Njooni tujipime kama kweli tunao upendo

Njooni tujipime kama kweli tunao upendo

Phlagiey

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
3,500
Reaction score
1,688
Daima upendo una sura mbili, japo wengi wanaijua moja wakati wa raha,faraja,kujirusha na zawadi kedekede wanaridhika na upendo huo, ila upendo unakipimo chake wakati wa shida waraha na wakati wa magonjwa wakati ambapo watu huona tabia kasoro na mapungufu yako hapo ndipo upendo hupimwa, yule anaeweza kusimama na wewe wakati wengine kawaida wangekukimbia tena awezae kukufichia aibu wakati wengine wangekutangaza yule ambae hapendi kuona unaharibikiwa hata mkikosana hapendi kuona unateseka.

Watu duniani wanahangaika kupenda vinavyopendeza, wanasahau kupenda vinavyopendeza hakuna thamani isipokuwa kupenda hisivyopendeka.

Jipime kama kweli wewe unao upendo, ulifanyaje ndugu yako, mpenzi wako, jirani yako alipokukosea ulimsengenya, ulimpenda, ulimpaka matope au ulimsamehe bure?

Upendo umekuwa kama kitendawili ndani ya familia na jamii yetu kiujumla, watu wanawapenda ndugu, wapenzi na jamaa zao kwasababu wana mali, umaarufu,elimu, pesa, magari na majumba ya kifahari je kwako ndiyo tafsiri ya upendo hiyo? kama unampenda kwaajili ya mali unafanya ziada gani.

Ni yupi alie mwenye upendo ikiwa tunapendwa kutokana kitu tulichonacho? upendo kwako ni nini?

Uliwahi kufanya/kufanyiwa nini ambacho hautakisahau kama ishara ya upendo kwako?

Jipime kama kweli una upendo usiishie kusema unaupendo wakati upendo wako ni wamaneno siyo vitendo
.:A S check_03:
 
upendo kwa sasa kuupata si rahisi.... bnadamu tumekuwa wanafiki hadi kwa nafs zetu wenyewe... tamaa zimetujaa hakuna upendo kati yetu... upendo kwa pesa tu saiv
 
wachache sana ambao tuna upendo wa aina hii
 
Uliwahi kufanya/kufanyiwa nini ambacho hautakisahau kama ishara ya upendo kwako?

Natarajia kufanyiwa mungu akijali disemba kama kitakua kama kilivyopangwa ntakisema siwex sema now mapema mno
 
Umeelewa nini tata?

Tata upendo wa kweli umekua adimu, watu tuna fake upendo hatuko real, l believe upendo wa kweli anao mamangu tu kwa kunikeep 9 month kwenye tumbo lake na kunilea mpaka hivi sasa naitwa baba nani, even myself najua nina vimelea vya upendo toka kwa my mon coz naipenda familia yangu especially wanangu, but 99% ya watu wanashow love ambayo inawalakini, l believe that.
 
Kwanza kabla ya yote,upendo ni nini?

Maana watu hapa wanaweza kujibu tu bila hata kujua upendo ni nini!
 
Kwanza kabla ya yote,upendo ni nini?

Maana watu hapa wanaweza kujibu tu bila hata kujua upendo ni nini!

Kwa uelewa wangu, upendo ni jambo ambalo ni inner feeling ambayo anakuwa nayo mtu kwa ajili ya mtu fulani, mfano upendo wa mama kwa mtoto, you see ni ile khali ya mtu kuwa tayari kujitoa kimwili, kihisia au kifikra kwa ajili ya mtu mwingine.
 
Tata upendo wa kweli umekua adimu, watu tuna fake upendo hatuko real, l believe upendo wa kweli anao mamangu tu kwa kunikeep 9 month kwenye tumbo lake na kunilea mpaka hivi sasa naitwa baba nani, even myself najua nina vimelea vya upendo toka kwa my mon coz naipenda familia yangu especially wanangu, but 99% ya watu wanashow love ambayo inawalakini, l believe that.
Lakini tata unawezaje kuamini kwamba mama yako ndiye mwenye upendo wa kweli kwa kigezo cha kubebwa tumboni miezi 9?, kubebwa tumboni miezi tisa siyo kipimo cha upendo wa mama, maana katika hali yoyote ile mwanamke ukishabeba mimba lazima mtoto akae tumboni hawezi kukaa mgongoni ama mahala pengine tofauti na tumboni. ukitumia hiki kigezo kama upendo unakosea.

Ukiachilia mbali swala la kubebwa miezi 9 hata ukigeukia hili la kukuzaa kukulea mpaka umekuwa mtu mzima hiyo ni haki yako ya msingi ambayo angefanya kinyume na hapo hata jamii yako ingestaajabu, upendo ni vyema tusiupime kwenye mambo yale yaliyo ya lazima kutokana na mazingira yanavyokulazimu kufanya, hapo hainatofauti na kusema wewe kuinunulia chakula familia yako ni upendo wakati hili ni swala la lazima maana bila wanao kula watakufa na wewe mwenyewe kama baba utakufa pia.
 
Binafsi niwehi kumuinua jamaa yangu kiuchumi akiwa hata kitu kabisa, alipata pesa sana mpaka akanizidi najivunia sana hili kila siku iyendayo kwa Mungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom