Tujadili Uhalali wa Tozo Daraja la Kigamboni

Goodluck Mshana

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,271
1,119
USHURU DARAJA LA KIGAMBONI

Hongera kwa waliofanikisha mradi wa daraja la Kigamboni. Iwe ni serikali ama NSSF. Juhudi zote hizo lengo ni kumsaidia mtanzania. Kumpunguzia adha na bugdha mkazi wa Kigamboni. Kumhakikishia mwananchi usalama wa maisha yake haswa ukilinganisha na ule mchezo wa feri zetu zilizokuwa zikizima na kuharibika mara kwa mara.

Hongera Rais JPM kwa uzinduzi na hivyo kubariki matumizi yake.

Anyway, hoja yangu sio kufurahia uzinduzi wa daraja.. Ama kuzungumzia katumbuliwa kwa Bi. Anne Kilango Malecela. Hoja yangu ni malipo ya matumizi kwa daraja hilo. Labda tujiulize swali moja lakini yenye mantiki kidogo na linalobeba dhana nzima ya matumizi ya daraja.

Swali: Daraja limejengwa na Serikali au mtu binafsi?

Labda tuanze na mifano. Ukifika nchini India utakutana na madaraja, barabara na treni zenye uasili wa daraja la Kigamboni. Kwa maana ya kutoza watumiaji wake. Ukichukua barabara ya kutoka Nerhu Place mpaka ilipo Taj Mahal utakutana na vizuizi njiani. Kila baada ya kilometres kadhaa unalipia matumizi ya barabara. Malipo yote utakayoyafanya yatategemea umbali uendao. Kwa maana ya kwamba ukimua kuendesha gari lako hapa hadi Kibaha. Utalipia umbali wa Kibaha. Ukienda Mbeya au Kilimanjaro, utalipia vivyo hivyo.

Kadhalika kwenye njia za treni. Malipo yote hufanyika kwenye vituo vya treni (metro station). Ukitaka kulipa cash money utalipa. Ukitaka kutumia rechargeable card ni wewe tu. Lakini mifumo yote hii ni tofauti.

Wenzetu wana miuondo mbinu ya aina mbili. Private na Government infrastructure. Kwa miuondo msingi ambayo ni private lazima mtumiaji alipe. Achangie investment cost ili mwisho wa siku watu watengeneze faida. Upande wa pili ni wa serikali. Ambapo matumizi yake ni bure kabisa. Mwananchi halazimiki kulipia popote maana ni miradi ya serikali. Ni miradi inaonekana na kodi za wananchi. Ni miradi iliyoanzishwa kusaidia kizazi cha maskini na mtu wa daraja la kati ambaye hawezi nunua helicopter. Miradi kwaajili ya mtu asiyeweza kupewa tenda za polisi kama Lugumi.

Sasa unaweza shangaa. Kwanini watu wanatumia hiyo ya kulipia na kuacha ya bure ya serikali?! Jibu ni kwamba miuondo mbinu ya serikali ni chakavu na haijatunzwa. Road map yake ni ndevu kuelekea uendako. Hii ya private imetunzwa na humchukua muda mfupi mtumiaji kufika anakokwenda. Ina security cameras. In case unapata shida basi wahusika watakuja on the spot na kukusaidia.

Sasa daraja la Kigamboni linapaswa kulipiwa! Daraja la serikali. Mali ya wananchi wanailipia. Kuna utofauti gani kati ya daraja hili na lile la Salender, lile la Mkapa kule Kibiti, daraja la Wami n.k? Je hili limejengwa na Lugumi Investment Co. Ltd?! Hata kama limejengwa na NSSF. Je serikali haiwezi kurejesha deni hilo kwa NSSF na kuwaacha wananchi wakafaidi matunda ya kodi zao?! Kila mwaka deni la Taifa linapanda. Huyo mkopaji ni nani? Na hizo pesa huwa zinaenda wapi?

Rai yangu kwa JPM.
Mh. Rais wapo waliojenga imani kubwa na wewe. Wapo Watanzania ambao wamerejesha utamaduni wa kuwahi taarifa ya Habari ya saa mbili wakitaka kujua Rais wao kafanya nini leo. Utamaduni huu ulishatoweka na kurejea kwake ni imani ya wananchi waliyonayo kwako. Wapunguzie adha Watanzania kwa kutembea bure juu ya daraja Lao. Wapite bure maana mradi huu huenda ulikuwa ni deal la watu. Kama kweli makatibu wataenda Bungeni kwa mabasi na hivyo kuokoa kiasi hicho cha pesa. Basi pesa hiyo ikalipe deni la NSSF kama ilivyokuwa kwa pesa za sherehe za Uhuru.

Washawishi matajiri wa nchi hii kuungana na kuanzisha miradi ya treni za umeme, private roads, n.k Serikali haiwezi fanya kila kitu. Wapeni uwezo wa kuwekeza. Pawepo na monitoring and evaluation ya uendeshwaji miradi hiyo ili siku ya mwisho irudi na kuwa mali ya serikali (baada ya wao kutengeneza faida).

Daraja la Kigamboni liwe huru, lilindwe na litunze na wote. Liwe la BURE kama ilivyo TBC.

By Goodluck Mshana
 
Mkuu, suala la kamera kuibiwa limeshakanushwa. Tukirudi kwenye hoja yako ya msingi daraja limejengwa kwa ushirikiano kati ya NSSF na serikali na NSSF imetoa sehemu kubwa ya gharama hizo. Pesa za NSSF ni pesa za wastaafu na zimewekezwa pale ili siku za usoni shirika liweze kumudu kuwalipa wastaafu hao.

Umetoa mifano kwa wenzetu kuhusu wanachofanya kwenye madaraja lakini pia zipo nchi kama Sweden kuna madaraja tena ya serikali watu wanalipia toka miaka hio hadi leo. Hivyo kuwa daraja la serikali au taasisi ya serikali inaweza isiwe kigezo.

Mwisho nikuunge mkono kwa hoja kwamba, kutokana na hali ya wananchi wa Tanzania.. Serikali inaweza ama kusaidia kupunguza deni la NSSF hivyo kipindi cha wananchi kulipa kikapungua au gharama zilizoainishwa mwanzo kulipwa na mwananchi kupunguzwa na yeye kulipa pungufu maana wananchi walipaswa kulipa mpaka fedha za NSSF zirudi. Serikali kutumia ubabe kwenye deni la wastaafu, shirika linaweza kuishia kama PSPF ilivyo sasa.
 
Ok...lakini tunapishana kwa vipato.Je atakayeshindwa......itakuwaje ......na ni mstaafu anayelipwa pension na NSSF waliogharamia daraja kwa pesa zake.
Wenye magari ndio wanalipia na si waenda kwa miguu wala baiskeli. Sasa wakati kuna pantoni wenye magari walikuwa wanalipia iweje washindwe kulipia kupita kwenye daraja?! Halafu katika hali ya kawaida huwezi kumiliki gari ukakosa tozo ya pantoni au daraja maanake usingeweza hata kujaza mafuta.

Kumbuka tozo ya pantoni ni ndogo kuliko bei ya lita moja ya petroli.
 
nadhani lengo la kuweka tozo, ni kupata mapato ya kuliendesha daraja, kama vile ukarabati, ulinzi, nk. tutambue kuwa ule ni uwekezaji ni lazima tuchangie ili daraja liendelee kudumu.
 
nadhani lengo la kuweka tozo, ni kupata mapato ya kuliendesha daraja, kama vile ukarabati, ulinzi, nk. tutambue kuwa ule ni uwekezaji ni lazima tuchangie ili daraja liendelee kudumu.
Kama tutadhibiti matumizi ya mapato na huu uwizi..hakuna haja ya kulipia.Ulaya kama vile Sweden wanalipia kuongeza kipato ili watuletee misaada na sisi tunaiiba....SHAME ON US.
 
nadhani lengo la kuweka tozo, ni kupata mapato ya kuliendesha daraja, kama vile ukarabati, ulinzi, nk. tutambue kuwa ule ni uwekezaji ni lazima tuchangie ili daraja liendelee kudumu.

Sehemu kubwa ya kulipia ni kurudisha gharama za uwekezaji kwa shirika la taifa la hifadhi ya jamii
 
tuelewe kuwa kwa maendeleo ya nchi yoyote, tozo ni faida kwa taifa, ika isiumize watu. waenda kwa miguu waliokuwa wanalipia ktk pantoni , darajani watapita bure. wenye vyombo vya moto watalipia kidogo. bila tozo hiyo, ulinzi, ukarabati mdogomdogo na mengineyo havitafanyika. so hamna shid.a
 
Ok...lakini tunapishana kwa vipato.Je atakayeshindwa......itakuwaje ......na ni mstaafu anayelipwa pension na NSSF waliogharamia daraja kwa pesa zake.
Hivi wanachama wa NSSF waliukizwa kama wamekubali fedha zao zitumike katika ujenzi wa daraja la kulipia?

Maana kama hawajaulizwa makisa yanaongezeka.

1. Hawajaulizwa hela zao kutumika kujenga daraja.

2. Hela zao zimetumika kujenga daraja.

3. Baada ya hela zao kutumika kujenga daraja, wanachangishwa tena kuzirudisha fedha zao. Hivyo wanachangia NSSF mara mbili au zaidi.
 
Back
Top Bottom