tujifunze utamaduni wa kusoma vitabu

tujifunze utamaduni wa kusoma vitabu

Reading!
idriss_quotes___Be2yR_hDtng___.jpg
idriss_quotes___Bd7wLtyjd8A___.jpg
idriss_quotes___BYkjdbaHqcN___.jpg
 
huku kwetu unanunua kitabu ama vitabu uhifadhi kabatini, vingine ni vya ulithi, vingine ni madini kwa anayevijua kuvipata watu watapata tabu sana...niliwahi kuwa na vitabu viwili sijawahi kuviona popote pale wala sikuwa najua lugha iliyoandikwa mule, hata Google haikunisaidia zaidi ya kuniletea comedy tu...nilitafuta wazee wa zamani ambao niliamini hawawezi zingua nikawaonesha, wakasema hivyo vitabu ni hatari kuliko hatari yenyewe wakivipata watu gani sijui, vina mambo makubwa na siku nikijua kuvisoma naweza hata kupotea....mh nkaona haya sasa mengine...sasa basi kuna siku katika maongezi tu ya kawaida na jamaa yangu yupo scotland, nikamgusia kuhusu vile vitabu viwili..akaomba japo screenshot aone naye kama ataambulia chochote, nikamtumia, baada ya wiki yule jamaa akasema anaweza kuja Africa kuviona? nikamwambia sio kuviona njoo uvibebe kabisa mi sivielewi elewi maana vilivyoandikwa humo ndani japo sielewi maana lakini taswira yake tuu inaonesha kama yaliyomo humo ndani ni makubwa....

zikapita siku kadhaa, na hatimae yule kijana akaja kweli, sikuwa hapa TZ kipindi hicho, nilikuwa nchi jirani, akanifuata hukohuko, alipofika tu swali la kwanza lilikuwa we hivi vitabu umevitoa wapi? Nikamwambia nilipovitoa na jinsi nilivyovutiwa na maandishi yake yalivyokaa na jinsi michoro yake na vile karatasi zake ziko kama magome ya miti, akaniuliza unaweza nipeleka kwa huyo aliyekuwa akivimiliki? nikamwambia kisha kufa.,dah, akasema naomba nivisome, nikamkusanyia nikampa..

yule jamaa alikuwa anasoma muda wote, akipumzika ni muda wa kula, au kulala, tulikaa huko nilikokuwa siku tatu kisha tukavuka kurudi Bongo akakaa haa siku tatu pia...na mwisho akaniambia ahsante sana ndugu yangu, vitabu vyako hivi hapa, mimi narudi nyumbani, nikamwambia vibebe nenda navyo akagoma, tena kagoma kama nimemwambia labda abebe vitu vya hatari...mi nikaona huu upuuzi siku anapanga mizigo yake nikamchomekea kimoja, aliofika kwao akakiona, akanipigia simu, kile kitabu kimempa shida sana kaika safari yake.

anapanga kuja Tz kukirudisha...akauliza kama kile kingine ninacho nikamwambia sina, kipo mbali sana na siwezi tena kwenda huko...sasa mwaka huu nimepigiwa simu na kaka wa jamaa akaniambia mdogo wake alitoka na kitabu gani sijui yeye alinitajia jina nikamwambia ndio, akasema hiko kitabu ndio kinamsumbua...kama nina hata karatasi moja nimebaki nayo nikitupilie mbali, kina nguvu za ajabu.....sina kitabu na wala sihitaji kuwa nacho..kuanzia kipindi hicho, hamu ya kusoma vitabu vya ajabu ikakomea hapo
 
kabisaa mkuu,mie naona hata serikali I invest kwenye makitaba ziwe nyingi nchini,

hata kama haitawavutia sie wahenga, watoto wetu wanaweza kubadilishwa taratibu huko mashuleni kuzitumia….

tena watu binafsi au makampuni pia wahamasishwe kujenga maktaba...hizo taasis za kibinadamu nazo zisiishie kutoa tu takwimu hapa kuna upungufu huu,ule bila kuwa involved kwenye solutions....
Kweli kabisa wataifiti wanakuja kusema watu wako hivi bila kuja na suruhisho lake
 
Siku hizi Smartphone zina Application za Kusoma Vitabu... Badilikeni si mpaka Mtu atembee na Mikaratasi ndo Mjue anasoma Vitabu...

Mie nina Application nina Download vitabu na Kusoma
kusoma kitabu hardcopy ni vizuri zaidi kuliko softcopy,
mimi ndio naona hivyo kwa upande wangu.
 
Hello JF,

Kielimu na nchi nyingine lets say western countries tunachotofautiana;

Ni culture ya kujisomea vitabu,

Tangia umri mdogo watoto wao wanaongozwa kusoma vitabu na kwenda library.

Watoto wanaimarishwa kuwa na 'intrest' ya kujisomea vitabu,

Si kweli wazungu wote wamefika elimu ya juu/chuoni......ila wengi wamesoma vitabu na wana general knowledge kubwa,unakuta mtu form four au six anajua mambo mengi,kwa sababu anasoma vitabu

Na sisi tunaweza use the same strategies tuwe na mkakati wa kuwa na watu wengi wanaojua general knowledge na sio wachache walioenda hadi chuo kikuu na MAJORITY kuwa gizani.

Naomba mpendekeze nini kifanyike kwa sasa kubadilisha hii culture?
Kusoma vitabu inahitaj uwe umekula umeshiba and well relaxed without life stress ndo maana inakua ngumu kwetu wa tz kuwa na utamaduni wakusoma sna vitabu kwani 70% ya wa tz ni walala hoi au ni watoto wa walala hoi
 
kama tunataka utamaduni wa kusoma vitabu uanzie utotoni kwa watu wote hatuna budi kutafsiri vitabu vingi tuwezavyo. Enzi za ujamaa vitabu vingi sana vilitafsiriwa. Nakumbuka kitabu kimoja kilikuwa kinaelezea jinsi Majeshi ya kisovieti yalivyopigana WWII na jinsi walivyoiteka Berlin. Nilikuwa primary wakati nakisoma, kingekuwa kwa kiingereza nisingekielewa. Kunatakiwa kuwa na jitihada za makusudi za kutafsiri vitabu kwa kiswahili. Vyote vilivyoisha muda wa patent vitafsiriwe na vile bora vyenye patent basi tununue ruhusa ya kuvitafsiri. Huu unatakiwa kuwa mpango kabisa.
 
Tafuta hicho kitabu cha David and Goliath usome sister,utakua mtu wa tofauti kabisa jinsi unavyo pambana na mazingira pamoja na changamoto za maisha.
Nampendaga sana. Malcom Gladwell. ila hicho David and Goliath reviewers wengi walisema hakijakaa poa basi nikahairisha kukisoma. umesoma Outliers ?
 
Nampendaga sana. Malcom Gladwell. ila hicho David and Goliath reviewers wengi walisema hakijakaa poa basi nikahairisha kukisoma. umesoma Outliers ?
Nimesoma outliers na ndiyo kilikua kitabu cha kwanza toka kwake mimi kusoma.Kitafute hicho cha David and Goliath utanipa mrejesho chief.
 
nimependa maandishi yako ila lugha imenipiga chini.
Technology has a big impact on the whole concept of literacy. Children of nowadays prefer games over books, an iPad is more interesting of course than the boring pages of a Book.[/QUOTE
 
Tatizo sio usomaji tatizo ni lugha, Vitabu vingi vizuri vimewekwa kwa Lugha ambayo wengi hatuimudu na kuishia kusoma vitu ambavyo vingi ambavyo havitusaidii.(majarida ya udaku)

Ukitaka kujua kuwa tatizo ni lugha angalia ujibuji wa maswali ya Literature huko mashuleni.

Mkuu ww umeongea ukweli ulio wazi. Elimu kubwa na vitabu vingi vipo kwa kiingereza. Kama wengi wangekuwa wanajua kiingereza ongezeko la wasoma vitabu lingekuwepo. Huwa sipati picha watu wakijifanya eti wanatetea kiswahili kwamba ni tunu ya taifa, lakini unakuta watu haohao watoto wao wanapata elimu kwa lugha ya kiingereza na wanaona fahari sana watoto wao wakiongea kiingereza kilichonyooka, na hawajivunii watoto wao kuongea kiswahili fasaha.

Kiingereza tutake tusitake ndio ilipaswa kuw lugha ya kufundishia toka chekechekea. Kiswahili kitumike mtaani tu. Hapo kiwango cha watu kujisomea vitabu na kiwango cha uelewa kingekuwa juu.
 
Siku Moja nilipata kumtazama bwana Richard S Mabala(Mwingireza/Mtanzania)-Hawa The Bus driver & Mabala The Farmer alikuwa akizungumzia kuhusu utamaduni wa kusoma vitabu,Watoto lazima wafundishwe utaratibu wa kujisomea vitabu wangali wadogo hivyo wazazi wananafasi kubwa sana katika kumuandaa Mtoto katika utamaduni wa kujisomea, kumnunulia baadhi ya vitabu na kumhmiza kusoma vitabu.

Pamoja na changamoto ya umaskini uliokithiri unaotutafuna tuliowengi lakini ni vyema kuwekeza sana katika Maarifa (vitabu) hivyo mtoto akianza utamaduni angali mdogo itamsaidia sana kupenda kujisomea vitabu mbalimbali hata akiwa mtu mzima,Hakuna Jambo gumu sana kujenga tabia ya kusoma vitabu ukubwani lakini inawezekana kwa taabu mno.

Serikali pia iwekeze sana katika Elimu vitabu mashuleni vitolewe kwa wingi walau kila mtoto aweze kumiliki kitabu chake na si kuchangia watoto wawili/watano kitabu kimoja Pia ingejenga Maktba kubwa kila kata na watu apewe Elimu na faida ya kusoma vitabu na majarida.

NINI FAIDA YA KUSOMA VITABU..??

Elimu kubwa na pana ipo nje ya mfumo wa Elimu zetu hizi,hivyo Kusoma vitabu kunafaida nyingi mno.

Jambo la msingi ni utambuzi wa vitabu gani usome na vipi usisome,Pia kusoma vitabu kwa malengo.Vitabu vinaweza kuwa Paradiso kwako au Jahanamu mbaya sana kwako lazima kuwa makini.

"Mtu anayesoma vitabu anaishi Maelfu huku mtu asiye soma vitabu huishi maramoja"

Elon Musk (Space X,Tesla Co)aliwahi kuulizwa nini siri yako yakutengeza mambo yakstaajabisha jibu lake lilikuwa moja tu-"Kwa sababu nasoma vitabu"
Elon anasoma maneno "word's" 1000 kwa Dakika moja hebu tafakari hilo,kaanza kujisomea vitabu akiwa kijana mdogo kwa siku vitabu viwili hivyo kwa mwezi kama vitabu 60.

Billionaire Warren Buffett anasoma pages 600-1000 kwa siku hebu tafakari hilo,Tesla genius alikuwa msomaji sana,orodha ya wasomaji vitabu wapo wengi na wamefanya makubwa sana,Bill gates,Marc(facebook),Sharukh khan,Barack Obama,Malcolm X,Jk Nyerere.

Utamaduni wa kujisomea vitabu unafaida lukuki,
-Unapata kuufahamu ulimwengu.
-Improves memory,
-Builds Vocabulary.
-Develops critical thinking skills.
-Reduces strees.
-Gives knowledge.
-improves writing skills.
-Improves imigination.

Inasemekana usomaji wa kitabu ndani ya dakika 6 inasaidia kupungaza " stress" kwa asilimia 68%.

"PEOPLE WHO LOVE BOOKS,LOVE PEOPLE WHO LOVE BOOK'S.

By Alisina Mwana Wa Andromeda.
 
Wa tznia ni wavivu sana katika, hata kusoma gazeti au jalida nishida wanatafuta picha tu sembuse kitabu....kama gazeti halina picha haliuzi......tena hii tabia ni kwa wote wasomi na wasio wasomi kwenye ndege wote buzy na simu kwenye basi kusizia na simu kwenye sehemu za kazi umbeya na simu nyumbani Tv na simu duh mie nachukia huu utamaduni kabisa....unakutana na mtu mzima hana maalifa mapya ya kukueleza zaidi, yakueleze eti enzi za Nyerere.
Hehe last sentence
 
Technology has a big impact on the whole concept of literacy. Children of nowadays prefer games over books, an iPad is more interesting of course than the boring pages of a Book.
I can say lack of knowledge and exposure, the majority of parents don’t understand the importance of regular reading. Poverty also contributes in this matter. How can you afford to buy a book while there is no merely a bread at home.


I couldn't say it better!
 
Shida sio kusoma vitabu , shida ni vitabu gani??? kuna wale wakukesha na vitabu vya SHIGONGO "Raisi anatembea na Mke wangu", "Mama angu anakula nyama za watu" hawa kama unawaweka kwenye kundi la wasoma vitabu basi nchi yetu inawasomaji wa vitabu wengi tu.
 
Hello JF,

Kielimu na nchi nyingine lets say western countries tunachotofautiana;

Ni culture ya kujisomea vitabu,

Tangia umri mdogo watoto wao wanaongozwa kusoma vitabu na kwenda library.

Watoto wanaimarishwa kuwa na 'intrest' ya kujisomea vitabu,

Si kweli wazungu wote wamefika elimu ya juu/chuoni......ila wengi wamesoma vitabu na wana general knowledge kubwa,unakuta mtu form four au six anajua mambo mengi,kwa sababu anasoma vitabu

Na sisi tunaweza use the same strategies tuwe na mkakati wa kuwa na watu wengi wanaojua general knowledge na sio wachache walioenda hadi chuo kikuu na MAJORITY kuwa gizani.

Naomba mpendekeze nini kifanyike kwa sasa kubadilisha hii culture?


Wonderful thread Rebeca!
Kuna kitu kina relate na hii nilijifunza mahala, but I have to dig a little deeper to come up with something insightful.
 
Rafiki yangu katoka South Korea ameka kwa miazi sita......kasema hivi sehemu zenye msogamano wa watu wengi ni public library, internet cafe, open public gardens, na museum, ....kwetu sehemu zenye msogamano sokoni, bar kumbi za starehe, basi stedi, msibani, nk.....culture yetu haiwezi huleta maendeleo tunahitaji kiongozi wa kubadisha mindset zetu ili tupate maendeleo.


Duh!, hii ngumu sana kumesa..
 
Back
Top Bottom