Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,494
- 1,874
Uhalisia wa kilimo kiitwaacho cha kibiashara (agribusiness). Kwa uelewa wa wengi ni kutumia mbolea za viwandani kwa wingi, madawa kwa wingi kwa ajili ya kuuwa wadudu. Pia ipo mbolea (kemikali) inayopuliziwa kwenye majani, si kuunga ardhini.
Matokeo yake ekari moja unayopata gunia 5 au 10 za mpunga au alizeti kwa kilimo cha asili bila mbolea na madawa, utapata gunia 30 hadi 40.
Uhalisia, si tu kilimo cha kibiashara unachopata mavuno au mazao mengi, bali pia unapata magonjwa mengi mwilini na ardhi kuharibika kabisa. Ni kilimo cha uharibifu wa mwili kiafya na kuichakaza ardhi - udongo, maji na mimea yenyewe.
Tunajitia sumu mwilini na kuiharibu kabisa ardhi na maji yaliyomo. Je, tuendelee kulima kibiashara kwa kemikali ili tupate mazao mengi na magonjwa mengi? Kuna mantiki gani ya kupata pesa nyingi na magonjwa mengi kama kansa, kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo, kuharibu mazingira, nakadhalika?
Na uhalisia mwingine ni huu: mazao yaliyolimwa kwa asili na kuwekwa mbolea ya asili kama vile mboji na samadi au kinyesi cha kuku, ng'ombe nk.; yatakuwa na soko sana na bei kubwa, japo ni kidogo. Ni kama vile dhahabu au madini mengine yenye thamani, unapata kidogo lakini faida kubwa sana.
Na zaidi sana, ukila mazao hayo ya asili, unajenga afya njema, si kuibomoa kwa kujitia sumu mwilini. Tutafakari!
Tuanze kampeni ya agri-health (kilimo afya) na si agribusiness (kilimo biashara)! Hiyo agribusiness ya sasa ni biashara kichaa - ashakum si matusi!