Tujikumbushe tuition za ukweli enzi hizo tukiwa madenti

Najuta kwanini nilichelewa kuingia Jamii forum, kuna raha ya ajabu. Mnanikumbusha mbali sana, mimi nataja tuisheni za shule ya msingi kwa kuwa mliotangulia mmetaja tuishweni zote za sekondari. Mitaa ya Sinza kuna ticha alikuwa anaitwa MT (Mtaalam) huyu alipata sifa sana ya kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba. Mitaa ya Mburahati kuna ticha alikuwa anaitwa Dan, nae huyu alikuwa noma.Alikuwa na uwezo wa kumpandisha mwanafunzi kutoka maksi 20/50 akakuwezesha hadi ukapata fisi (50/50). Mitaa ya Mabibo kulikuwa na ticha aitwae Ibunga Boni, ngoja niwape mikasa ya huyu mtu. Huyu ticha alishawahi kugombana na ticha mwenzake(MT) baada ya kutunga swali la kumkashifu kwenye mtihani. Mkasa mwingine wa huyu ticha ni kwamba alishawahi kumpa ujauzito mwanafunzi wake na skendo hii iliwahi kutoka kwenye gazeti la Alasiri. Wazazi wa yule binti wakamsusia bwana Ibunga na akajichukulia mzigo kiulaini. Pamoja na mikasa yote hii huyu ticha alikuwa na sifa moja kubwa. Alikuwa mtaalamu wa kutunga mitihani ya kila wiki yenye ubora wa hali ya juu. Kingine ninachokumbuka alikuwa anawandikia wanafunzi wanaofaulu mitihani kwake shule za sekondari watakazokwenda. Mfano anakuandikia utakwenda Azania,mbinu hii ilimsaidia kupata wanafunzi wengi wanaofanya mitihani kwake. Kwa wanafunzi waliosoma shule za msingi za Manispaa ya kinondoni watakuwa wanawakumbuka sana hawa watu.
 
Mkuu Companero umenikumbusha lile book kubwa lenye cover ya rangi ya manjano: 'University Physics'. Looh, lile book lilikuwa ma maswali magumu kweli kweli.

Lile buku lilikuwa noma, halafu tulikuwa tunatumia toleo la 3 au 4 kama sikosei - kufika chuo nikakuta wanatumia toleo la 7!
 
kule sinza karibu na shule ya ubungo national housing nako kulikuwa na twisheni kali za o-level, nimesahau majina ya maticha!
 
Kwa Ustaadh, nime tuit pale hadi unapewa kanda na kaseti kusikiliza nondo. Alikua akichambua lile pamphlet la Kadhege hadi raha. Tegeta pale kulikuwa na mwl Simon sijui sikuhizi yuko wapi. Makongo Nyambizi pale ila kipindi cha likizo. Yuko wapi chai jaba? Ha ha ha kweli watu sikuhz hawasomi.
 
ubungo national housing jamaa mmoja alikuwa anaitwa mode,tulianzia maeneo ya kombozi pmrimary manzese , jamaa siku hizi anafanya kazi Tanesco.
 
unakumbuka alivyokuwa anachora michoro ya bernoulli theorem ubaoni, yaani ilikuwa kama ya kwenye vitabu !

Huyu mzee Kazibure, miaka ya nyuma kipindi cha Mwl. Nyerere, alikuwa Mkurugenzi wa RTD, alifanya mistake moja, Mwl. nyerere akamtimua. Kisa cha kwenda kushika chaki pale Kibaha Sekondary ni Huyu Kambarage! Kazibure ametufikisha hapa tulipo sasa!!!
 
Unamjua "Mwl So Much"[/QUOTE]
So Much mtaalamu wa Adv Math and Chemisrty pia alikuwa na msemo wake University siyo choo kila mtu anaweza kuingia wakati huo Watu wanaingia UDSM(2000 tu kwa mwaka UDSM).Pia kwa PHYSCIS alikuwa mzee Kazibure...
 
Namkumbuka Mwl So much akifundisha tuition Azania lile darsa la mwisho karibu na fensi ya Muhimbili. Alikuwa akishusha organic chemistry si mchezo! Pia Mzee Kazibure (RIP) akitoka Kibaha Sec. Ni kipindi hiki Mzee Ruksa akiwa Prezda wetu alipopata skendo ya kwenda kuangalia 'Isambe' wakti Madaktari wa Muhimbili wamegoma!
Wewe sasa tulisoma darasa moja AZANIA......Unawakumbuka wakina Lukaza,Mjuni,Wale mapacha wa kipare...Aswime kabunga,Mzee wa Kambi,Limamba Evarist,Kirungi Luteganya ,Anord Nzali,Aristoto Mushi,Lusajo Mwakyusa,Josephat Kyaruzi,Mabwai,Akida Mussa,eeee wanatosha,,,eeeh Rweyemamu mdogo ns mkubwa?Substance Geofrey Bakanga...eeeee
 
Mudi mmarekan kichwa cha Physics matata ebana navua kofia kwa m2 huyu LUKINGA practical za physics KIBIRITI practical ya Chemia pale Pugu.
 
Wakati uleeee tukisoma, kulikuwa na Tuition moja ipo pale Mwenge nyuma ya Nakiete Phamacy (MAPAMBANO TUITION CENTRE) Nakumbuka kipindi kile wanafundisha wakina Selemani matipa, Magnus kibonde a.k.a P Didy, Mussa Detebha na wengine wengi nimewasahau, kwanza tulianzia pale karibia na Magorofa ya jeshi Mwenge kwa Mzee mmoja alikuwa anaitwa Mzee Chilumba ndo tukahamia nyuma ya Nakiete Phamacy. Enzi hizo vijana tulikuwa tunasoma si mchezo, kwanza palikuwa na ushindani wa shule kwa shule ili shule yako iwe ya kwanza lazima ushike No. 1. Palikuwa hapatoshi jamani siku ya pepa. Kipindi hiko Makongo ipo chini ya Kipingu, ilikuwa makongo ya ukweli si kama ilivyo sasa! Azania ilikuwa si mchezo, Pugu nao walikuwepo, Kibasila. Forodhani, Kisutu, Jangwani, Royola, Tegeta na Jitegemee kwa mbali ingawa walikuwa wanakimbia pepa kwa sana. Namkumbuka mdada mmoja wa jangwani alikuwa anaitwa Nanzoke alikuwa ni noma kwa Mathematics! Makongo ilikuwa inabebwa na vijana wa pure mathematics. Kimbembe kilikuwa wakati wa likizo, wakija wale waliobalikiwa kiakili yaani Mzumbe, Ilboru na Kibaha + Tabora Boyz. Hawa jamaa tulikuwa tunashindana nao mpaka kinaeleweka ingawa kiukweli walikuwa juu sana. Kwa sasa nashangaa vijana hawajitumi wanafeli kila kukicha, hakuna ushindani tena baina ya shule na shule! Enzi zetu tulikuwa tunasoma si mchezo jamani ndo maana tupo hapa tulipo au wewe ulipo au nakosea?

Ebu na wewe tukumbushe Tuition yako, bila kusahau zile za ubungo, Mchikichini nk.

Naomba kuwasilisha.

Ndugu yangu wakati huo Jitegemee (JITE) ilikuwa noma sana, nakumbuka ilikuwa mwaka 1999 walitoa vichwa zaidi ya 5 kwenda special school, hiyo bunch ilikuwa noma sana kuna mchizi mmoja alikuwa anaitwa Golota, huyu mchizi alikuwa amekuwa akiwa wa kwanza katika miaka yake yote alipokuwa hapo, alikuwa akisoma bure muda wote kwa kuwa wakati huo wanafunzi wanaofanya vizuri shuleni hapo kwa kuwa wa kwanza, katika mikondo yote walikuwa wanapata ofa ya kusoma bure, so msela alisoma bure miaka yote 4 . Mara ya mwisho nilikutanana naye Muhimbili akiwa Daktari. Jitegemee wakati huo ilikuwa ni nimo sana. Imetoa vichwa, nilikutana na msela mmoja tuliyesoma naye akaniambia hile bunch ya 1999 imetoa Madaktari 5. wote hao walikuwa wanasoma tuition kwa Mudi na Babangida Mchikichini. Sijui sasa JITE pakoje kwasababu kitambo sana.
 
mapambano ilikuwa tution ya matozi na wauza sura.......halafu ilikuwa haitoi product za ukweli kitu mchikichini pindi sh.100 kwa aiden ilikkuwa noma mpaka vijana walikuwa wanazimia kwa jotoooo

Kijana haujui unalosema, hao wote niliokuandikia hapo juu ni product ya Mapambano na wengi wao ni Madoctor, Ebu futa kauli yako maana umedhalilisha kiti changu cha kuzunguka nilichokalia hapa
 
Ndugu yangu wakati huo Jitegemee (JITE) ilikuwa noma sana, nakumbuka ilikuwa mwaka 1999 walitoa vichwa zaidi ya 5 kwenda special school, hiyo bunch ilikuwa noma sana kuna mchizi mmoja alikuwa anaitwa Goloka, huyu mchizi alikuwa amekuwa akiwa wa kwanza katika miaka yake yote alipokuwa hapo, alikuwa akisoma bure muda wote kwa kuwa wakati huo wanafunzi wanaofanya vizuri shuleni hapo kwa kuwa wa kwanza, katika mikondo yote walikuwa wanapata ofa ya kusoma bure, so msela alisoma bure miaka yote 4 . Mara ya mwisho nilikutanana naye Muhimbili akiwa Daktari. Jitegemee wakati huo ilikuwa ni nimo sana. Imetoa vichwa, nilikutana na msela mmoja tuliyesoma naye akaniambia hile bunch ya 1999 imetoa Madaktari 5. wote hao walikuwa wanasoma tuition kwa Mudi na Babangida Mchikichini. Sijui sasa JITE pakoje kwasababu kitambo sana.

JITE ya Masawe imetoweka kaka imabakia ya kutoa Div 3, 4 na 0 tu
 
Najuta kwanini nilichelewa kuingia Jamii forum, kuna raha ya ajabu. Mnanikumbusha mbali sana, mimi nataja tuisheni za shule ya msingi kwa kuwa mliotangulia mmetaja tuishweni zote za sekondari. Mitaa ya Sinza kuna ticha alikuwa anaitwa MT (Mtaalam) huyu alipata sifa sana ya kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba. Mitaa ya Mburahati kuna ticha alikuwa anaitwa Dan, nae huyu alikuwa noma.Alikuwa na uwezo wa kumpandisha mwanafunzi kutoka maksi 20/50 akakuwezesha hadi ukapata fisi (50/50). Mitaa ya Mabibo kulikuwa na ticha aitwae Ibunga Boni, ngoja niwape mikasa ya huyu mtu. Huyu ticha alishawahi kugombana na ticha mwenzake(MT) baada ya kutunga swali la kumkashifu kwenye mtihani. Mkasa mwingine wa huyu ticha ni kwamba alishawahi kumpa ujauzito mwanafunzi wake na skendo hii iliwahi kutoka kwenye gazeti la Alasiri. Wazazi wa yule binti wakamsusia bwana Ibunga na akajichukulia mzigo kiulaini. Pamoja na mikasa yote hii huyu ticha alikuwa na sifa moja kubwa. Alikuwa mtaalamu wa kutunga mitihani ya kila wiki yenye ubora wa hali ya juu. Kingine ninachokumbuka alikuwa anawandikia wanafunzi wanaofaulu mitihani kwake shule za sekondari watakazokwenda. Mfano anakuandikia utakwenda Azania,mbinu hii ilimsaidia kupata wanafunzi wengi wanaofanya mitihani kwake. Kwa wanafunzi waliosoma shule za msingi za Manispaa ya kinondoni watakuwa wanawakumbuka sana hawa watu.

Umenikumbusha mbali sana hata mimi nisoma kwa MT, alikuwa noma we hacha tu.
 
Mwl Machagga- A leve physisc. alikuwa mwl wa Kibaha ila anafundisha tuition Jangwani weekend.
Mwl Ngalawa(RIP)- std 7 Math tuition Oysterbay primary
 
Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom