Jeshi la Polisi lapiga marufuku Kamchape (Lambalamba), kuwasaka wote wanaohusika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,555

/
IMG_8477.jpeg
Hivi karibuni kumejitokeza wat wanajulikana kama Kamchape au Lambalamba wanaoendekeza imani potofu za kishirikina wakiidai wanao uwezo wa kufichua wachawi kitendo ambacho ni uhalifu.Watu hawa wameitokeza na kufanya uhalifu huo katika Mikoa ya Katavi, Kigoma, Rukwa na Songwe.

Mbinu wanayotumia ili kufanikisha uhalifu huo ambao ni utapeli, wizi, udhalilishaji wa watu, ukiukwaii wa haki za binadamu,uporaji wa mali za watu, uharibifu wa mali za watu binafsi na za serikall, uzalilishaji wa watu hasa wazee na kujeruhi, kuchonganisha watu na kuchochea mauaji,ni pamoja na kuchimbia hirizi, tunguli kwenye nyumba, mashamba,mazizi ya watu usiku a kisha kwenda kuvifukua mchana na kunasibu kuwa wamefichua mchawi jambo ambalo ni uwongo na utapeli mkubwa.

Ili kuhakikisha wanafanya uhalifu huo bila kipingamizi, wamekuwa wakitafuta wafuasi wa kuwaunga mono hususani vijana ambao huwanunulia pombe, wengine kuwavutisha bhangi na kuwagawia fedha wanazopora kutoka kwa watu wanaowasingizia kuwa ni wachawi. Vijana hao wasiopenda kufanya kazi hushinikiza uhalifu huo ufanyike ikiwa ni pamoja na kuwatishia Viongozi wa Serikali za mitaa kuwa watachoma nyumba zao moto endapo watawanima kibali cha kufanya vitendo hivyo vya kihalifu. Lengo lao likiwa ni kupata maslahi yanayopatikana kutokana na vitendo hivyo vya kihalifu.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Wananchi a Viongozi wa Serikali za Mitaa, kukataa na kutowaruhusu kuanza au kuendelea kufanya uhalifu huu unaoendekeza imani potofu za kishirikina na kutuabisha kama watanzania.

Kwa vile wanayofanya hawa Kamchape/Lambalamba a Washirika wao ni uhalifu, Jeshi la Polisi linapiga marufuku vitendo hivyo a linaendelea kuwasaka na kuwakamata wote waliofanya uhalifu huo popote pale ili wafikishwe mahakamani.

Tunatoa wito kwa wananchi wote wa Mijini na Vijijini kuungana katika kuwakataa wat hawa na wafuasi wao pamoja na vitendo vyao vya kihalifu manavyofanya vya kujipatia fedha na mali kwa nia ambazo hazina baraka za kisheria.

Imetolewa na:
David A. Misime - SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu Ndogo ya Polisi
Dares Salaam, Tanzania

Pia soma: Kama wewe ni mchawi usije Kigoma kipindi hiki, Kuna operesheni kubwa sana inaendelea

Kinachoendelea Kigoma kuibua wachawi ni udhalilishaji, upuuzi na uchonganishi
 
Mbinu wanayotumia kama ya ccm, honga pombe na pesa, watishe ili wakubali. Matokeo hali kadhalika, ni wizi, udhalilishaji, kuumiza mwili na hisia, kutojali haki za binadamu. Kweli ccm chama tawala, bahati mbaya polisi haioni uhalifu wa ccm.
 
NI kwili uchawi upo, ila hawa jama, wanabambikia watu, na kuwadhalilisha tu, wakishakutuhumu wewe ni mchawi hata kama huujui uchawi wenyewe una rangi gani umekwisha.
 
Back
Top Bottom