Tujikumbushe: Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Kenneth Kaunda wakioneshwa ramani ya ujenzi wa reli ya Tazara

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,208
4,705
Tukio hili limetokea miaka ya 1970's wakati wa mchakato wa Ujenzi wa Reli ya Tazara inayounganisha nchi za Tanzania na Zambia.

Mradi huo wa kimkakati ulifadhiliwa na na Serikali ya China.


FB_IMG_16129625723618967.jpg
 
Tazara ina urefu wa kilomita 1860.

Ni reli ya kiwango cha Cape Gauge.

ilijengwa toka mwaka 1970 mpaka 1975.

NB:
Standard Gauge Railway [sgr] ni 1435 mm.

Cape Gauge Railway ni 1067 mm.

Metre Gauge Railway ni 1000 mm.

Asante for clarifications. Kwanini Tazara inasuasua na ina kila sababu ya kufanya vizuri kibiashara?
 
kuna kitu hakiko sawa kula tunacho simamia lzm life kwa visingizio vya kutosha.
 
Huyu mzee ndio pekee aiyebaki katika timu Nyerere kwa nini UV CCM wasipange safari kwenda kumsalimia babu yao?
uvccm walivyo watu wa hovyo na mbumbumbu sidhani kama watafaidika kwa namna yoyote ile kwa kumtembelea Mzee Kaunda.
 
uvccm walivyo watu wa hovyo na mbumbumbu

NI watu hovyo na mbumbumbu kweli kwasababu hawafanyi utafiti hata kujua historia ya chama chao; wangekuwa na akili wangeweza kuwatumia watu kama marehemu Balozi Saleh Tambwe kabla ya umauti kumfika hivi karibuni, ambae alikuwa rafiki ya Rais Kaunda na walicheza sana golf pamoja wakati Tambwe alipokuwa balozi wa Tanzania Zambia. Nina hakika angeweza kuwaunganisha na Rais Kaunda na wangepata undani wa mradi wa TAZARA na hapo wangeweza kufananisha na jinsi SGR inavyotekelezwa na gharama zake.
 
Huyu mzee ndio pekee aiyebaki katika timu Nyerere kwa nini UV CCM wasipange safari kwenda kumsalimia babu yao?
Uvccm jukumu lao ni kusupport, kusema ndio na kuunga mkono juhudi zozote za serikali
 
Back
Top Bottom