Kulikuwa na mambo ya kuchagua gari langu, basi siku tumetoka shule tumeshagawana magari; kwamba lile la kwanza kuja litakuwa la A, la pili litakuwa la B hivyo hivyo mpaka mtu wa mwisho. Hii inakuwa wakati wa kutoka shule ile jioni.
Basi jamaa aliyekuwa namba 2 kwenye kuchagua gari lake likawa baya, akaja akang'ang'ania gari la mtu wa 3 ili yule wa 3 achukue lile la 2 baya, weeee! Mkono ukaibuka kwamba jamaa amemwibia gari, pigana pigana mpaka ticha akatufikia, kuulizia ile kesi sasa ticha alichoka mwenyewe maana hata magari yenyewe yameshapita hata hayaonekani.
Ilibidi kesho yake tuchapwe mstarini kwa kucheza michezo ya kijinga, lakini hatukukoma kugombea magari.