Tujenge tabia ya kuwatembeza watoto wetu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,267
Kutembea kunampa mtoto elimu ya ziada, pamoja na kuwa hali ni ngumu lakini likizo angalau mara moja kwa mwaka si mbaya.

Somo jigrafia mtoto akisoma aina ya milima kama alishafika Moshi na kuona mlima Kilimanjaro atakuwa na hamu Zaidi ya kujua volkano.

Kadhalika milima ya usambara ni mfano mzuri wa milima meza. Kama mtoto alishaona milima hiyo atakuwa na shauku ya kujifunza zaidi.

Unakuta wazazi wametokea Morogoro lakini mtoto wa darasa la saba anaishi Dar anakuambia hajawahi kuona mlima.

Kupanua uwezo wa watoto wetu kifikiri tuwaendeleze kwa kidogo tulichonacho
 
Ulichosema ni kweli kabisa, nakumbuka kipindi nilipokuwa mdogo baba alikuwa akinipeleka sehemu mbalimbali walipo marafiki zake wakubwa nikatembelee siku za likizo. Ilikuwa ni aghalabu sana kunikuta nakwenda likizo kwa ndugu, mara nyingi niliwatembelea marafiki zake hasa hasa waliopo vijijini.

Katika kipindi hicho nilitembelea maeneo kama vile kilwa, zanzibar, mbuga za selous, mikumi l, bwawa la mtera na maeneo mengineyo ya vijijini ambayo ni maarufu kwa shughuli fulani fulani za kiuchumi huku wenzangu wakiishia kuyaona kwenye kitabu cha maarifa ya jamii au atlas. Hii ilinifanya kukua kiakili na masomo mengi sana darasani niliyaona mepesi hasa katika zile ''case study''.

Pia ilinijengea uwezo wa kujiamini kwani mara nyingi nilikuwa nasafiri mwenyewe na mpaka hivi leo nimekuwa ni mtu wa kupenda sana kutembelea sehemu mpya na kujifunza tamaduni za sehemu tofauti tofauti.
 
Asante sana mkuu kwa kushare na sisi haya.
 
Back
Top Bottom