Tukio ambalo lilinivuta shati…………….

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,373
Mnamo mwaka 1996 nilifukuzwa chuoni. Lakini kilichonifukuzisha chuoni, ni kufuata mkumbo. Wenzangu waligoma kwa sababu ya posho, kwa upande wangu niliona dhahiri sababu ya kugoma kwao haikuwa na mashiko. Lakini nilishindwa kukataa kugoma, nikajikuta naungana nao. Labda utashangaa nikikwambia kuwa mimi niliyefuata mkumbo sikurudishwa kabisa chuoni, wakati wale waanzilishi wa mgomo wote walirudishwa na kuendelea na masomo.

Inashangaza eh!

pumzika kwa aman na siku ya ufufuo usifufuke kamwe!!!!!!!!!!!!!!maana unatuletea upupu!!!!!!!
 
yawezekana waanzisha mgomo walikua watoto wa wakubwa we ndo umefika chuo umetokea sijui huko NAMANYELE swax bush ukaiga mkumbo
 
yawezekana waanzisha mgomo walikua watoto wa wakubwa we ndo umefika chuo umetokea sijui huko NAMANYELE swax bush ukaiga mkumbo

Ni kweli mkuu, yaani kama ulikuwepo......................sisi watoto wa wa wakulima tuna mengi ya kusimulia.......
 
Acha usanii wewe.... Chuo gani ulifukuzwa, tupe full stori. Chanzo cha mgomo na vigezo vya kurudivilikuwaje????
Au chuo cha kata ulikuwepo?.......
Ninavyojua chuo cha magreat thinker hafukuzwi mtu..... Mgomo hadi kieleweke hakuna cha mtoto wa "a" wala "be"
 
Umenikumbusha msemo wa "bendera hufata upepo" lakini mwisho wa siku upepo hupita zake na bendera hubaki hapo hapo! Pole sana Mtambuzi ingawa ni kitambo kidogo!
 
Acha usanii wewe.... Chuo gani ulifukuzwa, tupe full stori. Chanzo cha mgomo na vigezo vya kurudivilikuwaje????
Au chuo cha kata ulikuwepo?.......
Ninavyojua chuo cha magreat thinker hafukuzwi mtu..... Mgomo hadi kieleweke hakuna cha mtoto wa "a" wala "be"

Halafu itakusaidia nini........................?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom