Tukio gani mwaka 2016 hutolisahau?

Tukio gani mwaka 2016 hutolisahau?

424d34815171d04b4750ddb9510fb984.jpg


Ilo hapo
Hahahaaa
umenishinda tabia wewe itabini nikurudishe ccm
 
  1. sitosahau tunavyommic sana kikwete wakati kipindi yupo madarakani tulimwona raisi fala sana...........
  2. mwendo kasi
  3. matamko yasiyotekelezwa na mawaziri
  4. kigwangara alivyowafungia nje wafanyakazi pale wizarani
  5. lipumba alivyorudi madarakani
  6. mwalimu msigwa
  7. jamaa wa mbeya aliyemwomba rais arudishe tena kupatwa kwa jua
  8. tetemeko la ardhi maana lilitokea nikiwa bukoba
  9. jinsi upinzani ulivyonyongonyea kama vile haupo propaganga zimebaki mitandaoni tu ''tanzagiza''
 
Acha uvivu wewe,kuna umbali gani hapa,mtu nilitembea Mwanjelwa hadi Mbalizi na sijalalamika.

Kwangu ni tukio la kumbukumbu chief, we si utakua na vigimbi kabisa mzee? Dah na ulitembea kwa kupenda au ulikosa hela kama mm?
 
Kwangu ni tukio la kumbukumbu chief, we si utakua na vigimbi kabisa mzee? Dah na ulitembea kwa kupenda au ulikosa hela kama mm?
Nilikosa nauli ya kurudia,kuna mtu nilimfuata Mbalizi nikamkosa.Niliisoma namba.
 
Mzee Wa bapa anapopewa tano kwa kukanusha vipimo halafu wapo wanamshangilia wakati kipimo hicho kinalipisha madereva faini na wanalipa.
 
nilipandishwa daraja(mshahara) mwez mei nikashushwa kupisha uhakk wa watumishi hewa hadi Leo bila bla
 
- Kupata mtoto wangu wa kwanza (Mugisha)
- Pesa za waathirika wa tetemeko Kagera kutojulikana matumizi yake mpaka sasa
 
KWA kweli hili la wahanga linasikitisha sana
 
Mimi binafsi kwa mwaka huu 2016 sitosaau nilivyo-experience maisha magumu chuoni...daaaah nimeyumbishwa Sana haswa maswala ya mkopo...hadi nilikata na tamaa....aseee....nilitamani nikae juu angani niwaambie bodi ya mikopo jinsi ninavyolia ...daaah huu mwaka hapana kwakweli....ila ngoja nisikilize appeal yangu...nikinyimwa tena huu mwaka ujao hautokuwa tofauti na uliopita...
Pole sana ndgu..
Sisi ww tu wanao nufaika na mkopo wote nadhan mwka huu..hawatausahau
 
Back
Top Bottom