Tujikumbushe Kipindi kileeee JAMBOFORUM!!

Kulikuwa na mwanachama mmoja Brazameni Sijui alienda wapi tena; topiki zake zilikuwa skewed upande mmoja tu na akawa anajua sana kuzijengea hoja na kuzitetea, tena kwa kistaarabu sana.

Pia kina Pundit, huyu jamaa huwa namfananisha sana na Kiranga, pia kuna yule dada Mwafrika wa Kike, na wengineo wengi. Kwa JF ilikuwa JF hasa ya kumkoma nyani giladi!
 
Wakati youngafrican ilipokuwa inakufa, bsctimes ikaibuka, lakini kabla ya hapo kulikuwa na kiwanja kama nyenzi, africaonline na vingine kadhaa... Hata ujio wa Jamboforum wengi walikuwa wakipita kule Gumzo na bsctimes. Data zilikuwepo za kumwaga... na utani wa hapa na pale.

Isingekuwa jina mkubwa mbona ningekusahau! Manake nilizoea ile avatar ya Rangi ya chama. Mtu wa Pwani yupo?
 
Heheheh Mkuu Malafyale si useme tu tulikuwa watata!! Umenikumbusha mbali, akina frg, YournameIsmine, caddy, pinky, sweetNcute,hasheemThabit, cleopatra, na wengine wengi, then 2006 tukampoteza jibaba aliye kuwa ameuawa kinyama Brazil.
Mkuu bado upo kumbe...kitambo sijakuona bora ulivyoitwa huku...Jibaba gani alipotea brazil?alikuwa member hapa? Tukumbushane bro
 
Mie nakumbukia tangu nimejua jamboforum, watu kumwaga ukweli wa mambo bila mods kukimbilia kufuta threads za watu.

Yaani enzi hizo hakuna hongo kwa mods, wala mods wapendeleao mtu au watu wanaotajwa humu.
 
Heheheh Mkuu Malafyale si useme tu tulikuwa watata!! Umenikumbusha mbali, akina frg, YournameIsmine, caddy, pinky, sweetNcute,hasheemThabit, cleopatra, na wengine wengi, then 2006 tukampoteza jibaba aliye kuwa ameuawa kinyama Brazil.

Umewaacha akina Tanya,Tunu,Mrembo,Mizz,Horney na Tina aliyekuja kuwa Mke wangu mwema na Mama wa watoto wangu ahahahah!Anaye ilaumu jambo forum alaaniwe
 
Jibaba aliyekuwa na mitala jambo forum kwa wa Horny wa Dar na Mrembo kwa UK!Jibaba aliyekuwa rafiki wa Gendaeka!

Alipigwa risasi Brazil na mwenzake Misso,ulikuwa msiba mkubwa hapa

Kaka memory card yako ina gb kubwa mno. Jukuwaa wakati ule lilikuwa tamu, unatafut rafiki online na
kuchat nae live. Mwenye matusi alikuwa anapuuzwa hadi anajirekebisha, Jukuwaa za sijui siasa au mapenzi zilikuwa hazipo. Unaaanzisha topic na watu husika sanachangia, zikaingia siasa zikatuharibu.
 
Namkumbuka maraliasugu, lizzy, idimin huyu bado yupo, babu msemaovyo, wengi nimewasahau. ktk yote jukwaa la muziki lol! mwenyewe nilikuwa najisikilizia zilipendwa kwa raha zangu
Mkuu upo hapa tangu 2006
hivi kweli umepoteza kumbukumbu hivyo?....Come..on bwana tunakusubiri
"shake before use".
 
Duuh nakumbuka Jambo Forum kipindi hiko habari inaanza kama tetesi kumbe jamaa alieianzisha ana data full nondo anasubiri watu mchangie changie then anashusha vituz vilivyo kamilika toka jikoni kabisa...EPA,Richmond,Rada na madudu kibao yalikua yanaanzia JF...na nondoz zote zilikuwepo zimekamilika duuh ilikua si mchezo..siku hizi hawa madot.com wanazuka tu hawana hata data just incase wakiambiwa evidence ziko wapi??Salut JF 2009 kurudi nyuma ilikua ni balaa!!
 
Kweli wenzetu mlifaidi sana kipindi hiko, najuta kuchelewa kuijua hii kitu kwani nimekosa mengi matamu.
Hapana Juta kwani kila kitu kina muda wake mkuu...ila kiukweli enzi zile JF ilikuwa haswa kisima cha habari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom