Shule za primary kimuundo ni nzuri kwa faida kuliko secondary. Mm ni mwalimu wa secondary, nina experience na biashara ya shule kwa takriban miaka mitano, ukianzisha primary school unapata watoto bado wadogo, ww ndo unaaanza nao, unawamold kitabia, unawapa first sight ya elimu ww, wanapata muda wa kukuzoea na kuanza kukupenda, kisha wanakuelewa. Hapo unakua na guarantee ya ufaulu wao wakimaliza darasa la saba. Ila changamoto ya sekondary ipo kwenye ufaulu tu..uwe na uhakika wa kupata pool nzuri ya watoto kutoka mashule tofauti, yaan pool nzuri kitabia lakini pia msingi wa kingereza na utayar wa watoto, experience yangu inaonesha watoto wengi wanamaliza shule ya msingi hata kiingereza hawajui, sasa na ww ndo unakabidhiwa hao watoto. Ni vgumu kufikia malengo kwakweli kwa njia hio.