MPYA Polisi wamwagiwa maji nchini Afrika kusini

MPYA Polisi wamwagiwa maji nchini Afrika kusini

Taarifa hii ni mpya na bado inafanyiwa tathmini
Source #1
View Source #1
Kumekuwepo na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kuonyesha raia wakimwagia maji magari ya polisi. Hata hivyo, kichwa cha habari kilichoambatanishwa na video hiyo kinapotosha uhalisia wa tukio.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wameeleza kuwa video hiyo ilirekodiwa nchini Afrika Kusini na kwamba magari yanayoonekana kwenye video si ya polisi, bali ni sehemu ya tukio linalohusishwa na kuingia kwa msimu wa joto baada ya kumalizika kwa msimu wa baridi.

Kwa mujibu wa madai hayo, baadhi ya raia humwagiana maji wakiwa barabarani kama sehemu ya utamaduni wa kusherehekea kuanza kwa msimu wa joto. Hivyo, tukio hilo si la raia kumwagia maji polisi kama ilivyoripotiwa awali.

Sambamba na hilo baadhi ya kurasa zimekuwa zikichapisha video ambazo zinaendana na matukio kama hayo ya kuanza kwa msimu mpya wa joto nchini afrikan kusini.
SOUTH AFRIKA.jpg

 
Back
Top Bottom