Tukio zima la wachawi wawili waliodondoka na ungo huko kahama- shinyanga..

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,128

WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI MWAJUMA MPONI (70) NA KULIA NI SHIJA NKWABI (80)

Watu wawili wamenusurika kuuwawa usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Mhongolo wilaya ya kahama mkoani shinyanga, baada ya kukutwa katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya kishirikina.

Watu hao waliojitambulisha kwa majina ya Mwajuma Mponi (70) wa Nduku, na Shija Nkwabi(80) wa Nyashimbi wilayani humo, wameanguka kijijini hapo wakitokea kijiji cha nduku wiyani humo wakielekea Nyihogo Kahama kwa shughuli za kishirikina.

Katika maelezo yao wazee hao wamedai kuwa wameanguka baada ya kutokea ajali ya kishirikina huko angani, ambapo waligongana na wenzao ambao hawakuwafahamu walikotoka na walikokuwa wanaelekea.

Sambamba na hayo imeelezwa kuwa wazee hao walikuwa uchi wakati wakianguka kabla ya kusaidiwa nguo na mama mmoja wa maeneo ya Kafe Latino barabara ya Mhongolo.

Jeshi la Polisi la Wilayani humo likiri kutokeakwa jambo jambo hilo na kwamba uchunguzi bado unaendelea na taarifa zitatolewa baadaye.

DSC00867.JPG

WAZEE WAKIWA HOI KITUOP CHA POLISI BABADA YA KUFIKISHWA KITUONI HAPO

DSC00869.JPG

WAZEE WAKIWA HOI,HUKU WA KUSHOTO AKIWA ANATEMA MATE OVYO KITUONI HAPO.

DSC00868.JPG

DSC00870.JPG

DSC00871.JPG

HAPA AKITEMA MAPOVU HUKU AKISEMA ANA NJAA SANA.

DSC00872.JPG

BIBI AKIWA AKIWA HOI BAADA YA KUDONDOKA USIKU WA LEO

164252_509851619071141_1546826640_n.jpg

HAPA BIBI AKISAIDIWA KUINUKA BABADA YA KUVALISHWA NGUO NA WASALIMIA WEMA.

mabibi.jpg

ASKARI POLISI WAKIWASAIDIA KUWAPANDISHA KWENYE GARI.

532183_509851902404446_798666857_n.jpg

HAPA WAKIPELEKWA KITUO CHA POLISI

DSC00876.JPG

MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MAJIRA PATRICK MABULA AKICHUKUA MAELEZO TOKA KWA MASHUHUDA WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO.

DSC00879.JPG

HAPA NDIPO ENEO AMBALO WACHAWI HAO WALIPODONDOKEA.
 
Juzi tu hapa kuna msanii alikuja hapa JF huku akitokwa na povu kudai kuwa hakuna uchawi duniani. Huu ni uthibisho tosha kabisa kwake. Wachawi walivyokuwa wapumbavu, mchana hawa wazee wanajifanya wagonjwa na kutembea hawawezi ila usiku wanakimbia marathon kukimbiza watoto mitaani kwa ajili ya misukule ili wakawalimie mashamba. Ah kweli duniani kuna mambo!
 
I don't believe this. Huu ni upuuzi. Kwani lazima wachawi wawe wazee Peke yao?. Hivi hakuna wachawi vijana. Hivi sisi tuna matatizo gani ya akili ya kufikiria.
 
Jamani hivi Serekali iko wapi Wazee wanadhalilishwa namna hii. Sisi tutapata Laana sisi. Jamani, jamani. Hiki ni nini jamani. Yaani katika nchi hii Ukizeeka tu, inakua laana?. Jamani. Kwani Uzee ni kilema?
 
Hivi ina maana trffic huko juu ya hawa wanasayansi ni kubwa hadi kuwa na ajali??? Ni wakati mwafaka wakaanza kuwa na jeshi la trffic polisi kwani matukio ya hii midondoko yanakuwa mengi sasa!! Mara Tabata, mara Bariadi......
 
Hii picha ya mahali walipodondokea ni kama grocery; je ina maana mambo ya LAGER ni antii-uchawi??? Nafikiria tuu
 
Jamani hivi Serekali iko wapi Wazee wanadhalilishwa namna hii. Sisi tutapata Laana sisi. Jamani, jamani. Hiki ni nini jamani. Yaani katika nchi hii Ukizeeka tu, inakua laana?. Jamani. Kwani Uzee ni kilema?

kwani wao wamejielezaje? ninachojua mchawi anaweza kuwa hata mtoto mdogo sana!
 
Kwa kuanzia, hizi picha ni udhalilishaji tuu usio na msingi!.

Binadamu akishafika umri wa miaka 65, anapata tatizo la "memory loss" na " high state of mind incapacitation!", anaweza kufanya lolote, asikumbuke chochote hadi kutembea bila nguo, na akiulizwa hana jibu lolote!.

So far katika tukio lote hilo, hakuna any proof ya ushirikina wowote, na thank God, watu hawakuwadhuri, na badala yake wamewasetiri na kuita polisi kuwaokoa!.

Mpiga picha sio profession katika tasnia ya habari, kwa kuleta baadhi ya picha za kudhalilisha utu wa mtu!, kama zile za kutema mate!.

Uchawi upo ila ni kwa anayeuamini tuu!, ukiwa huamini, then uchawi haupo na hauwezi kukufanya chochote!.
Mimi ni miongoni mwa wasio amini kabisa uchawi, na silogeki!, na sio uchawi tuu, ukijiaminisha hata maleria hakuna, maleria haikupati hata mbu wakuume vipi!, mimi ni mwaka wa 20 sasa, siujui ugonjwa wowote, ukiondoa ajali iliyonipata, sijawahi kwenda hospitali kwa kuugua chochote!, na kama binadamu, kuna wakati nilishacheza michezo ya hatari kwenye "grid ya taifa" na sikunaswa na "umeme!", hivyo ukijiaminisha kisawasawa, unaweza kushika live waya wa umeme na usirushwe wala usinaswe!.

Pasco.
 
Acha upotoshaji!
 
kuamini au kutokuamini uchawi siyo issue sana, ila nasikitika kuwa hizi picha zinaonyesha wahusika ni wazee, hii inaweza kuwa ni justification kuwa wazee ndio watuhumiwa wakubwa na isadikike kuwa wazee ndio wachawi na wazidi kuuwawa!
Hivi hawa wabibi si wameanguka toka angani "baada ya ajali ya kugongana huku juu", how comes sioni majereha au damu kutoka?, hakuna kuvunjika hata mguu? Walikuwa anga gani ya karibu kiasi hicho hata wasivunjike mguu "kwa uzee wao"? Isije kuwa mwenye Grocery amewatengenezea fitina just wanasumbua wateja wake kwa ombaomba!
 
Kwa kuanzia, hizi picha ni udhalilishaji tuu usio na msingi!.

Binadamu akishafika umri wa miaka 65, anapata tatizo la "memory loss" na " high state of mind incapacitation!", anaweza kufanya lolote, asikumbuke chochote hadi kutembea bila nguo, na akiulizwa hana jibu lolote!.

So far katika tukio lote hilo, hakuna any proof ya ushirikina wowote, na thank God, watu hawakuwadhuri, na badala yake wamewasetiri na kuita polisi kuwaokoa!.

Mpiga picha sio profession katika tasnia ya habari, kwa kuleta baadhi ya picha za kudhalilisha utu wa mtu!, kama zile za kutema mate!.

Uchawi upo ila ni kwa anayeuamini tuu!, ukiwa huamini, then uchawi haupo na hauwezi kukufanya chochote!.
Mimi ni miongoni mwa wasio amini kabisa uchawi, na silogeki!, na sio uchawi tuu, ukijiaminisha hata maleria hakuna, maleria haikupati hata mbu wakuume vipi!, mimi ni mwaka wa 20 sasa, siujui ugonjwa wowote, ukiondoa ajali iliyonipata, sijawahi kwenda hospitali kwa kuugua chochote!, na kama binadamu, kuna wakati nilishacheza michezo ya hatari kwenye "grid ya taifa" na sikunaswa na "umeme!", hivyo ukijiaminisha kisawasawa, unaweza kushika live waya wa umeme na usirushwe wala usinaswe!.

Pasco.

MB haya bana but duniani pana yanayoonekana na yasiyoonekana, uchawi na wachawi wala hii si kuamini bali ni mambo ya duniani. Hv hawa wanaoitwa misukule wanatokana na nn? Hata Bible inasema ole wao wachawi.
 
Back
Top Bottom