Mpaka taasisi zinagoma, sisi raia ndio wavumilivu sana na waelewa sana kila tunapopewa huduma mbovu na kunyimwa haki zetu?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu,

Ni kwamba "Wanyonge" ndio jina tulilokubali kuitwa na kuliishi hatuwezi kabisa kutoka humo hata tufanyiwe aina yoyote ya upuuzi hatutafanya kitu? Tunamuachia Mungu?

Tunalipia huduma hizi ni haki yetu kupata kilicho bora. Tunanyonywa na kodi za kila aina kwanini hatu-DEMAND kupata kilicho bora.

Tuko macho tu, tunaangalia mtu anaiba mamilioni kila mwaka na wala hatumfanyi lolote, na wengine tunadiriki kuwa chawa kumsafisha kwa wengine, hatuoni haya?

Ukiibiwa na kibaka huko mtaani mshipa unakusimama kama mlingoti kutoa povu, na ukikuta mwizi kashikwa sehemu unakuwa mstari wa mbele kumuadhibu!

Sasa kwanini tunawaangalia hawa wanaotupokonya haki kila siku, hawa ndio wanafanya barabara mtaani kwako ziwe mbovu, hupati maji, umeme wa kusuasua, huduma mbovu hospitali nk.

Kwa hili lililotokea kuhusu Bima ya NHIF kwanini tuko kimya? Kwa ubadhirifu unaofanyika serikalini, hatukutakiwa hata kulipa bima, huduma zingekuwa zinatolewa bure, lakini tunafanya nini? Kwanini tuko kimya?

Nawaacha na sentesi hii kutoka andiko moja la mwana JF;

"Ikiwa umempa fundi kazi akushonee nguo au akutengenezee kabati halafu fundi yule akala hela na kazi ikarudi mbovu, utampa tena akufanyie kazi nyingine? Sasa kwanini hupati uchungu kwa hawa wanaoharibu Tanzania hii moja tuliyonayo? Tunasubiri pakuche ndio tutafute shuka?"
 
1. Wameuza bandari kwa DP World tupo kimya .
2. Wameuza Ngorongoro kwa mwarabu tupo kimya.
3. Wameuza gesi ya Mtwara kwa mchina tuko kimya
4. Wameuza pori la Loliondo kwa mwarabu tupo kimya.

Sisi wananchi ni wa ajabu na tumejaa ubinafsi sana.
 
Watanzania ujamaa umewaharibu, wanadanganywa kuwa ipo siku ama watakuwa wateuliwa ktk hamashauri za wilaya, serikalini, TRA, n.k na wataula uteuzi kwa kuiba au marafiki, ndugu na jamaa watateuliwa nao watafaidi mapochopocho ya ufisadi, rushwa na wizi wa mali ya umma ambayo watanzania wanaamini mali ya umma ni dude la kuibiwa na yeyote atakayeikaribia nafasi au ajiri za umma.

Kifupi ujamaa unaleta dhana potofu kuwa tunachukua chetu mapema hivyo hakuna athari, wanavuta subira nao waibe mali yao ya umma kwa kijamaa.
 
Back
Top Bottom