Tujikumbushe adha za nyumba za kupanga

samilakadunda

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
1,780
354
Mimi nakumbuka mama mwenye nyumba alitoa amri ya wanaume wote wanatakiwa kukojoa wamechuchumaa kama wanawake,alichokuwaakifanya ukitoka chooni tu anakwenda kuangalia je? Umedosha japo tone la mkojo inje?.adhabu yake notes.je ww umewahi kutana na adha gani?
 
Naamka asubuhi,
nawasha jiko langu,
la mchina.
naweka maji ya kuoga,
baada ya kuoga,
napiga mayai matatu,
nayakaanga kwa,
kitunguu maji na kitunguu saumu.

Ghafla baba mwenye nyumba anapita kwenye korido na mayowe ya kizimwi.

Watu mnakaanga nini vya kunuka asubuhi yote hii???

Mnatutia kichefu chefu.

Maneno ya kweli hayo?
 
Usinikumbushe machungu ya nyumba za kupanga jamani.
Hyo nyumba ilikuwa ni full vituko asikwambie mtu.
Ilikuwa na vyumba 6,upande huu wanawake vyumba 3 na huu wanaume vyumba 3,afu wote hatujaolewa wala hawajaoa.
Sasa ole wako msichana mmoja wapo uingize mwanaume kutoka nje utakoma,
unanuniwa na wale wanaume.
Sema uzuri wake ilikuwa kama jumapili tunachukuana wote 6 tunaenda kutembea labda beach au bar.
Na uzuri mwingine ni kwamba wote 6 tulikuwa tunafanya kazi.
Hvyo asubh tunafunga nyumba na kutokomea.
Yani ilikuwa ni raha sana.
Sema tulihama wote baada ya mpangaji mmoja wa kiume kutaka kuzichapa na baba mwenye nyumba kisa kachukuliwa mwanamke.
 
Mi nilipewa notis baada ya kumwambia kuwa nahitaji kuoa,
Aliponiuliza nategemea kumuoa nani nikamwambia kuwa ni binti mmoja wa nyumbani kwetu,nilishangazwa na kauli yake.
Aliniambia nifanye nihame maana mi sina msaada kwake..nilipouliza kwa nini mzee?
Aliniambia etii,
Inamaana hawa mabinti zangu wote umewadharau mpaka ukaoe huko kwenu? Au unafikiri ni wanaume hawa?
Mwezi huu uwe mwisho wako kukaa hapa usiingize mwanamke wa nje kwa nyumba yangu.

Wakuu ilinibidi nihame tu kuepusha msongamano
 
zile zamu za kufagia ndo noumer. mademu kibao halafu wanataka wasio oa na wafanye usafi. mara ooh usiingie na viatu. Mia
 
Hahahahahahahahhaha

naamka asubuhi,
nawasha jiko langu,
la mchina.
Naweka maji ya kuoga,
baada ya kuoga,
napiga mayai matatu,
nayakaanga kwa,
kitunguu maji na kitunguu saumu.

Ghafla baba mwenye nyumba anapita kwenye korido na mayowe ya kizimwi.

watu mnakaanga nini vya kunuka asubuhi yote hii???

mnatutia kichefu chefu.

Maneno ya kweli hayo?
 
Ukianza tu kupika, mama mwenye nyumba atafanya kila namna achungulie mradi aone unapikia jiko gani! Sasa kosa akute unapikia jiko la umeme, anakukatieni wiki nzima na visingizio kibao!!
 
Wewe baba mwenye nyumba wetu ni noumer yaani ikifika siku za kudai kodi mtamkoma analewa mbaya
af anapiga makelele usiku kucha yaani ilikuwa hawezi kudai kodi ya pango bila kulewa lol
af cha kuchekesha zaidi anaombaga hela kila mara mwisho anajikuta analipwa 10000b yaani uswahilini kweli kazi sana
 
1. Mama mwenye nyumba atapikia sehemu ya kupikia wapangaji wote pikieni nje uwani.

2. Geiti kufunga saa mbili usiku ambaye hajarudi lazima aruke ukuta.
 
ac ha sa huku uswazi visa vingine vinatia kinyaa wamiliki wa nyumba wananyanyasa wapangaji kimtindo wengine wanawawangia kabisa wengine wanalazimisha mapenzi na wengine wanawabaka wapangaji ,unaweza kuwa mpangaiji mahali eti lazima ukipika umpatie mwenye nyumba na ole wako upukenyama kila siku af umbanie
 
Unanitonesha kidonda ndugu yangu, hapa asubuhi tu nusura nizichape na mtoto wa mwenye nyumba.
 
Namshukuru Mwenyezi Mungu [S.A.W]kwa kunifanya nisione taabu ya nyumba za kupanga.
Huu ni mwezi wa 6 tangu nimepanga,lakini mwenye nyumba hajawahi kuleta chokochoko wala nini. Ametulia,na amejenga kwange,na sisi wapangaji ametujengea nyumba yetu, unaweza kukaa hata mwezi hujamtia machoni!
So hzo taabu zianze kuanzia leo,lakini mpaka dakika hii hana tabu kabisaaaa!!
 
Jitayarishe kuwa mkwe wako.
 
umenikumbusha dah wenye nyumba noma hasa umkute mwanamama shida kibao nakumbuka nilipanga nyumba moja mama mwenye nyumba alipenda aabudiwe ukipika kitu kizuri umgawie ukiwa na kizuri chochote na yeye umpe basi mi nilikua jeuri ckufanya lolote analotaka alinichukiaje kama mke mwenzie
 
Naamka asubuhi,
nawasha jiko langu,
la mchina.
naweka maji ya kuoga,
baada ya kuoga,
napiga mayai matatu,
nayakaanga kwa,
kitunguu maji na kitunguu saumu.

Ghafla baba mwenye nyumba anapita kwenye korido na mayowe ya kizimwi.

Watu mnakaanga nini vya kunuka asubuhi yote hii???

Mnatutia kichefu chefu.

Maneno ya kweli hayo?

hahahahaha! Mbavu zangu jamani.
 
Mi nilipewa notis baada ya kumwambia kuwa nahitaji kuoa,
Aliponiuliza nategemea kumuoa nani nikamwambia kuwa ni binti mmoja wa nyumbani kwetu,nilishangazwa na kauli yake.
Aliniambia nifanye nihame maana mi sina msaada kwake..nilipouliza kwa nini mzee?
Aliniambia etii,
Inamaana hawa mabinti zangu wote umewadharau mpaka ukaoe huko kwenu? Au unafikiri ni wanaume hawa?
Mwezi huu uwe mwisho wako kukaa hapa usiingize mwanamke wa nje kwa nyumba yangu.

Wakuu ilinibidi nihame tu kuepusha msongamano

:biggrin1::biggrin1: dah makubwa kweli nyumba za kupanga zina mambo...eti ulifikiri hawa wanaume :biggrin1: eh kucheka sana asubuhi yote hii sio nzuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom