tujifunze utamaduni wa kusoma vitabu

tujifunze utamaduni wa kusoma vitabu

Hello JF,

Kielimu na nchi nyingine lets say western countries tunachotofautiana;

Ni culture ya kujisomea vitabu,

Tangia umri mdogo watoto wao wanaongozwa kusoma vitabu na kwenda library.

Watoto wanaimarishwa kuwa na 'intrest' ya kujisomea vitabu,

Si kweli wazungu wote wamefika elimu ya juu/chuoni......ila wengi wamesoma vitabu na wana general knowledge kubwa,unakuta mtu form four au six anajua mambo mengi,kwa sababu anasoma vitabu

Na sisi tunaweza use the same strategies tuwe na mkakati wa kuwa na watu wengi wanaojua general knowledge na sio wachache walioenda hadi chuo kikuu na MAJORITY kuwa gizani.

Naomba mpendekeze nini kifanyike kwa sasa kubadilisha hii culture?
Niache kutafuta hela ya kula niende nikasome vitabu?
 
Kuwa zimejaa si sababu ... Je Ushawahi kufanya utafiti kabla na baada ya smartphone kuingia hizo makitaba zimeingizaje watu.. wanaongezeka au wanapungua

mnh mkuu unabisha tu for the sake of kubisha,nenda library ya sehemu ulipo uone watu na masmartphone yao,kisha uulize ilikuwaje wako hapo library wakati wana smartphone...
 
Siku hizi Smartphone zina Application za Kusoma Vitabu... Badilikeni si mpaka Mtu atembee na Mikaratasi ndo Mjue anasoma Vitabu...

Mie nina Application nina Download vitabu na Kusoma
Kuna tofaut kubwa sana,kwenye smartphone na makaratas .
 
Wazo zuri lakini tatizo ni kwamba hata hivyo vitabu vyenyewe vingi vinaakisi mazingira na mandhari ya nchi zingine na siyo Tanzania.

Matokeo yake tunasoma sana vitabu vya wahindi na wamarekani vikiongelea changamoto na suluhisho la matatizo yanayoendana na mazingira yao.

Ndiyo hapo mtu akitaka kukitumia kama reference ya kutatua maswala yaliyopo Tz watu wengine wanamuona kituko.

Ni vitabu hivyo hivyo vimesema nchi haitaendelea kiviwanda mpaka itakapofanya mapinduzi ya kilimo ili kuandaa malighafi. Ukiwaambia hivyo sisiemu wanakuona umetumwa.
 
tembelea uone kama zinakuwaga empty...
Rafiki yangu katoka South Korea ameka kwa miazi sita......kasema hivi sehemu zenye msogamano wa watu wengi ni public library, internet cafe, open public gardens, na museum, ....kwetu sehemu zenye msogamano sokoni, bar kumbi za starehe, basi stedi, msibani, nk.....culture yetu haiwezi huleta maendeleo tunahitaji kiongozi wa kubadisha mindset zetu ili tupate maendeleo.
 
Hello JF,

Kielimu na nchi nyingine lets say western countries tunachotofautiana;

Ni culture ya kujisomea vitabu,

Tangia umri mdogo watoto wao wanaongozwa kusoma vitabu na kwenda library.

Watoto wanaimarishwa kuwa na 'intrest' ya kujisomea vitabu,

Si kweli wazungu wote wamefika elimu ya juu/chuoni......ila wengi wamesoma vitabu na wana general knowledge kubwa,unakuta mtu form four au six anajua mambo mengi,kwa sababu anasoma vitabu

Na sisi tunaweza use the same strategies tuwe na mkakati wa kuwa na watu wengi wanaojua general knowledge na sio wachache walioenda hadi chuo kikuu na MAJORITY kuwa gizani.

Naomba mpendekeze nini kifanyike kwa sasa kubadilisha hii culture?
Tupo watz wengi wasoma vitabu kama ambavyo wapo wenzetu wengi wasiosoma vitabu. Tanzania kuna vyama vingi vya wasoma vitabu. Kusoma vitabu ni hulka. Sio wenzetu wote wanasoma vitabu. General knowledge ni compulsory na haupatikani kwa kua mpenda vitabu tu. Kuanzia darasa la awali mpaka kidato cha 2 mtaala unampa nafasi mtu ya kujua mambo mengi bila kubagua. Kama upo makini utajua tu. Kuna wenzetu hawajui kuhusu logarithm lakini kwetu ni jambo la lazima kuijua logarithm labda uwe mzembe tu.
 
Leo hii ontario, zito, wakopi mada mitandaoni wanaonekana wana akili kwa sababu walikubali kupoteza muda wao na kusoma hata kwa saa mbili kwa siku.
 
Sisi sio wavivu wa kusoma tu, hata kuandika ni tatizo. Tena pengine kuandika ni tatizo kubwa kuliko kusoma.

Kwa sababu ukiingia bookshop yoyote leo, majority ya vitabu ni vya kiingereza, vilivyoandikwa na wazungu ili kukidhi matakwa na mazingira yao.

Leo hii ukitaka kitabu cha vita ya kagera itabidi usome kitabu kilichoandikwa na a certain english guy tena kwa kimombo. Someone else is writting our own history, and we don't see it as a problem!

Utamaduni wa kusoma ni lazima uende na utamaduni wa kuandika. Tunahitaji vitabu vyetu wenyewe vya historia, uchumi na siasa. Yani leo mimi naifahamu vizuri French revolution kuliko vita ya Maji maji, na sijawahi fika ufaransa!

We have to jump out of the passenger seat, and take the driving wheel.

By the way, vitabu ni hazina kuu ya maarifa. A good book can change lives of so many people out there!

Last month nimesoma vitabu vinne. Na niko kwenye utaratibu wa kuifanya hii ratiba kua sehemu ya maisha yangu.

Deuces!
 
Wazo zuri lakini tatizo ni kwamba hata hivyo vitabu vyenyewe vingi vinaakisi mazingira na mandhari ya nchi zingine na siyo Tanzania.

Matokeo yake tunasoma sana vitabu vya wahindi na wamarekani vikiongelea changamoto na suluhisho la matatizo yanayoendana na mazingira yao.

Ndiyo hapo mtu akitaka kukitumia kama reference ya kutatua maswala yaliyopo Tz watu wengine wanamuona kituko.

Ni vitabu hivyo hivyo vimesema nchi haitaendelea kiviwanda mpaka itakapofanya mapinduzi ya kilimo ili kuandaa malighafi. Ukiwaambia hivyo sisiemu wanakuona umetumwa.

umeongea jambo la msingi sana mkuu....hivyo vitabu view na contents zinazoakisi mazingira yetu…

mtoto akikua huku anasoma mazingira yake,itapelekea kuwa mwepesi kupambana na changamoto zinazoikabili jamii yake….kuwa mbunifu,,,etc

ila ni vizuro kujua na kupata exposure ya mambo ya nje pia...
 
Nimekua mpenzi wa kusoma vitabu toka niko primary,nakumbuka wilayani kwetu kulikua na bookshop moja in late 90s ambayo nilikua naenda kununua vitabu mara 2 kwa mwezi mpaka muuzaji alikua ananishangaa.

Nilijengwa na mzee toka nikiwa mdogo ambapo kila jioni alikua anatusomea hadithi toka kwenye vitabu vya picha kabla hata sijaanza shule.Kipindi kile kulikua hakuna TV so knowledge ilikua vitabuni,siku hizi disruption kila sehem kuanzia TV ,games na smartphone.

Kitu kingine ambacho kinafanya watu wasisome vitabu nadhani ni bei.Vitabu ni ghali na upatikanaji wake ni kwenye miji iliyochangamka tu,lugha pia ni shida.Bahati mbaya kwa sasa siwezi soma kitabu cha kiswahili hata sijui kwa nini.Kitabu changu nilichomaliza kusoma juzi.
 
Hizo ndo akiri za wtz na limbukeni kwaTechnologia ya mawasiliano......wenyewe wanafiri kila kitu kinachoweza kufanyika kwenye simu lazima kifanywe..mkrugenzi wa micro soft au wa compuni ya simu ya apple hotuba yake anaandikiwa kwenye karatasi na anaisoma vzr...sio kwamba hawezi kuisoma kwenye ipand, trump raisi wa dunia pia speech yake anakua typed and printed ili aisome sio kwamba hajui technology mpya ya simu.....lakini Mtazania wa Gongolaboto hataki kusoma hard copies kisa ana smart phone....huo ndo ushamba nalimbukeni ya wabongo wamakuja mjini wakiwa watu wazima ndomaana duh.
 
Baadhi ya vitabu nikivyosoma mwaka huu,pesa mingi sana.
IMG_20180804_092539.jpg
IMG_20180804_092527.jpg
1533363815481.jpg
IMG_20180804_092554.jpg
IMG_20180804_092743.jpg
IMG_20180804_092646.jpg
IMG_20180804_092707.jpg
 
kabisaa mkuu,mie naona hata serikali I invest kwenye makitaba ziwe nyingi nchini,

hata kama haitawavutia sie wahenga, watoto wetu wanaweza kubadilishwa taratibu huko mashuleni kuzitumia….

tena watu binafsi au makampuni pia wahamasishwe kujenga maktaba...hizo taasis za kibinadamu nazo zisiishie kutoa tu takwimu hapa kuna upungufu huu,ule bila kuwa involved kwenye solutions....

Tatizo sio maktaba, ni utamaduni wa kujisomea.

Wangapi wameshawahi kufika hata maktaba ya taifa kujisomea au kutafuta kitabu?

Isitoshe sasa hivi teknolojia imekuwa kubwa sana, watu wanaweza kununua au kuazima vitabu mtandaoni na kujisomea.
 
Back
Top Bottom