Tujikumbushe tuition za ukweli enzi hizo tukiwa madenti

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,536
2,187
Wakati uleeee tukisoma, kulikuwa na Tuition moja ipo pale Mwenge nyuma ya Nakiete Phamacy (MAPAMBANO TUITION CENTRE) Nakumbuka kipindi kile wanafundisha wakina Selemani matipa, Magnus kibonde a.k.a P Didy, Mussa Detebha na wengine wengi nimewasahau, kwanza tulianzia pale karibia na Magorofa ya jeshi Mwenge kwa Mzee mmoja alikuwa anaitwa Mzee Chilumba ndo tukahamia nyuma ya Nakiete Phamacy. Enzi hizo vijana tulikuwa tunasoma si mchezo, kwanza palikuwa na ushindani wa shule kwa shule ili shule yako iwe ya kwanza lazima ushike No. 1. Palikuwa hapatoshi jamani siku ya pepa. Kipindi hiko Makongo ipo chini ya Kipingu, ilikuwa makongo ya ukweli si kama ilivyo sasa Palikuwepo na vijana kama Kamna Shomari, Alex mavika, Daudi Bupilipili, Pale Forodhani nawakumbuka wakina Shabani kingazi kwa sasa ni dr, Big Noise, Jangwani namkumbuka Nanzoke Mvungi sijui yuko wapi, Mzumbe namkumbuka Benjamini kamala kwasasa ni dr, Loyola namkumbuka Mtabazi, Azania nimewasahau, kibasila nimeawsahau ila walikuwepo sana tu pamoja na zanaki, Watu walikuwa wanajituma kichizi, Tegeta namkumbuka Datius Mshala kwasasa ni pirot! Azania ilikuwa si mchezo, Pugu nao walikuwepo, Kibasila. Forodhani, Kisutu, Jangwani, Royola, Tegeta na Jitegemee kwa mbali ingawa walikuwa wanakimbia pepa kwa sana. Namkumbuka mdada mmoja wa jangwani alikuwa anaitwa Nanzoke alikuwa ni noma kwa Mathematics! Makongo ilikuwa inabebwa na vijana wa pure mathematics. Kimbembe kilikuwa wakati wa likizo, wakija wale waliobalikiwa kiakili yaani Mzumbe, Ilboru na Kibaha + Tabora Boyz. Hawa jamaa tulikuwa tunashindana nao mpaka kinaeleweka ingawa kiukweli walikuwa juu sana. Kwa sasa nashangaa vijana hawajitumi wanafeli kila kukicha, hakuna ushindani tena baina ya shule na shule! Enzi zetu tulikuwa tunasoma si mchezo jamani ndo maana tupo hapa tulipo au wewe ulipo au nakosea?

Ebu na wewe tukumbushe Tuition yako, bila kusahau zile za ubungo, Mchikichini nk.

Naomba kuwasilisha.
 
Afroquick - arusha 2likuwa pale shule ya msing mbele ya st.tereza chuch wakaamia relini
 
Afroquick - arusha 2likuwa pale shule ya msing mbele ya st.tereza chuch wakaamia relini

Iyo imekaa vizuri maana mm Arusha nimekaa miaka 3, vipi ushindani wa Tuition yenu ulikuwaje ukilinganisha na sasa.
 
Mm nilikua napiga tuition moja pande za sinza inaitwa SOKWAMBI=Soma Kwa Mbinu. Nilikacha nakiete mana ilikua msongamo. Nilipiga na ya chang'ombe pia kwa mtaalam wa language. Ni kweli vijana wa sasa ni bongofleva tu.
 
M2 moja alikuwa anaitwa Mbuga..gwiji la Chemistry na Biology pale pande za mchikichini.
 
Babangida mtaalam wa Chemistry na Biology pale mchikichini,Mood mtaalamwa physics pala mchikichini (huyu alikuwa na vibwagizo vyake kama "TIME IS APPROACHING AT ZERO,LET US END HERE........." NA JINSI ANANYOONGEA BURUDANI TUPU), Makanya Magomeni, Wenzi, point 7 ya Azania ( Huyu alikuwa anawapa kiburi watoto wa Azania kujiona wao ndio zaidi mpaka wengine wakaambulia vibuyu)
 
Unamjua "Mwl So Much"

Nampata, alikuwa anashuka namba pale Migomigo!

Kwenye Kemia kulikuwa na Mama Shija pale Azania!

Fizikia alikuwepo mzee mzima Babu pale Tambaza!

PS. Kuna mwalimu wa Kemia alikuwa anapenda sana kusema 'yellow boy' - alikuwa anaitwa nani?
 
Kaka umenikumbusha mbaaali sana!
madogo siku hizi wanashindia FAISI BOOK wakiuza sura na kutafuta videmu.

Kuna ticha mmoja mkaleee wa Language anaitwa USTADHI... mitaa ya TMK ANATUMIA tape kufundishia.

Mkali wa somo la GEOGRAPHY pande za ILALA MSIMBAZI CENTRE Ticha MTEGETWA alikua noma ile mbaya. anaangalia swali anakupa jibu kbla ya calculations.

ENZI HIZO MALANGALI TUNAKACHA VIPINDI SHULE MIEZI KADHAA TUMEJICHIMBIA DAR KUKAMUA KWA HAO MATICHA TUKIRUDI SHULE NI VIPANGA MPAKA MATICHA WANABROU.

KAKA ACHA SASA TULE BATA KWENYE VIYOYOZI ILIKUA FULL KUTOBOA.... DAH
 
Mm nilikua napiga tuition moja pande za sinza inaitwa SOKWAMBI=Soma Kwa Mbinu. Nilikacha nakiete mana ilikua msongamo. Nilipiga na ya chang'ombe pia kwa mtaalam wa language. Ni kweli vijana wa sasa ni bongofleva tu.

umeona mpatanishi? masharobalo kibao kwenye elimu, wao na miziki tu, enzi hizo hata darasa la 7 tulikuwa tunapiga tuition kwa mwl. kitabu pale knyama na kwa jamaa mmoja pale shule ya msini sinza mihogoni kwa mt, alikuwa anajiita mtaalam. upo hapo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom