Naamini Watanzania walioitazama filamu ya Royal Tour hawafiki elfu 10

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,716
36,187
Niko Dar es salaam hapa tangu Royal Tour itoke. Sijawahi kusikia mtu yeyote au kikundi cha watu mtaani wakihadithia filamu ya Royal Tour.

Mimi mwenyewe sijawahi kuiona, only kwenye vi clip vya sekunde 30 ndani ya safari channel ndo naviona.
Nilijaribu kuwauliza vijana wenzangu kazini kama wamewahi kuitazama angalau kwa lisaa limoja wote wanasema hapana. Wengine ndo kwanza hata main character hawamjui.

Hivi inawezekana Wazungu kushobokea filamu ya Kibongo ambayo hata wabongo wenyewe hatuijui?
 
Umeshawahi kuona Wachaga wakijiangaisha na kupanda mlima Kilimanjaro?

Hiyo filamu wametengenezewa wazungu kuwatangazia vivutio vya Tanzania.

Kuna channel ya TBC Tanzania Safari channel kila kitu kipo humo sasa Mtanzania royal tour kwake ya kazi gani?

Punguza chuki utapata vidonda vya tumbo ni ugonjwa mbaya Sana.
 
Bora kupakua pilau ,kuliko kupakua hiyo kitu,twiga na Simba kila siku tunawaona,mlima Kilimanjaro hatujaanza kuuona leo
 
Back
Top Bottom