Jinsi viumbe wanavyowasiliana, kujenga mashirikiano au mahusiano na viumbe wa tabaka lingine tofauti kwa kufuata kanuni maalumu

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,332
Tunatambua juu ya uwepo wa viumbe mbalimbali katika matabaka tofauti tofauti zaidi zaidi tumepata kuyajua haya kwa njia ya imani.

Leo hii tunatambua kuwa kuna kiumbe chenye uhai katika daraja la juu kabisa yaani Mungu, likifuatia daraja la malaika, halafu binadamu na mwisho ni shetani na majini(malaika wakosefu/roho chafu)

Nilichobaini ni kuwa kila kiumbe katika daraja la tabaka lake haruhusiwi au hakuna mwingiliano wa moja kwa moja na tabaka lingine ambalo kiumbe husika ajaumbwa kuishi.

Ila chakushangaza ni kuwa hakuna chakuzuia kiumbe yeyote kati ya hao mwenye nia ya kufika katika tabaka lingine kushindwa kufanikisha nia yake hiyo.

Japo hili kiumbe husika kati ya hao kutoka katika madaraja yote hapo aweze kufika au kufikisha ujumbe au kupokea taarifa au kutengeneza mahusiano yeyote au kusababisha chochote katika tabaka lingine linalokaliwa na viumbe tofauti lazima atumie njia ambayo inaingiliana au inaruhusu mkondo wa mawasiliano/mwingiliano kuwapo.

Kwa tabaka la juu zaidi na la pili yaani malaika kuleta(kubariki) au kuchukua(kuondosha) au kusababisha lolote katika tabaka lisilo mbinguni walipo wao njia inayotumika zaidi hapa ni dhamira/nia(ikikubalika na kutumainika uwa imani)

Hivyo lengo la uwepo wa msisitizo juu ya viumbe kufanya ibada,kuomba,kutoa sadaka na kuishi kwa upendo,utii n.k nikufanikisha dhamira yenye kutumainia/nia njema kuvushwa na kuleta muunganiko wa kiroho kati ya kiumbe binadamu na Mungu ili mawasiliano yaweze kuwapo kati ya mbingu na dunia na kinyume chake.

Tabaka la tatu yaani binadamu ambao ndiyo wenyeji wa dunia na tabaka la mwisho yaani shetani na majini waishio katika kiza/kuzimu, hawa uishi katika matabaka mawili tofauti lakini yaliyopakana sana yakitenganishwa na giza na mwanga pia kuonekana na kutoonekana.

Hivyo mfumo wa mawasiliano au mahusiano kati ya viumbe hivi viwili kwa wale wenye nia yakufanya hivyo iwe nzuri au mbaya yakufika katika tabaka lisilo la asili ya kiumbe katika madaraja haya mawili ya binadamu na shetani au majini,

huwa kwa njia mbili yaani kupitia njia ya dhamirio/ibada iitwayo ushirikina(ushirika na roho ovu),na njia ya pili ni kuenenda katika utaratibu ambao ni kinyume cha asili ya mwanadamu katika kusaka maarifa, yaani kujua nakuona yaliyojificha(gizani) na kuwa pia muda huo huo katika yaonekanayo kwa macho (ya nuruni)

mara nyingi hii utumiwa na wanadamu wanaojihusisha na vitendo vya tahajudi,usomaji nyota,wenye elimu au vipawa kadhaa vya kuona/kutenda au kuelewa yaliyojificha pasipo kuhusanisha na ushirikina/uchawi,

bali wote hawa yaani wachawi na wenye maarifa ya gizani na nuruni kwa wakati mmoja ufanya kosa la kupenya nakuingia katika tabaka lingine ambalo halipo kwa ajili yao.

Kwanini iwe hivi, wote tumesoma katika mafundisho ya imani kadhaa kuwa kuna viumbe vilivyoumbwa kwa roho hivi katu havionekani,kuna vilivyoumbwa na moto au upepo na kuna vilivyoumbwa na udongo wakimemo binadamu,

sasa hili uishi na binadamu wapaswa kuwa na mwili na pia ukitaka kuishi na viumbe vingine vyote ambavyo havionekani kwa kuwa vimetenganishwa tabaka lao na letu kwa kunyimwa mwili na nuru hivyo roho hizi uishi katika giza totoro.

mfano shetani na majini yakupasa uende kwao au uwakaribishe kwako kwa njia ya dhamirio la kiroho ila katika njia ya kizani/kuzimu/kutenda maovu. Sawa na ukitaka kuwasiliana na Mungu au malaika utatumia njia hiyo hiyo ya dhamirio la kiroho kuwafikia au kuwaruhusu wakufikie kwa njia ya nuru/kutenda nakukusudia mema.

Hivyo basi uonapo au kusikia kuwa jini limemvaa mtu au linajiusisha nae juwa kuwa kiumbe huyo amevuka tabaka lake la asili kama ambavyo kuna mwanadamu pia anavuka na kuingia matabaka mengine hapo juu na kuonana na viumbe au kuishi nao katika ulimwengu wao kwa ridhaa au bila ridhaa yao.

Hivyo hili kiumbe husika asikiuke kanuni husika za kuwasiliana au kuingia tabaka lingine inampasa kuzingatia njia/taratibu sahihi za kuingia huko kinyume chake nikusababisha uharibifu/uovu au machukizo katika tabaka lililovamiwa na kiumbe wa tabaka lingine.

Kwa lugha nyingine ni kuwa kama ambavyo tunasumbuliwa na roho chafu na mashetani hapa duniani kwa kuwa si mahali pao ila wanashinikiza kuwepo na kutawala vivyo hivyo na mbinguni pia mapambano hayo ufanyika kila siku katika daraja la pili la malaika,

kuzilinda ngome hizo zisiruhusu kupenya kwa roho hizo na kwa kuwa mbingu inaulinzi thabiti na ufuata kanuni za mwingiliano kwa usahihi hapana kiumbe yeyote awezaye kupenya na kuingia katika tabaka hilo kirahisi.

Kinyume chake viumbe hawa uvamia zaidi duniani na duniani pia uvamia zaidi kuzimu nakuleta dhahama kwa viumbe vya matabaka yote mawili

ambapo mwenye kuathiriwa zaidi huwa ni mwanadamu kwa kuwa yeye ni wa nuruni ambapo gizani hausiki kabisa ila wa kizani umwonea kijicho wa nuruni kama mwenye neema na hivyo utamani zaidi kumpokonya au kuishi nae katika tabaka lake lenye mwanga(nuru ya jua) na giza(kiasi na mbalamwezi)pia udongo,maji, upepo, moto, miti,wanyama,wadudu na vingi vya kupendeza anavyomiliki mwanadamu.

Ambavyo kwa namna moja uwavutia sana viumbe hawa kuisi kuwa walipaswa kuishi wao duniani hivyo ufanya mpango wa kuwa na ushirika na baadhi ya binadamu

kwa kuwalaghai nakuwafanya wawasaliti binadamu wenzao na wajitenge kabisa na dhamira ya upendo na mema(mpende jirani yako kama nafsi yako) hivyo wawe pia mbali na Mungu wao(mpende Mungu wako)

Na wakati mwingine ushinikiza kuingia katika tabaka la dunia bila kufuata utaratibu kwa njia ya mapambano ya kiroho ndiyo maana kuna idadi kubwa ya majini/mapepo huku duniani kuliko roho za binadamu huko kuzimu.

Hii inachagizwa na mwingiliano wa pande hizi mbili kuwa na wigo mpana zaidi wa machaguo ya mashirikiano/mianya mingi kuliko matabaka yale ya juu ambayo hayana njia mkato ila moja kwa moja.

Ukimwondoa Mungu pekee aliyemuumba binadamu kwa mfanowe ambaye anauwezo wakufata au kuamua kutokufuata kanuni hizi na asifungwe na asili, mfano mdogo ni kuzaliwa kwa Yesu na kufa kwake kulitimiza kanuni hii na kupalizwa kwake akapaa katika mwili na roho wake mtakatifu akatuachia duniani ilikuwa kinyume cha kanuni ya matabaka haya mawili isipokuwa dhamirio jema ambalo ni daraja halikukiukwa,

binadamu alipewa nafasi adimu ya kuchagua kati ya jema(uzima wa milele) au baya(kifo) na yeye akachagua vyote pale edeni, akapewa roho(sifa pekee waliyo nayo viumbe wengine)

Pia akapewa na mwili(unaompa starehe,shida,vishawishi na ridhiko kwa muda mfupi wa kuishi duniani ambao viumbe wengine hawana hivyo anapaswa kuamua hatima yake ndani ya muda huu akiwa na mwili aidha achague uzima wa milele ama kifo)

na pindi akifa kutegemeana na chaguo lake uangukia katika sehemu kuu tatu; Mwenye kuipenda dunia,Mwenye kuurithi ufalme wa mbinguni na Mwenye kuishia jehanamu.

Hivyo roho hizi hazipenyi kuingia tabaka lingine bila utaratibu maalumu(zitabakia katika tabaka la dunia) ni mpaka siku ile ya ufufuo na hukumu ndipo ambapo wale waliokwisha kata tiketi ya mbinguni au jehanamu wao wataunganisha moja kwa moja kwenye vituo vyao vya kazi na wale wapenda dunia(undecided) watapewa tena nafasi ya mwisho kuamua.
 
Hivyo roho hizi hazipenyi kuingia tabaka lingine bila utaratibu maalumu(zitabakia katika tabaka la dunia) ni mpaka siku ile ya ufufuo na hukumu ndipo ambapo wale waliokwisha kata tiketi ya mbinguni au jehanamu wao wataunganisha moja kwa moja kwenye vituo vyao vya kazi na wale wapenda dunia(undecided) watapewa tena nafasi ya mwisho kuamua.
asante kwa somo hili
p
 
Back
Top Bottom