baada ya moja:


  1. “Halafu hata ujapiga mahesabu kwa welezi kwa kampuni za simu zinapata pesa wakati wa ununuzi wa vocha au wakati wa matumizi?”
Hili nimeshajibu.

  1. “sio kwamba ukinunua vocha tu hela yao ina clock? sasa ukizima simu wao inawaumiza vipi na vocha umeshanunua?”
Hata kama umeshanunua vocha, thamani yake haitumiki MPAKA unapoiweka kwenye simu yako na kuitumia. Usipoitumia hawapati mapato.

  1. “na wao watasaidia vipi kuondoa hii sheria?”
Kampuni hizi zimesaini mkataba na serikali kuwa wakala wa kukusanya mapato kwa serikali, kuanzia na kodi hii. Kodi hii inakatwa wakati unapotumia simu yako, kwa takriban kiwango cha Shs. 33 kwa siku. Watu milioni 10 wakishiriki kwenye mgomo hii kwa siku, hiyo ni sawa na Shs. 330,000,000 ambazo serikali inakuwa imeshindwa kuzikusanya kwa siku hiyo. Kama mgomo ni wa siku 3, serikali inakuwa imeshindwa kukusanya Shs. 990,000,000 kwa muda huo. Uwakala wao unakuwa hauna faida kwa serikali.

  1. “dawa ni kusaini hapa Petition: Wito wa kusitisha tozo/kodi ya laini ya simu kila mwezi kufuatia mabadiliko ya sheria kisha wabunge wazalendo wafanye kazi”
Tangu lini umewaona “wabunge wazalendo” wakifanya kazi? Ipi? Kwa mafanikio yapi? Hiyo petition ni sawa sawa na – ashakum si matusi – karatasi ya kuchambia msalani, kwani haina mashiko. Lengo hapa ni kutoa “athari hasi” (negative effects), ambazo zinamfanya mlengwa kuhamaki na kusema: Kumbe hapa ninapata hasara? Ulimwona wapi mfanyabiashara anayekubali kupata hasara kwa sababu za kijinga?

  1. “hakuna sababu za kupingana kama unavyotaka kufanya as if njia inatakiwa iwe moja tu”
Sijasema njia iwe moja tu: Ziko njia nyingi, nimeanzia na njia ambayo italeta mafanikio yanayotakiwa kwa ufanisi mkubwa zaidi, kwa haraka zaidi. Kama ulisoma pendekezo la pili, utatambua kwamba pendekezo hilo ni la kuendelea. Njia ziko nyingi, lakini hili la petition na kwenda kuandamana kama Mnyika anavyotaka kufanya ni kupoteza muda na kuwafanya Watanzania kupigwa virungu na kujeruhiwa na Polisi, bure tu. Wanapoumizwa na kupelekwa hospitali, Mnyika ataenda kuwatibia wote?

Ndugu yangu, mimi ni mwanaharakati, nimefundishwa mbinu hizi nilipokuwa Marekani. Kama wewe unaona kusaini petition ni njia sahihi, endelea, lakini tuache sisi tuendelee na mpango wetu huu. Au umetumwa kutudadisi?

Huwezi kutuvurugia kwa kuwa tayari najua KILA RESPONSE ya watu kama wewe. Ni dhahiri umetumwa, la sivyo usingeshabikia nitake kuelezea jinsi tunavyoibiwa na jinsi tutakavyowakosesha mapato. Nimekujibu pia kwa faida ya wanaharakati wenzangu kama nilivyotamka mwanzo kabisa wa majibu yangu haya.

Kwa leo nimemalizana na wewe. Kila la heri.
 
Last edited by a moderator:
kuwaelimisha ili wakubali kuzilipa au kuziondoa, sijaelewa!

omujubi maulize wanaoelewa zaidi yako, utaelimishwa. Au soma post yangu mpya niliyoiandika awali leo, post ya pili niliyomjibu POSHO MAVYEO, lakini pia nimeiandika kwa faida ya wanaharakati wenzangu.
 
Mwaka 2007 nchi vinara kwa kutoza kodi kubwa kwenye mawasiliano ni Turkey, Uganda, Brazil, DR Congo, Zambia, Ukraine, Ecuador , Tanzania, Greece na Kenya HIZI ZILITOZA KODI ZAIDI YA 20% ………Nchi ambazo zinatoza kodi ya chini ni Bhutan, Myanmar,
Swaziland, China, Syria, Malaysia, Angola na Lesotho, HIZI ZILITOZA KODI CHINI YA 5%
kwa ufafanizi rahisi ni kwamba kuna nchi masikini zinatoza kodi ndogo kwenye mawasiliano ili hiyo sekta ipanike, lakini kuna nchi masikini pia ambazo zinatoza sana kwenye hii sekta na kuathiri ukuwaji wake.

SAINI PETITION kusimamisha hizi kodi mpya tunalipa zaidi ya 25% mpaka sasa serikali itafute vyanzo vingine vya mapato, na ipunguze matumizi yakeWITO WA KUSITISHA TOZO/KODI YA LAINI YA SIMU KILA MWEZI KUFUATIA MABADILIKO YA SHERIA YA KODI 2013

View attachment 102787
 
pole sana mleta mada, walioipitisha wenyewe waanza kuipinga, sasa wewe ushaanza kuushambulia upinzani. Pole sana.
Msafiri Kasian wewe ni kibaraka tu. Nani aliyeipinga hii mada kama si wewe kibaraka, nduli, msaliti? Nimeushambulia wapi upinzani? Nimesema UKOMBOZI HULETWA NA WANANCHI, SI WANASIASA, na haijalishi kama wanasiasa hao ni wa upinzani au chama tawala. Kwani wote ni wanasiasa.

Hatufungamani na siasa; huu ni mkakati wa WANANCHI, ndio maana hatuna Kamati ya Uongozi wala kiongozi. Mimi ni mwanaharakati mwanzilishi, si kiongozi, ndio maana wanaounga mkono harkati hizi WOTE NI WANAHARAKATI na WOTE NI VIONGOZI. Tukianza kuleta siasa kwenye harakati daima hatutafanikiwa. Kwenye ukombozi wa Tanzania, KILA MTU ANAYEUNGA MKONO HARAKATI ni MWANAHARAKATI PIA.

Jifunze kusoma "picha kuu", itakusaidia kuelewa nini kinachoendelea, badala ya kupokea hizo Buku 7 Lumumba na kuanza kutukejeli sisi tunaoipenda nchi yetu. Ninapenda nchi yangu, niko tayari kuifia, na KAMWE sitakuwa mwanacham wa chama chochote cha siasa, ila nitaunga mkono yeyote mwenye nia njema ya kuikomboa Tanzania!
 
Last edited by a moderator:
Change Tanzania, E Bwana Eeeee, HATUSAINI hiyo petition yenu ya kuzugia. Petition NGAPI zimefanikiwa kuleta mabadiliko?

Uzi ni ule ule. Tarehe 19-20 Agosti, SIMU ZINAZIMWA KAKA!

Baada ya Awamu ya Kwanza kufanikiwa, ziko awamu nyingine zinafuatia. Udhalimu wote utaondolewa, KAMA ALIVYOFANYA MWALIMU NYERERE. Hatuwezi kuwaalika wawekezaji halafu wanakuja kutufilisi! HUU NI UKOLONI!

Usiogope. Hizi ni rasharasha, masika bado.

Umenisoma?
 
Change Tanzania, E Bwana Eeeee, HATUSAINI hiyo petition yenu ya kuzugia. Petition NGAPI zimefanikiwa kuleta mabadiliko?

Uzi ni ule ule. Tarehe 19-20 Agosti, SIMU ZINAZIMWA KAKA!

Baada ya Awamu ya Kwanza kufanikiwa, ziko awamu nyingine zinafuatia. Udhalimu wote utaondolewa, KAMA ALIVYOFANYA MWALIMU NYERERE. Hatuwezi kuwaalika wawekezaji halafu wanakuja kutufilisi! HUU NI UKOLONI!

Usiogope. Hizi ni rasharasha, masika bado.

Umenisoma?


zote zifanyikwa kwa pamoja hakuna mbaya, mishale yote ina lengo moja, soma maana ya petition , Misri wamemtoa mosri kwa kusaini petition jeshi likaona waliosaini ni wengi kuliko waliompa kura wakamtoa, hata kama ni siasa kama unavyosema kwa siasa ni nini? siasa ndio kila kitu kama kuna hoja watakubali tu
 
Back
Top Bottom