jchofachogenda
JF-Expert Member
- Jan 8, 2012
- 537
- 123
Najuta kwanini nilichelewa kuingia Jamii forum, kuna raha ya ajabu. Mnanikumbusha mbali sana, mimi nataja tuisheni za shule ya msingi kwa kuwa mliotangulia mmetaja tuishweni zote za sekondari. Mitaa ya Sinza kuna ticha alikuwa anaitwa MT (Mtaalam) huyu alipata sifa sana ya kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba. Mitaa ya Mburahati kuna ticha alikuwa anaitwa Dan, nae huyu alikuwa noma.Alikuwa na uwezo wa kumpandisha mwanafunzi kutoka maksi 20/50 akakuwezesha hadi ukapata fisi (50/50). Mitaa ya Mabibo kulikuwa na ticha aitwae Ibunga Boni, ngoja niwape mikasa ya huyu mtu. Huyu ticha alishawahi kugombana na ticha mwenzake(MT) baada ya kutunga swali la kumkashifu kwenye mtihani. Mkasa mwingine wa huyu ticha ni kwamba alishawahi kumpa ujauzito mwanafunzi wake na skendo hii iliwahi kutoka kwenye gazeti la Alasiri. Wazazi wa yule binti wakamsusia bwana Ibunga na akajichukulia mzigo kiulaini. Pamoja na mikasa yote hii huyu ticha alikuwa na sifa moja kubwa. Alikuwa mtaalamu wa kutunga mitihani ya kila wiki yenye ubora wa hali ya juu. Kingine ninachokumbuka alikuwa anawandikia wanafunzi wanaofaulu mitihani kwake shule za sekondari watakazokwenda. Mfano anakuandikia utakwenda Azania,mbinu hii ilimsaidia kupata wanafunzi wengi wanaofanya mitihani kwake. Kwa wanafunzi waliosoma shule za msingi za Manispaa ya kinondoni watakuwa wanawakumbuka sana hawa watu.