deo paul555
JF-Expert Member
- Oct 22, 2018
- 1,405
- 520
Aisee...
Huyo mzee huwa napenda sana sauti yake. Sijaona mwandishi mwenye sauti kama Masoud Masoud.Kuna mzee anaitwa Masoud Masoud yuko TBC nafikiri mpaka sasa, namuelewa sana kwenye simulizi za historia ya mziki wa zamani na ndiye aliyetangaza msiba wa Michael Jackson
TUMBO TAMIMU RISASI.TUMBO RISASI.
Hili ni tatizo kwa taasisi nyingi la kuwapa wafanyakazi majukumu wasiyoweza. Taasisi kama TBC inatakiwa kuwa na wafanyakazi wenye uelewa mpana wa historia ya sekta na mwajiri wao, wapi ilitokea, wapi iliko na wapi iendako.Nilienda kipindi fulani kwenye maonyesho ya sabasaba, nikaingia banda la TBC/ Radio Tanzania.... Nikauliza kama naweza kupata michezo ya radio ya akina Havijawa , au vituko vya Pwagu na Pwaguzi na jingle kama za kipindi cha majira, michezo ile saa mbili kasoro..
Niliishia kupata fedheha , nikakuta vijana kwenye banda hawajui hata naongelea kitu gani.. Sikurudi tena ....
Kuna historia na kumbukumbu nzuri.. Ilikuwepo Radio Tanzania
yeah unaweka watu mchanganyiko kufuatana na mahitaji ya soko.Hili ni tatizo kwa taasisi nyingi la kuwapa wafanyakazi majukumu wasiyoweza. Taasisi kama TBC inatakiwa kuwa na wafanyakazi wenye uelewa mpana wa historia ya sekta na mwajiri wao, wapi ilitokea, wapi iliko na wapi iendako.
Freddy yupo radio citizenLenny Mambombotela ni Mkenya I think,alikuwa KBC,nakumbuka alikuwa na kipindi cha UHALIFU HAULIPI CHOCHOTE(kama sikosei),pia KBC nao walikuwa wazuri sana enzi hizo,bila kumsahau mtaalamu Freddy Obacho Machoka
Lenard Mambo Mbotela,wema haulipwi chochote.Freddy yupo radio citizen
Umemsahau Ben KikoTake a break, na tujikumbushe enzi zile za RTD, ambapo kulikuwa hakuna FMs rado kama sasa. Hakika kulikuwa na watangazaji, vipindi bomba na hata nyimbo za kutambulisha vipindi zilikuwa makini sana. Hebu ngoja niwakumbushe baadhi ya watangazaji wa wakati huo.
1. Nassoro Nsekeli- alikuwa na sauti kama ya mafua hivi alikuwa mtaalamu wa kipindi cha Majira- ndiye aliyetangaza kifo cha Nico Zengekala
2. Bujago Izengo wa Kadago- Kibesi chake kilikuwa safi sana
3. David Wakati (DG) - kipindi cha Nipe habari- Kwaherini wote, mungu awalinde na mmbaki salama, mungu akipenda..............
4, Khalid Ponera- Zilipendwa
5. Ahmed Kipozi- taarifa ya habari
6. Hassan Mkumba- matangazo ya vifo
7. Siwatu Luwanda
8. Salama Mfamao
9. Mohamed Amani (Mohamed Dahman)
10. Salim Seif Nkamba
12. CHisunga Steven- kipindi cha Ugua pole duu
13. Bathoromeo KOmbwa (bati Kombwa) - WAkati wa Kazi
14. Ahmed Jongo- Mpira
15. Christina Chokunogela
16. Dominic Chilambo- Mpira
17. Edda Sanga
18. Debora Mwenda- Mama na Mwana
19. Aloycea Maneno- Ombi lako, cheichei Shangazi, mama na mwana
Duu nawamiss sana hawa watu tofauti na watangazaji wa sasa