Chipolopolo
JF-Expert Member
- Feb 14, 2012
- 1,425
- 725
Ninaongea juu ya wakati wa siasa za Ujamaa na Kujitegemea zilipokuwa zimeshika hatamu.Kunawakati bidhaa ziliadimika sana. Sukari, sabuni, chumvi zikawa bidhaa za anasa kuwa nazo. Kuvipata hadi kwa mgawo zaidi ya huu wa umeme wa TANESCO, na tena ikawa kwa foleni.
Msimuliaji wangu aliyeshuhudia enzi hizo anasema wakati huo kijijini kwao huwezi kufahamu bidhaa hizo zinauzwa wapi. Ikitokea, huwa kwa kificho sana.
Mwenye bidhaa anaweka mkaa kwenye chombo kisha anaweza nje juu ya kiti. Huo ni utambulisho ya kwamba hapo kuna bidhaa inauzwa. Unachotakiwa unapanga foleni hata kama hufahamu bidhaa gani inauzwa; utafahamu mwisho wa foleni. Chakushangaza: Ukifika mwisho "unaulizwa unataka nini wewe?". "Sukari," unamjibu.
Lakini, cha kusikitisha jibu linaweza kuwa: "hapa tunauza sabuni." Kwakuwa bado unahitaji bidhaa hiyo, ulipaswa kwenda kubahatisha sehemu nyingine hadi hapo utakapo fanikiwa.
Swali ni je, uzalendo huu na uvumilivu wa kiwango hiki,ulichangiwa na nini? Je, kwa kizazi chetu hiki?