Tujikumbushe tuition za ukweli enzi hizo tukiwa madenti

Kaka umenikumbusha mbaaali sana!
madogo siku hizi wanashindia FAISI BOOK wakiuza sura na kutafuta videmu.

Kuna ticha mmoja mkaleee wa Language anaitwa USTADHI... mitaa ya TMK ANATUMIA tape kufundishia.

Mkali wa somo la GEOGRAPHY pande za ILALA MSIMBAZI CENTRE Ticha MTEGETWA alikua noma ile mbaya. anaangalia swali anakupa jibu kbla ya calculations.

ENZI HIZO MALANGALI TUNAKACHA VIPINDI SHULE MIEZI KADHAA TUMEJICHIMBIA DAR KUKAMUA KWA HAO MATICHA TUKIRUDI SHULE NI VIPANGA MPAKA MATICHA WANABROU.

KAKA ACHA SASA TULE BATA KWENYE VIYOYOZI ILIKUA FULL KUTOBOA.... DAH
hata mimi niesoma kwa mtegetwa alikuwa noma! cjui yupo wapi, madenti wa siku hizi wana visimu vya internet kutwa facebook!
 
Yani wote Mmemsahau Lindugani E.A Nililile,basi namba iliwapitia kushoto....

Aisee Babangida ni nomaaaaa
Na Mkandawile(Hyu Jamaa nasikia ana shule yake huko pugu kaanzisha,alichukua mkopo barclays mil500)
 
Geography kwa mama Msuya pale Jamhuri Primary (sasa nadhani ni sekondari) alikuwa anatupanga foleni yaani ana session karibu tano kwa siku kila kundi na mda wake.... infwacti kama sio yeye...ningekuwa nakamua machicha ya mbege kule Kirua Vunjo...... maana shule za A level hatukuwa na ticha hata mmoja na hata nilipohama yakawa yale yale...
 
elimu ya sasa haina ushindani kabisa yaani watoto wa st mary wanawakimbiza vipanga wa ilboru?!
 
kuna ticha mmoja mrefu alikuwa anafundisha fizikia sikumbuki jina lake - wanafunzi walikuwa wanajiuliza waende kwake au kwa babu kazibure (huyu mzee alikuwa hatumii kitabu kufundishia na inasemekana alikuwa anadai nelkon alisoma naye na alikuwa mchovu tu darasani hivyo hawezi kutumia kitabu chake - michoro na maswali yake yalikuwa yamekaa kama ya kitabu cha university physics!)
 
Taaarifa.......

Mkandawile alianzisha shule maeneo ya pugu kigogo fresh..... Akakopa mil. 500 benki, ashindwa kuzirejesha. Akashindwa kulipa walimu.... Walimu wakahamishia familia zao nyumbani kwa mkandawile tabata segere kwa bibi. Jamaaa akalala mbele.... Wanafunzi wakakosa mwelekeo... Sijui kilichoendele ila mdogo wangu nilimhamishia st.
 
Wakati uleeee tukisoma, kulikuwa na Tuition moja ipo pale Mwenge nyuma ya Nakiete Phamacy (MAPAMBANO TUITION CENTRE) Nakumbuka kipindi kile wanafundisha wakina Selemani matipa, Magnus kibonde a.k.a P Didy, Mussa Detebha na wengine wengi nimewasahau, kwanza tulianzia pale karibia na Magorofa ya jeshi Mwenge kwa Mzee mmoja alikuwa anaitwa Mzee Chilumba ndo tukahamia nyuma ya Nakiete Phamacy. Enzi hizo vijana tulikuwa tunasoma si mchezo, kwanza palikuwa na ushindani wa shule kwa shule ili shule yako iwe ya kwanza lazima ushike No. 1. Palikuwa hapatoshi jamani siku ya pepa. Kipindi hiko Makongo ipo chini ya Kipingu, ilikuwa makongo ya ukweli si kama ilivyo sasa! Azania ilikuwa si mchezo, Pugu nao walikuwepo, Kibasila. Forodhani, Kisutu, Jangwani, Royola, Tegeta na Jitegemee kwa mbali ingawa walikuwa wanakimbia pepa kwa sana. Namkumbuka mdada mmoja wa jangwani alikuwa anaitwa Nanzoke alikuwa ni noma kwa Mathematics! Makongo ilikuwa inabebwa na vijana wa pure mathematics. Kimbembe kilikuwa wakati wa likizo, wakija wale waliobalikiwa kiakili yaani Mzumbe, Ilboru na Kibaha + Tabora Boyz. Hawa jamaa tulikuwa tunashindana nao mpaka kinaeleweka ingawa kiukweli walikuwa juu sana. Kwa sasa nashangaa vijana hawajitumi wanafeli kila kukicha, hakuna ushindani tena baina ya shule na shule! Enzi zetu tulikuwa tunasoma si mchezo jamani ndo maana tupo hapa tulipo au wewe ulipo au nakosea?

Ebu na wewe tukumbushe Tuition yako, bila kusahau zile za ubungo, Mchikichini nk.

Naomba kuwasilisha.
sijawahi soma kitu kinachoitwa tuishen, hiyo ni kwa watu wasiojiamini.,hivi unaenda tuishen ya Geography au uchum hili iweje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom