Tujiulize: Kwanini kila mwaka Watanzania hawana furaha?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Je, ni Siasa mbaya, Maendeleo madogo, kukosa haki muhimu, ubinafsi, tofauti ya vipato. Pamoja na kujengewa barabara wanasiasa wanakimbia ukweli kwamba Watanzania hawanaraha na maisha yao. Hata Rwanda pamoja na Kagame kusema wanamaendeleo tatizo ni nini? Botswana nayo iko chini sana

Mimi kwa mawazo yangu ni mambo mawili tu makubwa kwa Tanzania (1) Tuna utamaduni wa kuangaliana sana. Tunajiita wazalendo lakini hatuna mapenzi ya maendeleo tuna sisi ni wale wa kuogopa mwenzio kuendelea. Wakati wa katiba za Kenya na Tanzania nakumbuka Wakenya wakasema Mkenya ni Mkenya hata awe wapi. Tanzania diaspora walipigwa vita kama vile ni majambazi wakati ni Watanzania wanaotafuta maisha yao. Sababu kubwa Watanzania hawapendi wengine wapate hata kama kupata kwako hakumzuii mwingine.

Hii inaonyesha watu hawana raha kwa mfano huu. Nakumbuka vilevile MD wa TPDC alivyopata kazi alipigwa majungu miaka mitatu kwasababu alitoka nje tu mpaka akarudishwa na Magu. (2) Sababu ya pili nchi yetu imekuwa nchi kama ya kijeshi. Watu hawako huru wanaosema tuko huru ni walewale wanaonufaika. Unyanyasaji umeongezeka sana kuanzia kubambikwa kesi, kupigwa, uhuru kwa vyama wananchi wanakatishwa tamaa sana na vitendo vya unyayasaji

Pamoja na bongo flava yetu ni aibu sana kuwa chini hivio

1. Afghanistan

2. South Sudan

3. Zimbabwe

4. Rwanda

5. Central African Republic

6. Tanzania
 
Furaha ili iwepo lazima ajira ziwepo. Lazima watu wawe na kipato cha ku meet basic needs..

Watanzania wengi hawa meet basic needs even skilled citizens
 
Hivi Kwa mantiki hii furaha ni nini?!

Juzi juzi nilikua nasoma jarida Fulani hivi linaloonyesha kua maisha ya jijini Tokyo ni ya stress Sana na watu hawana furaha kawani hawana muda wa kupumzika kwani hufanya kazi masaa mengi.
 
Umefanywa uwe masikini kimakusudi yaani kusomeshwa namba ili iwe rahisi kutawaliwa hio Furaha itoke wapi,haya ni mapito na ni kawaida Mkristo akishika usukani,
 
Mkuu Kamundu, usiziamini kila tafiti, hicho kiwango cha wasio na raha ni kwa mujibu wa vigezo vya wazungu, lakini sisi Watanzania wenyewe pamoja na shida zetu zote, sisi ni watu wenye furaha sana na tuna raha sana, uthibitisho ni kila miaka 5, kwa raha zetu tunawachagua watu wale wale, chama kile kile kinachotupa raha na kutufanya ni watu wa furaha.

Nenda vijijini pita pita uone jinsi Watanzania waliopigika kwa umasikini uliotopea wanavyo smiles kwa raha zao, kwa vile mimi ni mtu wa video production, nina video clips mamia zikionyesha jinsi Watanzania wanavyo smiles kwa raha zao!. Hata uwe na shida vipi, ukiizoea ni raha tuu. Vijini visivyo na umeme, giza likiisha ingia tuu, ni raha tuu!. Vijijini maji kisimani ni mbali, trip ya kwenda kuteka maji kwa dada zetu ni raha tuu hadi wachumba wanapatikania kisimani kama Rebecca mke wa Yakobo alivyopatikana, ni raha tuu. Usukumani Chagulaga ni raha tuu, Uzaramoni mdundiko ni raha tuu, kila mahali Tanzania ni raha tuu.

Tulipoamua kufuata mfumo wa vyama vingi, asilimia 80% walitaka chama kimoja, hawa asilimia 80% ndio wanaichagua CCM kwa raha zao na kuipa ushindi wa kishindo kila uchao.

Watanzania tuna raha sana na tuna furaha daima licha ya matatizo lukuki yanayotukabili, ikiwemo umasikini, ujinga, maradhi, rushwa, ufisadi, ubadhirifu, uhujumu uchumi, etc kwasababu yote haya tumeisha yazoea, tunaishi nayo na ndio maisha yetu na raha zetu.
P
 
Screenshot_20200303-141241-picsay.jpeg
 
Pascal Mayalla,
Huo utafiti wa 80%
Mosi, ilikuwa ni baina ya ccm kwa CCM,
Pili, wakati ule si sawa na wakati huu
Tatu, Kutumia data za kale kuhalalisha
Nne, Unatumia generic reasoning point of view zaid
Tano, wewe binafsi kwa kuamua tu kutoka moyoni mwako na kusema Watanzania tuna furaha, ni kumkosea MUUMBA MBINGU NA DUNIA kwa kuwa unaongelea nafsi usizojua kuwa zinawaza nini
Sita, hujafafanua nini maana ya furaha
 
Tujiulize: Kwanini kila mwaka Watanzania hawana furaha!?
Sio kwamba kila mwaka ukosaji wa furaha unaongezeka?
 
Pascal Mayalla,
Pascal Mayalla leo umeongea ukweli kwa namna ya kupinda pinda kidogo.Ila ukweli wenyewe ni kuwa SISIEMU imeidumaza nchi hii katika nyanja zote kiuchumi,kisiasa,kijamii na kimataifa.

Tunalazimishwa kuwachagua viongozi ambao kama natural Justice ingekuwepo nchini walitakiwa sasa hivi wawe wafungwa kwa matendo yao.

We are stuck Brother. We need to Reconstruct Our Tanzania,though it won't be that easy task.
Katiba Mpya haikwepeki ili kila MTU asimamie maendeleo yake na ya nchi.
 
Mkuu Kamundu, usiziamini kila tafiti, hicho kiwango cha wasio na raha ni kwa mujibu wa vigezo vya wazungu, lakini sisi Watanzania wenyewe pamoja na shida zetu zote, sisi ni watu wenye furaha sana na tuna raha sana, uthibitisho ni kila miaka 5, kwa raha zetu tunawachagua watu wale wale, chama kile kile kinachotupa raha na kutufanya ni watu wa furaha.

Nenda vijijini pita pita uone jinsi Watanzania waliopigika kwa umasikini uliotopea wanavyo smiles kwa raha zao, kwa vile mimi ni mtu wa video production, nina video clips mamia zikionyesha jinsi Watanzania wanavyo smiles kwa raha zao!. Hata uwe na shida vipi, ukiizoea ni raha tuu. Vijini visivyo na umeme, giza likiisha ingia tuu, ni raha tuu!. Vijijini maji kisimani ni mbali, trip ya kwenda kuteka maji kwa dada zetu ni raha tuu hadi wachumba wanapatikania kisimani kama Rebecca mke wa Yakobo alivyopatikana, ni raha tuu. Usukumani Chagulaga ni raha tuu, Uzaramoni mdundiko ni raha tuu, kila mahali Tanzania ni raha tuu.

Tulipoamua kufuata mfumo wa vyama vingi, asilimia 80% walitaka chama kimoja, hawa asilimia 80% ndio wanaichagua CCM kwa raha zao na kuipa ushindi wa kishindo kila uchao.

Watanzania tuna raha sana na tuna furaha daima licha ya matatizo lukuki yanayotukabili, ikiwemo umasikini, ujinga, maradhi, rushwa, ufisadi, ubadhirifu, uhujumu uchumi, etc kwasababu yote haya tumeisha yazoea, tunaishi nayo na ndio maisha yetu na raha zetu.
P

Kama ni wazungu mbona kuna nchi nyingine nyingi sana za Africa ziko juu. Mfano Kenya hatuna tofauti za kiutamaduni wako juu yetu. Kuna kundi la Watanzania linafikiri Watanzania wana furaha hawa ni wale wa matabaka ya juu. Vilevile naona umeingiza siasa kama Watanzania wangekuwa na furaha kila mwaka kwanini wachague chama ambacho kimetufanya tuwe masikini kila mwaka. Hakuna nchi ya Demokrasia ya kweli kwenye Dunia hii ambayo Chama kimoja tu ndiyo kinatawala haijawahi kutokea Duniani. Ukiona hivyo ujue ni demokrasia ambayo haijakomaa
 
Pascal Mayalla,
Huo utafiti wa 80%
Mosi, ilikuwa ni baina ya ccm kwa CCM,
Pili, wakati ule si sawa na wakati huu
Tatu, Kutumia data za kale kuhalalisha
Nne, Unatumia generic reasoning point of view zaid
Tano, wewe binafsi kwa kuamua tu kutoka moyoni mwako na kusema Watanzania tuna furaha, ni kumkosea MUUMBA MBINGU NA DUNIA kwa kuwa unaongelea nafsi usizojua kuwa zinawaza nini
Sita, hujafafanua nini maana ya furaha

Lakini jiulize na kuonewa kote Dunia nzima 6 kutoka mwisho hata kama kuna mapungufu!!!!
 
Police na traffic police! Zaidi chini ya utawala huu, ongezea na viongozi wapenda sifa kila pahala ni vurugu tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom