Tukio la kushangaza la kikombe

Tukio la kushangaza la kikombe

Wakuu kuna kitu cha kushangaza kimetokea sijakielewa.

Jana jioni wakata naandaa chai (Mimi napenda kunywa chai jioni) kuna kikombe kidogo kilizama ndani ya kikombe kingine kikubwa cha udongo. Kwa namna vilivyoshikana ilikuwa ngumu sana kuvitenganisha hata nilipojaribu kwa muda mrefu sana. Hatimaye nilikata tamaa nikajisemea nitajaribu kuvitenganisha asubuhi.

Sasa cha ajabu asubuhi naamka nafika sebuleni nakuta vikombe vimetenganishwa. Hapa nyumbani naishi na dada wa kazi, hivyo nikamuuliza kama ndiye akasema hapana. Na kwa vyovyote siyo yeye kwasababu wala hakuwa na taarifa ya hivyo vikombe kuungana coz ilikuwa ameshalala muda napika chai.

Kwa sasa nipo njiapanda wala sielewi hili tukio limetokea vipi? Je, ni nguvu gani iliyotumika kutenganisha hivi vikombe. Muujiza gani huu?

Naombeni msaada wenu kwasababu maswali ni mengi ila muda mchache.
Anza maombi haraka tena uombe na dada wa kazi usilale bila kuomba vunja nguvu za giza
 
Kitaalam joto ndilo lilivitenganisha hivyo vyombo.
Bila shaka kikombe kilichodumbukia ndani ya kingine ni chepesi alafu kilikuwa hakijaacha nafasi ya kupumulia/yaani kilijaza vizuri bila kuacha pancha yoyote.
Pia inaonekana ndani ya kikombe kikubwa kulikuwa na vitone vya maji.
Sasa baadae kutokana na joto, vile vitone vya maji vilitoneshwa na kuwa hewa yenye unyevunyevu ambapo hewa hiyo ilifanya kuwe na presure kati ya kikombe kikubwa na kidogo hali iliyopelekea kikombe cha ndani kurushwa na kutua pembeni ya kikombe kikubwa.

Ondoa hofu usitatanishwe na wanaowaza ushirikina kila mara.
 
Na hili suala la kukuta vimegeuka?
 
Ilikuaje Kikombe kikazama ndani ya kikombe kingine?
Hiki kikombe kidogo ni cha plastiki vile vya kufunika thermos. Huwa nakitumia kuchotea unga wakati wa kusonga ugali. Kikombe kingine kikubwa ni cha udongo.
 
Wakuu kuna kitu cha kushangaza kimetokea sijakielewa.

Jana jioni wakata naandaa chai (Mimi napenda kunywa chai jioni) kuna kikombe kidogo kilizama ndani ya kikombe kingine kikubwa cha udongo. Kwa namna vilivyoshikana ilikuwa ngumu sana kuvitenganisha hata nilipojaribu kwa muda mrefu sana. Hatimaye nilikata tamaa nikajisemea nitajaribu kuvitenganisha asubuhi.

Sasa cha ajabu asubuhi naamka nafika sebuleni nakuta vikombe vimetenganishwa. Hapa nyumbani naishi na dada wa kazi, hivyo nikamuuliza kama ndiye akasema hapana. Na kwa vyovyote siyo yeye kwasababu wala hakuwa na taarifa ya hivyo vikombe kuungana coz ilikuwa ameshalala muda napika chai.

Kwa sasa nipo njiapanda wala sielewi hili tukio limetokea vipi? Je, ni nguvu gani iliyotumika kutenganisha hivi vikombe. Muujiza gani huu?

Naombeni msaada wenu kwasababu maswali ni mengi ila muda mchache.
Vilitenganishwa na kuwekwa pembeni kila kimoja peke yake au ilikuwaje! Ungeweka na picha ya hivyo vikombe ingependeza zaidi mkuu!?

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom