Fikra za Mlimwengu

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
214
229
JICHO LA MLIMWENGU

Kamwe milima huwa haikutani ni binadamu tu wanaokutana ni mojawapo ya hekima za walimwengu ambazo waliwahi kunena.
Ni Maneno yanayomtoka kinywani Shungu baada ya kupotezana na rafiki yake wa damu Koba. Wanakutana kwenye viwanja vya Nyerere Square makao makuu ya nchi ,Dodoma. Wote wameenda kuhudhuria mkutano mkuu wa vijana ambao unafanyikia Dodoma. Koba ni Mkurugenzi wa kampuni ya MANUNGU LTD ambayo inadeal na kukusanya takataka na kuzipeleka kiwandani kwa ajili ya kuzalisha malighafi nyingine(Waste Recycling) na Shungu yeye ni Afisa maendeleo wa Wilaya ya Itigi.

Kitendo cha kuonana wanakumbatiana kwa furaha sana maana mara ya mwisho kupotezana mwaka 2004 baada ya kumaliza kidato cha sita shule ya sekondari Azania. Kwa bahati nzuri Olevel walisoma shule moja ya Tegeta High school na uzuri wakachaguliwa tena kidato cha tano shule ya Azania. Urafiki wao ulichagizwa zaidi na vitu wanavyopendelea kama kucheza mpira wa miguu pamoja na kuimba. Kipindi chao cha shule Koba alikuwa anaimba hiphop na Shungu anaimba R&B. Hivyo kipindi cha enzi zao za shuleni walijulikana sana kwa sifa yao kubwa ya kuimba vizuri kutokana jinsi walivyoshirikiana. Na mashabiki wao wengi waliwapata shule za Zanaki pamoja na Jangwani.

Wakiwa bado wamekumbatiana kwa furaha.. Irene yuko wapi? Koba alimuuliza Shungu, bila kusita Koba alimjibu " Aiseee umenikumbusha mbali sana huwezi amini Irene baada ya kumaliza Jangwani alipata scholarship akaenda USA hadi sasahivi sijui chochote kuhusu yeye." Wanaangaliana na kuanza kucheka baada ya kukumbushana mbali habari za shule kama za mchikichini pamoja na coco beach. Wanasogelea sehemu yenye viti wanaketi ili wapate kuzungumza vizuri kwa kina.Koba anamuuliza Shungu " Hivi bado una sifa kama zamani?" Shungu anacheka kisha anamjibu.." Huo ulikuwa utoto nilishaacha zamani sasahivi tunafocus na maisha pamoja na kuangalia familia. Koba anacheka sana kwa majibu ya rafiki yake.. " Vipi wewe sifa zako bado unazo?" Koba anamjibu.." Mimi sifa zangu haziwezi kuisha na ndio zimepelekea nipate mafanikio ambayo niliyonayo hadi sasahivi maana bila kutaka sifa kutoka Jangwani nisingefaulu hata kidogo hii hali imenipelekea nifanye kazi kwa bidii ili niendelee kupata sifa.

Mwaka jana nilipata tuzo nchini Marekani ya utunzaji wa mazingira, mbali na kupata sifa mimi vilevile nililipatia sifa taifa langu. Na leo hii naona fahari kuwa mmojawapo wa vijana nitakaozungumza kama key speaker kwenye mkutano wa vijana. Tulichukulia vibaya kupenda sifa lakini sifa ni nzuri kuna wakati hata hapa natamani sifa nilizokuwa nazo kipindi kile cha shule zirudi nifanye makubwa zaidi ya haya. Mimi napenda kusifiwa na napenda kuwa bora ndio maana hata Shule nilikuwa namiliki mrembo mzuri shule nzima". Shungu anacheka...." hahaaha acha uwongo Irene alikuwa hamfikii Tunu wangu hapo umezidisha Koba...kumbe hujaacha mambo yako. " Sasa unataka nisifie demu wako kuwa mzuri kuliko wangu basi nitakuwa siyo mimi Koba mtoto wa kimanyema. Wote wanacheka huku wakiendelea kunywa juice ya ukwaju.

"Shungu nakuona hauko sawa kabisa siyo wewe ninayekujua vizuri. Unafanya kazi nzuri lakini hauko smart kabisa yaani ulivyo na maisha yako ni tofauti. Hauna nuru kabisa." Shungu anamjibu " Hapana kaka mambo ya kuvaa nilishaacha na siku hizi ukipendeza sana utaonekana unatumia rasilimali za nchi huu utawala ni wa kufanya kazi tu. Ndio maana unaona niko hivyo mimi nafanya kazi sana hata huu mkutano wa vijana nimechaguliwa mimi kuwakilisha mkoa kwa sababu ya uchapakazi wangu na lifestyle yangu, ukijifanya smart sana hata hawakuchagui na hapa ninapata posho ambazo zinanisaidia kusukuma maisha."

Hahahaaahaaa ! Koba anacheka.. " Nyinyi ndio mnaochafua maana sahihi ya kufanya kazi sidhani kama huko umechaguliwa kwa ajili ya muonekano wako bali wamekuchagua kwa sababu ya ubunifu ulionao kichwani mwako. Shungu i know you very well....ulikuwa mbunifu toka enzi za Umiseta na ninaamini kama ile ari ya ufanyaji kazi ungeendelea nayo hadi sasahivi ungekuwa mbali sana. Kipindi tunasoma tayari wewe unauza michoro yako kwenye magazeti. Nani ambaye alikuwa hakujui kwa Dar es salaam kipindi tunasoma. Kaka naona umefeli kwenye kukosa sifa wewe siyo wa kukaa Itigi kaka. Hapo ulipo siyo sehemu yako.... sehemu yako ni nzuri zaidi ya hiyo". What do you mean?.... "Maana yangu ni kwamba wewe siyo Shungu ninayemjua..ninasikitia kuona umemuua Shungu".... Nimemuua kivipi? nipo kaka....nina vitu vingi sana kichwani na nimeandika miradi mingi sana ila mazingira ya kazini ukijifanya unaleta mawazo mapya unaonekana unapenda sifa ndio maana huwa nakausha ipo siku nikitulia nitafanya mwenyewe.

Koba anamuangalia sana rafiki yake kisha anacheka...." Unadhani muda unakusubiri? Huu ndio muda wako wa kufanya unapoanza kupata ugonjwa wa kutotaka sifa ujue unachimbia fikra zako kaburini. Kila mtu duniani anapenda sifa, hata Rais wetu JPM anapenda sifa na ndio maana anajitahidi kufanya kazi kwa bidii ili wananchi wampe sifa na siku akiachia madaraka watu wabaki na alama ambayo kaijenga mioyoni mwao. Nashangaa wewe unasema hutaki sifa ebu rudisha sifa ulizokuwa nazo kipindi tunasoma. Nakumbuka kwenye mpira wa miguu ulikuwa na kiwango cha kawaida lakini ilikuwa tukifanya mashindano na shule jirani ulizidisha juhudi ambazo zilikuwa nje ya kiwango chako na kuonekana mchezaji mzuri. Lakini sasahivi nasikitika kuona rafiki yangu upo upo tu kama mtu ambaye hana dira. I am not proud of you kama mtu ambaye nimesoma naye. Inabidi nikutambulishe kwa rafiki zangu wengine leo kuna wawekezaji wametoka Belgium inabidi nikutane nao. Kaka ebu jenga profile yako. Wewe huoni fahari kuwa na rafiki yako kama mimi ambaye serikali inanitambua na vilevile ninaheshimika kutokana na kazi yangu ninayoifanya."
Wakati Koba anazungumza Shungu muda wote kamungalia rafiki yake usoni mwake.

Haya mazungumzo ya hawa vijana wawili yakanipelelea Mlimwengu mimi kujifunza kitu kuwa vijana wengi sasahivi hatupendi sifa ndio maana tunafanya vitu ambavyo ni wastani hatuendi beyond tumekuwa wa kawaida sana. Tumepooza tunahitaji sifa ambazo zitatutambulisha na vilevile zitakuwa ngao kwa nchi yetu. Ila tukifanya yote tukumbuke kuwa too much of anything is harmful. Huku kwetu wana kauli moja wanasema kuwa ' Bamusiima okuiruka yashaaga owaabo' ( kwamba amesifiwa anajua kukimbia amekimbia hadi akapitiliza nyumbani kwao.

Leo Jicho la Mlimwengu limeona watu wengi hawapendi sifa. Na kupenda sifa kumechukuliwa kama dhambi. Naomba niishie hapa mlimwengumimi a.k.a mpenda sifa.
#mlimwengumimi
#jicholaMlimwengu
ji.jpeg
 
Back
Top Bottom