habari ya hapa
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 12,789
- 8,753
Upendo haupo katika maneno, upendo huonekana kwa matendo, huonekana kwenye raha na huthibitika wakati wa shida, daima upendo una sura 2 japo wengi wetu twaijua moja, wakati wa raha, faraja, nyimbo na zawadi kedekede, tunajisahau na kuridhika kwa upendo huo, kimsingi kila upendo una kipimo chake wakati wa shida, raha na wakati wa magonjwa, wakati ambao unaonajionea tabia na kasoro mbalimbali hapo ndipo upendo hupimwa.
Yule anayeweza kusimama na ww kwa matatizo, wakati wengine kwa kawaida wangeweza kukukimbia, yule ambaye asingependa kuona unaharibikiwa, yule anayeweza kukutunzia siri zako za ndani wakati wengine wangekutangaza, yule ambaye hatakama mkikosana hapendi kukuona ukiseteseka, wakati wengine wangefurahia na kukuona ukiharibikiwa kabisa, tulio wengi hapa duniani tanahangaika kupenda vinavyopendeza tunasahau kuwa kupenda vinavyopendeza hakuna thamani isipokuwa kupenda visivyopendeka,
Hebu tujipime leo wana JF, tuna upendo wa kweli?? ulifanyaje wakati nduguyo/mpenzi alipokukosea? ulimsengenya au ulimuombea, ulimpenda bure au ulimpaka matope??