Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

"Ben Kiko" style yake ya kuripoti matukio ilinifanya nipende kipindi cha majira saa 12:30 asb na jion saa 3:00

I real miss the past!
 
Redio Tanzania RTD mama wa tbc ndio redio kongwe nchini. Imechangia sana maendeleo ya nchi yetu tangu Uhuru.
Huwezi kuzungumzia historia ya Tanzania bila kutaja mchango wa RTD.
Radio hii imesaidia sana kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili. Imesaidia kuwaelimisha Watanzania katika mambo ya siasa, uchumi, historia, afya na michezo.

RTD imesaidia kuliunganisha taifa hili linaloundwa na watu toka makabila mengi. Redio hii imekuwa mwalimu kwa wananchi wote toka siku nyingi. Elimu hii ilipitishwa kupitia watangazaji wake mahiri ambao hakika tutawaenzi daima.

Tunawamiss sana Julius Nyaisanga RIP, Halima Mchuka, Bati Kombwa, Sara Dumba, Paul Sozigwa, Abdallah Mlawa, Khalid Ponera, Thecla Gumbo, Mshindo Mkeyenge na wengine.
Tunauenzi pia mchango wa Halima Kihemba, Betty Mkwassa, Abdallah Majura, Charles Hillary, TIDO MUHANDO, Pascal Mayalla, Eda Sanga, Nswima Ernest, Jacob Tesha, Mikidadi Mahmoud, DAVID WAKATI, BEN KIKO na nk.
Pia wapo Yusuf Omar Chunda, Ahmed na Sango Kipozi, Abisai Stephen, Ahmed Jongo, Salim Mbonde, Suleiman Hega, Hamza Kasongo, Idrissa Sadalla na Suzanne Mongi.
Tunawamiss pia Vick Ntetema, Deborah Mwenda , Alecia Maneno, Sekion Kitojo, Ana Kidela, Suleiman Kumchaya, Mohamed Kisengo, Sued Mwinyi, Juma Nkamia na wengine wengi kama Shaban Kissu ambaye pia ni mtangazaji makini.
Sifa kwao pia ambao labda nimewasahau.
Watangazaji hawa nawaita kama ni "unsung heroes". Wametoa mchango mkubwa sana kwa nchi hii ingawa walikuwa wakilipwa mishahara midogo sana.
Wamekuwa wazalendo kwa nchi yetu kwa kiwango cha juu kabisa. Nchi iwaenzi watangazaji hawa ambao ndio walikuwa chachu ya kukuza umoja, uzalendo na mshikamano Tanzania.
 
Umemsahau kaka yetu Paschal Mayalla
 
Yupo ndugu. Angalia vizuri
Oooops!
My bad!
Mayalla ni mtangazaji na mwandishi mzuri sana.
Namkubali sana kwa kazi zake toka akiwa enzi zile DTV na akina Betty Mkwasa.
Nashindwa kuelewa watu kama akina Ayoub Rioba, Tido Mhando, Ruge au ITV ni kwa nini wanashindwa kumtumia jamaa
 
TANZIA: Mtangazaji wa zamani maarufu na gwiji la kutangaza kandanda Ahmed Jongo amefariki dunia leo, Jumapili.

> Nguli huyo wa utangazaji wa Redio Tanzania kwa sasa TBC, alistaafu mwaka 2005 .

======

Ahmed Jongo aliwahi kuomba msaada wa matibabu kupitia vyombo vya habari

> Alikuwa akisumbuliwa na miguu na macho

P
 
Mola akurehemu ahmed jongo mtangazaji mahiri sana wa kandanda.msalimie sana mwana habari mwenzako mahiri wa sport mshindo mkeyenge huko akhera
 
Take a break, na tujikumbushe enzi zile za RTD, ambapo kulikuwa hakuna FMs rado kama sasa. Hakika kulikuwa na watangazaji, vipindi bomba na hata nyimbo za kutambulisha vipindi zilikuwa makini sana. Hebu ngoja niwakumbushe baadhi ya watangazaji wa wakati huo.

1. Nassoro Nsekeli- alikuwa na sauti kama ya mafua hivi alikuwa mtaalamu wa kipindi cha Majira- ndiye aliyetangaza kifo cha Nico Zengekala

2. Bujago Izengo wa Kadago- Kibesi chake kilikuwa safi sana

3. David Wakati (DG) - kipindi cha Nipe habari- Kwaherini wote, mungu awalinde na mmbaki salama, mungu akipenda..............

4, Khalid Ponera- Zilipendwa

5. Ahmed Kipozi- taarifa ya habari

6. Hassan Mkumba- matangazo ya vifo

7. Siwatu Luwanda

8. Salama Mfamao
9. Mohamed Amani (Mohamed Dahman)

10. Salim Seif Nkamba

12. CHisunga Steven- kipindi cha Ugua pole duu

13. Bathoromeo KOmbwa (bati Kombwa) - WAkati wa Kazi

14. Ahmed Jongo- Mpira

15. Christina Chokunogela

16. Dominic Chilambo- Mpira

17. Edda Sanga
18. Debora Mwenda- Mama na Mwana
19. Aloycea Maneno- Ombi lako, cheichei Shangazi, mama na mwana

Duu nawamiss sana hawa watu tofauti na watangazaji wa sasa
Chisunga Steven amefariki leo
 
Back
Top Bottom