Tukio la kushangaza la kikombe

Tukio la kushangaza la kikombe

Jane Lowassa

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Posts
5,009
Reaction score
9,208
Wakuu kuna kitu cha kushangaza kimetokea sijakielewa.

Jana jioni wakata naandaa chai (Mimi napenda kunywa chai jioni) kuna kikombe kidogo kilizama ndani ya kikombe kingine kikubwa cha udongo. Kwa namna vilivyoshikana ilikuwa ngumu sana kuvitenganisha hata nilipojaribu kwa muda mrefu sana. Hatimaye nilikata tamaa nikajisemea nitajaribu kuvitenganisha asubuhi.

Sasa cha ajabu asubuhi naamka nafika sebuleni nakuta vikombe vimetenganishwa. Hapa nyumbani naishi na dada wa kazi, hivyo nikamuuliza kama ndiye akasema hapana. Na kwa vyovyote siyo yeye kwasababu wala hakuwa na taarifa ya hivyo vikombe kuungana coz ilikuwa ameshalala muda napika chai.

Kwa sasa nipo njiapanda wala sielewi hili tukio limetokea vipi? Je, ni nguvu gani iliyotumika kutenganisha hivi vikombe. Muujiza gani huu?

Naombeni msaada wenu kwasababu maswali ni mengi ila muda mchache.
 
uchawi upo
cc mshana jr
[emoji3][emoji3][emoji3]
IMG-20210113-WA0020.jpg
 
Maamaa duh mzee yaani kazi unayo nakwambia ukisema nchale ukikaa nchale, yaani usiponitafuta uta!

Kwa msaada njoo PM[emoji23][emoji23]

#Mkuu piga dua kisha muachie Mungu
 
He jion? dada wa kazi? ameshalala? unapika mwenyew? upo single? uyo dada anafanya kazi gani?? unganisha izo keypoint utapata jibu vimetokaje
 
he jion? dada wa kazi? ameshalala? unapika mwenyew? upo single? uyo dada anafanya kazi gani?? unganisha izo keypoint utapata jibu vimetokaje
Ione mibavicha jadili mada sio mtu akilo zenu mnazijua wenyewe
 
Sasa ww unawaza nn hapo mtakufa siku si zenu kwa kujipa mawazo ya kijingakijinga huyo housegirl ndo kavitenganisha ivo vikombe sema atak kusema km kuna mauza uza mengine humo nyumban weka hapa mezan ila km ni vikonbe acha kuwaza ujinga
 
Kama uliviacha ndani ya kwenye maji ni sawa ulichokikuta.na hata kama uliviacha nje ya maji ni sawa pia ulichokikuta.Hakuna uchawi

Kuna upepo ulikuwa ndani ya kikombe kikubwa kwa ndani,baadae ulitoka wenyewe ukaviachia.

Ndiyo maana serikali inaongeza walimu wa sayansi nchini
 
Iyo style ya popopawa siku si nyingi atakuingilia kimwili, iliisha mtokea dada yangu kama wewe ivyo ivyo

Nakushauri ununue KY au kilainishi chochote,

Utakuja kunishukuru baadae TRUST ME
Popobawa ni nini kaka?
 
Kama kilichozama ni cha mpira(plastic) kilitoka chenyewe baada ya kutikiswa kidogo tu. Kilitoka kutokana na kusinyaa baada ya joto kupungua.
 
Wakuu kuna kitu cha kushangaza kimetokea sijakielewa.

Jana jioni wakata naandaa chai (Mimi napenda kunywa chai jioni) kuna kikombe kidogo kilizama ndani ya kikombe kingine kikubwa cha udongo. Kwa namna vilivyoshikana ilikuwa ngumu sana kuvitenganisha hata nilipojaribu kwa muda mrefu sana. Hatimaye nilikata tamaa nikajisemea nitajaribu kuvitenganisha asubuhi.

Sasa cha ajabu asubuhi naamka nafika sebuleni nakuta vikombe vimetenganishwa. Hapa nyumbani naishi na dada wa kazi, hivyo nikamuuliza kama ndiye akasema hapana. Na kwa vyovyote siyo yeye kwasababu wala hakuwa na taarifa ya hivyo vikombe kuungana coz ilikuwa ameshalala muda napika chai.

Kwa sasa nipo njiapanda wala sielewi hili tukio limetokea vipi? Je, ni nguvu gani iliyotumika kutenganisha hivi vikombe. Muujiza gani huu?

Naombeni msaada wenu kwasababu maswali ni mengi ila muda mchache.
metaphor?
 
Back
Top Bottom