SI KWELI Tukio katika video linaonesha maji yakisomba magari

SI KWELI Tukio katika video linaonesha maji yakisomba magari

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mdau shiriki kuthibitisha Video inayoonesha maji yakisomba magari ni halisi au imetengenezwa?
1741932892745.png
 
Tunachokijua
Akili mnemba (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Ujio wa teknolojia hii umeathiri kwa kiwango kikubwa mfumo wa utengenezaji na usambazaji wa taarifa kwani inampa mtumiaji uwezo wa kutengeneza maaudhui katika muundo wa picha, video, maandishi ama sauti kwa ubora wa hali ya juu ambapo wakati mwingine yanaweza kutumika kwa lengo la kupotosha.

Na Kama ilivyo kwa maeneo mengine ulimwenguni Tanzania pia inakumbana na kadhia ya maudhui ya upotoshaji yanayotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba hivyo ni muhimu sana kufahamu na kujifunza kila wakati mbinu zitakazokuwezesha kutambua maudhui yaliyotengenezwa kwa teknolojia hiyo ili kuepuka upotoshaji unaoweza kufanyika katika sekta zote za jamii.

Video inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha maji yakisomba magari, inahofiwa kama imetengenezwa au kuwa halisi.

Uhalisia wa video hiyo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Video hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba (AI)

Aidha JamiiCheck imebaini mapungufu kadhaa katika video hiyo yanayokinzana na uhalisia hivyo kuthibitisha kuwa video hiyo imetengezwa. Sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kutokuwepo chanzo halisi cha maji machafu yanayotembea kwa kasi kwani yanaonekana kuibuka sehemu ndogo na kuongeza kasi haraka, kutengana kwa maji kiasi cha kutochangamana kwa maji hayo na ziwa/bahari.

Tukio la Magari yanayosombwa na maji halina uhalisia kwa sababu ya umbali wa maji hayo yalipoanzia hakuna uwezekano wa magari hayo kubebwa katika eneo ambalo halioneshi kuhifadhi magari. Pia maji hayo ni machafu sana lakini magari hayaonekani kuchafuliwa na maji hayo.

Kutokuchukua tahadhari kwa watu wanaoonekana kuwa pembeni ya eneo hilo huku wakionekana wakirekodi video huku mtu mmoja akionekana kupiga hatua kuyaelekea maji hayo hatimaye kusombwa. pia watu wanaoonekana kuwa juu ya daraja, wawili katikati, mmoja anaonekana akirekodi video kwa simu mbili lakini ghafla simu moja inapotea, pia inaonekana mikono miwili ambayo mtu husika haonekani.
​
Ni ya kutengenezwa hiyo... tukio serious hilo watu wako jirani wanashangaa shanghai na kuchukua video
 
Imetengenezwa hyo, watu wakae wanaangali bila kukimbia maji yawasombe tu?
Akili mnemba
 
Back
Top Bottom