Tukikumbuka ya Magufuli, hatutayasahau ya Bernard Membe

Nimei LOVE sababu ya kunickesha. Ey

Nitakujibu ifuatavyo.
1.Katiba ya mwananchi ni haki yake ya kimsingi maana sheria nyingi ZILIZOPO zina elements za UKOLONI-Magufuli HAJAKATAA ila timing haikuwa nzuri. Na serikali naamini haikuwa na hela za KUPOTEZA kwa mambo ambayo hayakuwa ni ya KIPAU MBELE
Ilibidi kufanya Maendeleo ya nchi ya nchi kwanza halafu Katiba ITAFUATA.-
Huo NI MTAZAMO WANGU BINAFSI.

2.Katika kufuta Ujinga na umasikni Tanzania chini ya Magufuli imepunguza kiwango cha UMASKINI kwa asilimia kubwa sana kwa asilimoa 8%
Kutoka 34.4% 2007 mpaka {26.4%-2018 kumbuka ni miaka MITATU tu Baada ya Magufuli kushika Utawala.wakuingoza nchi.{ 2019 World Bank Report}

3.Hilo la darasa la saba si kweli. Vijana wengi sasa wanahimizwa wasome na wanasoma kweli. Zingine ni siasa za uongo.

4.Wakulima kwa miaka mingi tulipotoka tu Ujamaa na kuubakiza kwenye nadharia tu, ilichukuwa muda mrefu MKULINA mwenyewe KUJIELEWA. Sasa anaweza kuuza mazao yake atakavyo-SOKO HURU.

5 Ni NGUVU GANI ya vyama vya Ushirika ambayo ungetaka wapewe? Maana vyama vya Ushirika ndo vunahimizwa ili kuwasaidia wakulima WASIDHULUMIWE na MADALI- Hilo si kweli.

6. Binadamu wote ni sawa na Africa ni moja. Mtu mmoja akikosea ni yeye peke yake na si kujumlisha.

7.WALIOCHAGUA UPINZANI ni Watanzania na wana haki yao ya Kikatiba kufanya siasa zao WAKATI UNAPOFIKA kama sasa hivi. siku hizi si WANAKUSANYIKA na tena wanapata coverage ya vyombo vya habari kama TV.? -Hilo pia si kweli.

8. Wanapozuiwa LABDA wahusika wanataka kuvuruga amani ama MATAMSHI ya UCHOCHEZI.La sivyo Sioni sababu ya wao kutouza sera zao kwa USTAARABU.
Naamini nimekujibu nilivyoweza. Kumbuka haya ni MAONI YANGU BINAFSI na ni mtazamo wangu mimi mwenyewe.
7. na 8. Umepiga siasa vilivyo moyoni unajua kina Msukuma and co walifanyacho... bado hapo hatujagusa vyombo dola
 
Hili la asilimia kubwa zaidi ya 2015 hukunijibu!!
View attachment 1502131

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inayashikilia magari 10 ya wagonjwa ambayo yalikuwa yagawanywe kwa kata 10 za Jimbo la Same Magharibi na Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Mathayo David kama utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa mwaka 2015.

Magari hayo yalikuwa yagawanywe kwa kata hizo jana tarehe 08.07.2020 kupitia ofisi za CCM Wilaya ya Same lakini TAKUKURU ikaingilia kati na ikamuita Dkt. Mathayo na kumhoji kuhusu tukio hilo, kuelekea mchakato wa kupata wagombea ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu
Ni kweli... na huu ndio mfano achilia mbali wanaopewa pesa "wakahonge!!"
 
Hata wananchi pamoja na uhuru wao lakini nao hukosea,
kuna jamaa huko philipino alikuwa mwana mziki aliendesha maandamano kumtoa raisi aliyekuwapo na kuafanikiwa kuchukua hiyo nafasi ya uraisi, na aliungwa mkono na wananchi.
Lakini baada ya miaka miwili nae wakamtoa kwa maadamano, kwa hiyo hawakuchagua kwa usahihi pamoja na uhuru waliokuwa nao,

Pili kuna raisi wa misri aliemtoa mubarak madarakani lakini alipoingia ndo akawa mwiba na kuongeza ma sheria makari
Pia haohao wananchi wakamtoa pia na akahukumiwa kunyongwa.
Sasa jiulize ni hasara ngapi walipata kutokana na maandamano ya mara kwa mara hao wananchi kwa kukosa umakini kwa kigezo cha uhuru wao?

Wananvhi waelimishwe ili wanapohitaji mabadiliko yawe yenye tija na sio kukurupuka na mihemko ya kisiasa na kingizia taifa hasara zisizo na tija.
Kunakuwaga na wakati watu wengine huwa hawajui nini hasa wanachokitaka. Wengine hufuata mkumbo tu.
 
Nikitoa jawabu katika swali ambalo unayo majibu yake sitokutendea haki na mwisho wa siku utaona aidha ninakutusi au nakukosea adabu.
Wewe ni muungwana, Hata ukinijibu kimihemko ama kimuegemeo bila tusi stajali.
Maana tangu tuuanze mjadala huu hatujatupiana maneno mabaya.

Mwanamageuko una UHURU wa kuniambia chochote na UKWELI wowowte uujuao na mahali ambapo unaniona nakupinga chenga.Sitahesabu hilo kama tusi bali MAONI na mtazamo wako.
Shukrani
 
Kwa hiyo aliyesema alitolewa "jalalani" na ile kauli ya "wapumbavu" ni kauli za kiungwana?
Inategemea nasentensi ilivyotumika katika wakati husika .
Huwezi kumwambia mtu kwa mfano "Wee mtu wa jalalani utatuambia nini?"
Utakuwa umemdhalilisha.
 
Inategemea nasentensi ilivyotumika katika wakati husika .
Huwezi kumwambia mtu kwa mfano "Wee mtu wa jalalani utatuambia nini?"
Utakuwa umemdhalilisha.
Ahaa wanena vema kwa hiyo waliodai kuokotwa jalalani wakiambiwa hivyo itakuwa wametusiwa?
Ila je lile la malofa wapumbavu linatumika wakati sahihi au sio?
 
Nadhani siasa, demokrasia na hizi taratibu nyingine kama uchaguzi n.k tumezikopi na kupaste kama tufanyavyo kwenye ushabiki wa soka bila kujua sisi ni nani, tunaenda wapi na tunahitaji nini kufika huko!!
 
Ahaa wanena vema kwa hiyo waliodai kuokotwa jalalani wakiambiwa hivyo itakuwa wametusiwa?
Ila je lile la malofa wapumbavu linatumika wakati sahihi au sio?
Nafikiri lugha yeyote isiyo na staha si lugha nzuri. bila kujali ni nani ametumia.
Wakati mwingine mwanadamu hujisahau na kuteleza katika usemi wake hasa kama si mwangalifu katika kujua neno hili litaudhi ama la.

Kwa kifupi mwadamu huyu ambaye ni wewe na mimi tunajikuta tumekosea pasipo kutaka.
Baada ya mtu kutambua kuwa neno lililotamkwa limeleta MADHARA ,ndo hapo regrets zinakuja "SIJUI NI KWA NINI NILITAMKA HIVYO?" Matamshi yakishatoka kuyarudisha huwa ni kibarua.
Ndo waingereza wanasema mtu anaanza kufanya kile wanachokiita
"DAMAGE CONTROL"
 
Back
Top Bottom