tujifunze utamaduni wa kusoma vitabu

tujifunze utamaduni wa kusoma vitabu

Tafuta hicho kitabu cha David and Goliath usome sister,utakua mtu wa tofauti kabisa jinsi unavyo pambana na mazingira pamoja na changamoto za maisha.

Mkuu, nimekukubali Gladwell is one of the Best.
Don't miss on his other great works too, BLINK, The Tipping Point..
 
Nipo hapa nasoma "how to win friends and influance them"..kusoma vitabu kuna shape akili sana..
 
huku kwetu unanunua kitabu ama vitabu uhifadhi kabatini, vingine ni vya ulithi, vingine ni madini kwa anayevijua kuvipata watu watapata tabu sana...niliwahi kuwa na vitabu viwili sijawahi kuviona popote pale wala sikuwa najua lugha iliyoandikwa mule, hata Google haikunisaidia zaidi ya kuniletea comedy tu...nilitafuta wazee wa zamani ambao niliamini hawawezi zingua nikawaonesha, wakasema hivyo vitabu ni hatari kuliko hatari yenyewe wakivipata watu gani sijui, vina mambo makubwa na siku nikijua kuvisoma naweza hata kupotea....mh nkaona haya sasa mengine...sasa basi kuna siku katika maongezi tu ya kawaida na jamaa yangu yupo scotland, nikamgusia kuhusu vile vitabu viwili..akaomba japo screenshot aone naye kama ataambulia chochote, nikamtumia, baada ya wiki yule jamaa akasema anaweza kuja Africa kuviona? nikamwambia sio kuviona njoo uvibebe kabisa mi sivielewi elewi maana vilivyoandikwa humo ndani japo sielewi maana lakini taswira yake tuu inaonesha kama yaliyomo humo ndani ni makubwa....

zikapita siku kadhaa, na hatimae yule kijana akaja kweli, sikuwa hapa TZ kipindi hicho, nilikuwa nchi jirani, akanifuata hukohuko, alipofika tu swali la kwanza lilikuwa we hivi vitabu umevitoa wapi? Nikamwambia nilipovitoa na jinsi nilivyovutiwa na maandishi yake yalivyokaa na jinsi michoro yake na vile karatasi zake ziko kama magome ya miti, akaniuliza unaweza nipeleka kwa huyo aliyekuwa akivimiliki? nikamwambia kisha kufa.,dah, akasema naomba nivisome, nikamkusanyia nikampa..

yule jamaa alikuwa anasoma muda wote, akipumzika ni muda wa kula, au kulala, tulikaa huko nilikokuwa siku tatu kisha tukavuka kurudi Bongo akakaa haa siku tatu pia...na mwisho akaniambia ahsante sana ndugu yangu, vitabu vyako hivi hapa, mimi narudi nyumbani, nikamwambia vibebe nenda navyo akagoma, tena kagoma kama nimemwambia labda abebe vitu vya hatari...mi nikaona huu upuuzi siku anapanga mizigo yake nikamchomekea kimoja, aliofika kwao akakiona, akanipigia simu, kile kitabu kimempa shida sana kaika safari yake.

anapanga kuja Tz kukirudisha...akauliza kama kile kingine ninacho nikamwambia sina, kipo mbali sana na siwezi tena kwenda huko...sasa mwaka huu nimepigiwa simu na kaka wa jamaa akaniambia mdogo wake alitoka na kitabu gani sijui yeye alinitajia jina nikamwambia ndio, akasema hiko kitabu ndio kinamsumbua...kama nina hata karatasi moja nimebaki nayo nikitupilie mbali, kina nguvu za ajabu.....sina kitabu na wala sihitaji kuwa nacho..kuanzia kipindi hicho, hamu ya kusoma vitabu vya ajabu ikakomea hapo
Kinaitwaje hicho kitabu?
 
kusoma vitabu ni kitu kizuri ila baadhi ya vitabu ni tabu sana kuvisoma
 
kusoma vitabu ni kitu kizuri ila baadhi ya vitabu ni tabu sana kuvisoma
Ukiona unapata tabu kusoma kitabu fulani jua hukuandikiwa wewe
Put it aside and pick up the good one for you.
 
Kupenda kusoma vitabu si kwamba ni hali tu mtu au jamii inazaliwa nayo. Isipokuwa ni ustaarabu unaoanzishwa na kuendelezwa na kurithishwa, mwisho wa siku unakuwa ni desturi ndani ya jamii/ mtu.

Ukiiangalia jamii yetu ya Tanzania hilo suala limekuwa kinyume chake. Jamii ndivyo ilivyolelewa na ndivyo inavyolelewa kwenye hiyo hali, matokeo yake jamii inaifanya ni sehemu ya Desturi hiyo hali. Cha kufanya ni kuibadilisha hiyo hali, kivipi?.. Hili suala linahitaji nguvu kutoka serikalini. Nguvu iwekezwe kwenye Elimu, nguvu iwekezwe kwenye kuielimisha Jamii.Elimu inayotolewa imfanye pia mwanafunzi aelewe kuna maarifa anayoweza kuyapata nje na kile anachosomea, nayo atayapatia kwenye kusoma vitabu mbalimbali. Wasikaririshwe kwamba maarifa ni kusoma kile unachosomea tu.

Jamii nayo vilevile iimbishwe huu wimbo kwa sababu unaweza ukatumia nguvu kubwa kwenye upande wa utoaji wa elimu kumbe wapokeaji wa hiyo elimu wakawa hawana muamko. Jamii ni nini? Ni mtu mmoja mmoja ambapo kwa ujumla ndipo wanaunda jamii. Na katika mmoja mmoja wazazi nao wapo, nao ni sehemu ya jamii. Kwa sababu licha ya wanafunzi kuwa mashuleni lakini huwa wanarudi nyumbani, kwa hiyo mzazi atacheza nafasi yake naye kwa watoto. Hii hali ikiendelezwa, ikirithishwa, ikidumishwa itaenziwa. Na ikienziwa itakuwa ni Desturi tayari.

Nguvu ya Serikali inahitajika sana kwenye hili suala. Pasipo wao itakuwa ni sawasawa na kuwinda Simba baharini. Kwa sababu Serikali ndiyo inayounda watu wake wawe wa namna gani.
 
UMEJUAJE HEBU NITAFUTIE NILICHOTAKIWA KUSOMA
Tafuta mwenyewe kiongozi wewe ndiye utasoma na utaelewa
Hicho unachosema haukielewi kuna mwingine anasoma na kuelewa sawia.

Vivyo hivyo kuna utakachosoma na ukapendezewa nacho
 
k
Tafuta mwenyewe kiongozi wewe ndiye utasoma na utaelewa
Hicho unachosema haukielewi kuna mwingine anasoma na kuelewa sawia.

Vivyo hivyo kuna utakachosoma na ukapendezewa nacho
kama una library tushirikishane basi ili nipate kujaribu
 
Naombeni mwenye kitabu cha THINK BIG kilichoandikwa na BEN CARSON anitumie hapa link nikipakue ili niweze kupata busara za huyo jamaa.
 
Back
Top Bottom