Tujenge tabia ya kuwatembeza watoto wetu

Tujenge tabia ya kuwatembeza watoto wetu

Ulichosema ni kweli kabisa, nakumbuka kipindi nilipokuwa mdogo baba alikuwa akinipeleka sehemu mbalimbali walipo marafiki zake wakubwa nikatembelee siku za likizo. Ilikuwa ni aghalabu sana kunikuta nakwenda likizo kwa ndugu, mara nyingi niliwatembelea marafiki zake hasa hasa waliopo vijijini.

Katika kipindi hicho nilitembelea maeneo kama vile kilwa, zanzibar, mbuga za selous, mikumi l, bwawa la mtera na maeneo mengineyo ya vijijini ambayo ni maarufu kwa shughuli fulani fulani za kiuchumi huku wenzangu wakiishia kuyaona kwenye kitabu cha maarifa ya jamii au atlas. Hii ilinifanya kukua kiakili na masomo mengi sana darasani niliyaona mepesi hasa katika zile ''case study''.

Pia ilinijengea uwezo wa kujiamini kwani mara nyingi nilikuwa nasafiri mwenyewe na mpaka hivi leo nimekuwa ni mtu wa kupenda sana kutembelea sehemu mpya na kujifunza tamaduni za sehemu tofauti tofauti.
Mm tulikuwa tunasafiri wote kila likizo tukiwa njiani anakuwa ananionyesha sehemu na kunisimulia historia yake kiukweli nimejifunza mengi, madam alichosema ni sahihi kwny huu uzi
 
Kwangu ni hobby na kizazi changu nitakikuza ivyo kupenda kujua vitu vipya kwa macho.
 
Tena kama hutaki kusumbua mtu mnafikia guest chai kwa mama ntilie mnakaa siku tatu zinatosha
Mnaweza kwenda kuona bonde la ufa na mengine mengi

Kuna mambo mengi hatufanyi ya kifamilia ambayo ni mazuri zaidi.
 
Siku hizi tunawatembeza Kwa akina Mickey and the roadster racers Disney
Uzungu umetuharibu
 
Back
Top Bottom