Tujikite kwenye Kiswahili au tujifunze lugha za kimataifa?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Tatizo la lugha linaendana na uwezo wa kiuchumi na ukubwa wa idadi ya watu wanaozungumza lugha husika.

Tanzania tumeanza kupigania lugha ya Kiswahili itambulike Duniani lakini tunapaswa kujiuliza tatizo ni lugha au tatizo ni kukuza uchumi?

China wapo wengi lakini maamuzi na mikataba au sheria zao zinatumia lugha za kimataifa kikiwemo kiingereza hivyo pamoja na wingi wao lugha yao haipo sokoni bali wanatumia lugha ya kiingerza na lugha nyingine kupenya sokoni. Hakuna sehemu wanahubiri watu waongee kichina ila wewe kwa mahitaji uliyonayo utalazimika kujifunza.

Sisi tupo chini sana Tena watu wengi vijiji Kiswahili kinawapiga chenga, badala tutafute kukua kupenya kwenye soko la kiingereza tupanue wigo wa ajira nje ya mipaka tunaanza kujikita kwenye Kiswahili ,huko sokoni wanahitaji lugha ya Kiswahili? Ni tunadhani tunakwama kwa sababu ya lugha ya Kiswahili?

Kiswahili kitakuwa si kwa kukiwekea mkakati bali ni kwakupanua waongea Kiswahili wawepo maeneo tofauti Duniani na njia yakuwafanya wawepo maeneo mengi nikuwahimiza wajue lugha za Dunia ili wasambae na tukitembea kila Kona Duniani tuwe tuna ndugu anayeongea Kiswahili.

Tupanue uelewa wa lugha zakigeni kwa sababu Kiswahili cha kuongea tayari tunacho
 
Wewe kama wewe jifunze kila unachoweza..., the more you know the better...

Kuhusu lugha lazima ukubali kwamba kingereza ndio kiswahili cha dunia..., ila ukijua na kichina, kijapan, kindengereko n.k. unazidi kujiuza zaidi (marketable)...

Kukuza lugha yetu hakutakuja kwa kupigiana kelele na kuhimizana bali ni kwa kuwa na vitu ambavyo watu watapenda kuvipata / kuvielewa..., kwahio wasanii na watunzi wana nafasi kubwa sana, mfano, kwa kutunga nyimbo, tamthiliya pamoja na vitabu ambavyo ni vizuri sana kupelekea watu kutaka kuelewa (Hususan nyimbo) maana tamthiliya kuna substitles..

Ni hayo tu kwa sasa....
 
Watu waongee Kihaya, Kisukuma, Kibena, Kimatumbi, ama Kizigua, shida, eti ni ukabila, wakiongea Kiingereza, shida, eti ni kuutukuza ukoloni. Wakiongea Kiswahili, heko, eti ndo uzalendo! Swali je, lugha kusudio lake ni nini hasa?
 
Wakati mwingine nikijaribu kufikiria mawazo ya viongozi wetu napata shida sana kuona kesho yetu katika maendeleo!! Kama unashindwa kuelewa KATIBA yetu inashida unawezaji kusema tatizo la nchi yetu ni lugha?

Pili ngoja nikupe siri kutoka ndani ya mfumo wetu wa Elimu “ Nilikuwa katika kituo cha kumark mtihani ya form 4 , nilijaribu kuuliza nini hatima ya Elimu yetu, aisee nilipata jibu ambalo mpka leo najaribu kuwaza naona tuma safari ndefu alafu hatujui tunaenda wapi, kiongozi anasema wanataka kuweka mfumo wa kujibu mtihani kama darasa la Saba yani ( kujibu kwa kushedi tu kwa form4)”

Kila siku nasema kama mtaala wetu umejifisha kwenye neno siasa hakika nakwambia hatuwezi kutoboa katika maendeleo yetu , na kila siku tutakuwa tunatafuta mchawi!!

Maana hao wanapiga kelele ambao ni viongozi waulize wanafeli wanakwenda wapi ( jibu watakalo kupa watakuwa bodaboda)

Kwangu mimi nitaweza kumtetea rais kama ataweza kuweka mfumo wa Elimu imara na wenye impact katika nchi, kujenga hakuna maana kama mfumo wa mtaala ni msiba.

So kwa raia wa Tanzania vitu vya kutumia akili kwao ni mtihani na mpaka mwisho hatuwezi kuwafikia wazungu!!

Yani hapa sio Kiswahili wala kingereza chenye tatizo, tatizo ni mtaala mbovu ambao hauna direction na nchi hilo ndio tatizo.
 
KiSwahili kifundishwe kama Native Language! Lakini 1. Kiingereza, 2. KiChina (Mandarin), 3. Kihispaniola 4. Kifaransa zijumuishwe katika masomo ya lugha kwa ulazima.

2025+ Utahitaji kufahamu japo lugha 4 kuweza kuwa competent enough katika masuala mbalimbali, kuanza na mikataba, teknolojia, biashara, kazi na kijamii.
 
KiSwahili kifundishwe kama Native Language! Lakini 1. Kiingereza, 2. KiChina (Mandarin), 3. Kihispaniola 4. Kifaransa zijumuishwe katika masomo ya lugha kwa ulazima.

2025+ Utahitaji kufahamu japo lugha 4 kuweza kuwa competent enough katika masuala mbalimbali, kuanza na mikataba, teknolojia, biashara, kazi na kijamii.
Mkuu. ,kiswahili iwe ni somo kama masomo mengine,,

Ila muhimu sana kujifunza

English
French.
Portuguese.
Spanish.

Hizo lugha mbili muhim sana,,ndy zinazo runs duniani.

Kichina kitoe hapo,,hakina mpango wowote.
 
Mkuu. ,kiswahili iwe ni somo kama masomo mengine...
Lugha inazidi kupata nguvu inavyokuwa na wazungumzaji wengi na inavyozidi kupata mifumo ya kiundeshaji, dunia ijayo KiChina kitakuwa baina ya lugha 4 kuu.

Spanish na Portuguese bora Spanish inauzito zaidi na imejitosheleza ni rahisi na utamuelewa Portuguese vizuri tu.

Kwangu nitapendekeza Kiingereza, KiChina, Kihispaniola na Kifaransa.
 
Tatizo la lugha linaendana na uwezo wa kiuchumi na ukubwa wa idadi ya watu wanaozungumza lugha husika....

Kwanza ni muhimu tujiulize soko la kiswahili hapa nyumbani ni wapi na kinahitajika kwa walaji wepi vivyo hivyo huko nje tujiulize ni akina nani wanataka bidhaa yetu hii " kiswahili" ama sivyo tukiingia kichwa kichwa bila bila kufanya utafiti wa kina huko mbele tutajikutaa tumebaki na masalo yetu kama muuza nyanya wa kariakoo asiyejua soko lipo wapi
 
Kiswahili kitumike kufundishia hadi chuo kikuu.
Kwa hali iliyopo sasa, na ili hii ifanyike sahihi tutahitaji kuwekeza fedha nyingi katika kutafsiri material yaliyo, hasa kwa kingereza, kwenda kiswahili.
Hii itakua ni mradi wa kudumu kwa kuwa sisi tumekua ni watumiaji na sio watengenezaji wa elimu.

Maswali ya kujiuuliza
- hao watafsiri, huko mbeleni, watajua wapi kiingereza cha kubobea kuweza kutafsiri? au tutakua na shule maalumu za kiingereza?

- tunauwezo wa kutafsiri vitabu millioni ngapi? nani atakua anaamua vipi vitafsiriwe na vipi visitafsiriwe?

- kwanini unaona option ya kuwekeza katika kutafsiri ni bora kuliko option ya kuimarisha ufundishaji wa kiingereza na kutumia kama lugha ya kufundishia?

- kuna tatitizo gani watanzania wakijua kiswahili na kiingereza kwa ufasaha?
 
Lugha inazidi kupata nguvu inavyokuwa na wazungumzaji wengi na inavyozidi kupata mifumo ya kiundeshaji, dunia ijayo KiChina kitakuwa baina ya lugha 4 kuu.

Spanish na Portuguese bora Spanish inauzito zaidi na imejitosheleza ni rahisi na utamuelewa Portuguese vizuri tu.

Kwangu nitapendekeza Kiingereza, KiChina, Kihispaniola na Kifaransa.
Ujifunze kichina uongee na jet Lee? Au nani?

Duniani lugha zinazoengelewa na mataifa mengi ni English,, French,,na Spanish..

Kichina na kihindi lugha inayoongewa na watu wengi duniani,,
Na sio mataifa mengi..
 
Back
Top Bottom