Daraja la Nyerere foleni kuvuka na magari imekua kubwa NSSF mnatengeneza foleni

byakunu

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
513
1,141
Hili daraja sasa limeshaanza kuwa kero, Kigamboni inakua watu wanaongezeka, magari yanaongezeka lakini daraja gate out na gate in ni zile zile, na zinazidiwa sasa.

IMG_4469.jpg

Imefika wakati foleni inajaa upande wa magari yanayotoka mjini kuingia kigamboni foleni inaanzia mpaka kwenye daraja lenyewe.

NSSF mnatafakari nini katika kukabili hili ongezeko kubwa la watu? Ongezeko la magari na vyombo vingine vinavyotegemea hii njia?

Muda wa hizi foleni, Watu wanakuwa wamechoka wametoka makazini lakini hapa anaweza maliza nusu saa nzima kupenya penya kuja gate out.

Hili nalo mkalitizame
 
Je, ongezeko hilo ni kwa sababu gani?

1. Ongezeko la wakazi wenye magari?

2. Ubovu wa vivuko Kivukoni?

3. Uwepo wa barabara mpya ya Kilwa hivyo magari mengi kuitumia sasa?

4. Ukuaji wa mji wa Kigamboni?
 
Mtoa mada umeongeza chumvi, nimepita muda huu ni kweli kulikuwa na foleni ila hata ikiwa darajani haichukui dakika kumi kuvuka(nilifanya timing siju moja).
Je kila siku foleni inakuwa ndefu?
Ukiona foleni imekuwa ndefu ujue gari zilinasa njia ya bandarini hivyo pakifunguka gari nyingi sana zinafika darajani kwa wakati mmoja. Hata ungekuwa na mageti mangapi situation kama hii lazima foleni iwepo.
Kama NSSF watasoma hapa nawashauri waweke gate maalum kwa wale wa CASHLESS kama walivyoweka gate maalum la bodaboda limesaidia sana kuondoa vurugu.
 
Back
Top Bottom