Tujadili Uhalali wa Tozo Daraja la Kigamboni

Tujadili Uhalali wa Tozo Daraja la Kigamboni

Hivi wanachama wa NSSF waliukizwa kama wamekubali fedha zao zitumike katika ujenzi wa daraja la kulipia?

Maana kama hawajaulizwa makisa yanaongezeka.

1. Hawajaulizwa hela zao kutumika kujenga daraja.

2. Hela zao zimetumika kujenga daraja.

3. Baada ya hela zao kutumika kujenga daraja, wanachangishwa tena kuzirudisha fedha zao. Hivyo wanachangia NSSF mara mbili au zaidi.

Mkuu nadhani umechokoza ili usikie watu wanasemaje lakini unajua jibu la swali lako.
  • NSSF inachukua makato ya wafanyakazi watakayowalipa baadae (uzeeni).
  • Wana fiduciary responsibility kupitia board of directors kuwekeza na kukuza hizi fedha za wafanyakazi.
  • Kuwekeza kwenye daraja, gesi, nishati ni sawa tu na benki ya biashara kuchukua hela za wateja na ku-invest kwenye miradi.
  • Benki ya biashara haituulizi kama tunaridhia savings zetu ziwekezwe kwenye gesi au uzalishaji umeme.
  • Umeme ukizalishwa kwa mkopo kutoka benki ya biashara (hela zetu) bado itabidi tulipie umeme (kwa bei ya faida kwa wawekezaji).
 
Unalinganisha benki ya biashara na malipo ya uzeeni. Viwili hivi ni tofauti katika namna ya msingi.

Kwanza, kwenye benki ya biashara una uwezo wa kutoa fedha zako wakati wowote bila masharti.

Katika mfuko wa malipo ya uzeeni huna uwezo huo. Not without being penalized. Hiyo ni tofauti moja tu ya msingi inayofanya mfano wako usiwe na mantiki kwa sababu unalinganisha vitu viwili tofauti.
 
Point ya msingi ni uhalali wa tozo katika kulitumia daraja la kigamboni, tunakwenda nje ya mada.
 
Bora lipo tulipie kuliko lisingekuwepo na tusingelipia kitu. I mean something is better than nothing
 
Unalinganisha benki ya biashara na malipo ya uzeeni. Viwili hivi ni tofauti katika namna ya msingi.

Kwanza, kwenye benki ya biashara una uwezo wa kutoa fedha zako wakati wowote bila masharti.

Katika mfuko wa malipo ya uzeeni huna uwezo huo. Not without being penalized. Hiyo ni tofauti moja tu ya msingi inayofanya mfano wako usiwe na mantiki kwa sababu unalinganisha vitu viwili tofauti.

Lakini mkuu hata hizi retirement accounts za huku majuu (kama IRA, Fidelity-IRA, n.k.) huwa hawatuulizi wanapofanya investments na hela zetu. Kila quarter watakuletea ripoti tu ya matokeo ya uwekezaji wao lakini hawaombi ruhsa wakati wanapowekeza.

Quarterly report za NSSF za uwekezaji wao ziko bayana wakati wowote (sio tu kama chombo cha serikali bali kama wadhamini wa hela za watu). Cha muhimu ni kuwa mahesabu ya NSSF husimamiwa na bunge na hukaguliwa na serikali (CAG).
 
Lakini mkuu hata hizi retirement accounts za huku majuu (kama IRA, Fidelity-IRA, n.k.) huwa hawatuulizi wanapofanya investments na hela zetu. Kila quarter watakuletea ripoti tu ya matokeo ya uwekezaji wao lakini hawaombi ruhsa wakati wanapowekeza.

Quarterly report za NSSF za uwekezaji wao ziko bayana wakati wowote (sio tu kama chombo cha serikali bali kama wadhamini wa hela za watu). Cha muhimu ni kuwa mahesabu ya NSSF husimamiwa na bunge na hukaguliwa na seriukali (CAG).
Retirmenet accounts kama za IRA Fidelity etc unapewa online access, unatengeneza username na password, unapewa option uchague mwenyewe unataka investment strategy yako iwe vipi.

Mimi ninayo yangu Principal.com, hata sasa hivi nikitaka kubadili investment strategy yangu sihitaji hata kuongea na mtu. Na log in online www.principal.com na kubadilisha tu.

Kama ni kijana ndiyo unaanza kuchangia unashauriwa uwe aggressive, kama unakaribia kustaafu unashauriwa kuwa conservative. Wanapokutumia ripoti wanakuonyesha funds zote walizo invest na performance yake. Kwa wenzetu huwezi kuchagua funds/ stocks moja moja kwa sababu ni nyingi sana, ila una uwezo wa kuchagua investment strategy na how aggressive/ conservative you want to be. Kwa hiyo una choice.

Halafu, kingine, hizo funds kama IRA, Fidelity etc si sawa na NSSF. Hizo ni retirement funds zinazokuwa managed na private industry. Kwa hiyo bado unalinganisha vitu tofauti.

Retirement funds kama za NSSF unaweza kuzilinganisha na Social Security hapa US. Hela za Social Security haziwi invested nje ya government bonds ambazo ni ultra safe, with low returns. The main objective is wealth preservation, not investment. Ndiyo maana kila siku unasikia Social Security itakuwa affected sana na inlation.

George W. Bush alijaribu kui privatize Social Security akashindwa. Baada ya financial crisis ya 2008 watu wakaelewa kwa nini Social Security kuingizwa katika mifuko ya investment na private industry ilikuwa a crazy idea.
 
USHURU DARAJA LA KIGAMBONI

Hongera kwa waliofanikisha mradi wa daraja la Kigamboni. Iwe ni serikali ama NSSF. Juhudi zote hizo lengo ni kumsaidia mtanzania. Kumpunguzia adha na bugdha mkazi wa Kigamboni. Kumhakikishia mwananchi usalama wa maisha yake haswa ukilinganisha na ule mchezo wa feri zetu zilizokuwa zikizima na kuharibika mara kwa mara.

Hongera Rais JPM kwa uzinduzi na hivyo kubariki matumizi yake.

Anyway, hoja yangu sio kufurahia uzinduzi wa daraja.. Ama kuzungumzia katumbuliwa kwa Bi. Anne Kilango Malecela. Hoja yangu ni malipo ya matumizi kwa daraja hilo. Labda tujiulize swali moja lakini yenye mantiki kidogo na linalobeba dhana nzima ya matumizi ya daraja.

Swali: Daraja limejengwa na Serikali au mtu binafsi?

Labda tuanze na mifano. Ukifika nchini India utakutana na madaraja, barabara na treni zenye uasili wa daraja la Kigamboni. Kwa maana ya kutoza watumiaji wake. Ukichukua barabara ya kutoka Nerhu Place mpaka ilipo Taj Mahal utakutana na vizuizi njiani. Kila baada ya kilometres kadhaa unalipia matumizi ya barabara. Malipo yote utakayoyafanya yatategemea umbali uendao. Kwa maana ya kwamba ukimua kuendesha gari lako hapa hadi Kibaha. Utalipia umbali wa Kibaha. Ukienda Mbeya au Kilimanjaro, utalipia vivyo hivyo.

Kadhalika kwenye njia za treni. Malipo yote hufanyika kwenye vituo vya treni (metro station). Ukitaka kulipa cash money utalipa. Ukitaka kutumia rechargeable card ni wewe tu. Lakini mifumo yote hii ni tofauti.

Wenzetu wana miuondo mbinu ya aina mbili. Private na Government infrastructure. Kwa miuondo msingi ambayo ni private lazima mtumiaji alipe. Achangie investment cost ili mwisho wa siku watu watengeneze faida. Upande wa pili ni wa serikali. Ambapo matumizi yake ni bure kabisa. Mwananchi halazimiki kulipia popote maana ni miradi ya serikali. Ni miradi inaonekana na kodi za wananchi. Ni miradi iliyoanzishwa kusaidia kizazi cha maskini na mtu wa daraja la kati ambaye hawezi nunua helicopter. Miradi kwaajili ya mtu asiyeweza kupewa tenda za polisi kama Lugumi.

Sasa unaweza shangaa. Kwanini watu wanatumia hiyo ya kulipia na kuacha ya bure ya serikali?! Jibu ni kwamba miuondo mbinu ya serikali ni chakavu na haijatunzwa. Road map yake ni ndevu kuelekea uendako. Hii ya private imetunzwa na humchukua muda mfupi mtumiaji kufika anakokwenda. Ina security cameras. In case unapata shida basi wahusika watakuja on the spot na kukusaidia.

Sasa daraja la Kigamboni linapaswa kulipiwa! Daraja la serikali. Mali ya wananchi wanailipia. Kuna utofauti gani kati ya daraja hili na lile la Salender, lile la Mkapa kule Kibiti, daraja la Wami n.k? Je hili limejengwa na Lugumi Investment Co. Ltd?! Hata kama limejengwa na NSSF. Je serikali haiwezi kurejesha deni hilo kwa NSSF na kuwaacha wananchi wakafaidi matunda ya kodi zao?! Kila mwaka deni la Taifa linapanda. Huyo mkopaji ni nani? Na hizo pesa huwa zinaenda wapi?

Rai yangu kwa JPM.
Mh. Rais wapo waliojenga imani kubwa na wewe. Wapo Watanzania ambao wamerejesha utamaduni wa kuwahi taarifa ya Habari ya saa mbili wakitaka kujua Rais wao kafanya nini leo. Utamaduni huu ulishatoweka na kurejea kwake ni imani ya wananchi waliyonayo kwako. Wapunguzie adha Watanzania kwa kutembea bure juu ya daraja Lao. Wapite bure maana mradi huu huenda ulikuwa ni deal la watu. Kama kweli makatibu wataenda Bungeni kwa mabasi na hivyo kuokoa kiasi hicho cha pesa. Basi pesa hiyo ikalipe deni la NSSF kama ilivyokuwa kwa pesa za sherehe za Uhuru.

Washawishi matajiri wa nchi hii kuungana na kuanzisha miradi ya treni za umeme, private roads, n.k Serikali haiwezi fanya kila kitu. Wapeni uwezo wa kuwekeza. Pawepo na monitoring and evaluation ya uendeshwaji miradi hiyo ili siku ya mwisho irudi na kuwa mali ya serikali (baada ya wao kutengeneza faida).

Daraja la Kigamboni liwe huru, lilindwe na litunze na wote. Liwe la BURE kama ilivyo TBC.

By Goodluck Mshana

Magari ya mafuta ndo walipie kwa sababu daraja limejengwa kwa ajili yao.
 
Retirmenet accounts kama za IRA Fidelity etc unapewa online access, unatengeneza username na password, unapewa option uchague mwenyewe unataka investment strategy yako iwe vipi.

Mimi ninayo yangu Principal.com, hata sasa hivi nikitaka kubadili investment strategy yangu sihitaji hata kuongea na mtu. Na log in online www.principal.com na kubadilisha tu.

Kama ni kijana ndiyo unaanza kuchangia unashauriwa uwe aggressive, kama unakaribia kustaafu unashauriwa kuwa conservative. Wanapokutumia ripoti wanakuonyesha funds zote walizo invest na performance yake. Kwa wenzetu huwezi kuchagua funds/ stocks moja moja kwa sababu ni nyingi sana, ila una uwezo wa kuchagua investment strategy na how aggressive/ conservative you want to be. Kwa hiyo una choice.

Halafu, kingine, hizo funds kama IRA, Fidelity etc si sawa na NSSF. Hizo ni retirement funds zinazokuwa managed na private industry. Kwa hiyo bado unalinganisha vitu tofauti.

Retirement funds kama za NSSF unaweza kuzilinganisha na Social Security hapa US. Hela za Social Security haziwi invested nje ya government bonds ambazo ni ultra safe, with low returns. The main objective is wealth preservation, not investment. Ndiyo maana kila siku unasikia Social Security itakuwa affected sana na inlation.

George W. Bush alijaribu kui privatize Social Security akashindwa. Baada ya financial crisis ya 2008 watu wakaelewa kwa nini Social Security kuingizwa katika mifuko ya investment na private industry ilikuwa a crazy idea.

Sawa kabisa mkuu.

Sasa tuchukulie Social Security Funds kama sawa na NSSF funds. NSSF imenunua government bonds za Tanzania ili ku-finance 60% ya mradi wa daraja. NSSF haikusanyi mapato ya wanaotumia daraja - serikali ndio inayokusanya. Wao wanasubiri serikali iwalipe dividends za bonds walizonunua na kupata mkupuo wa mwisho bond zikiiva.

Kama ilivyo Social Security Fund inavyonunua govt. bonds za marekani ndivyo ilivyo NSSF ilivyonunua bonds za serikali ya Tanzania. Wajenzi wa daraja ni serikali ya Tanzania. Hiki kima kilichotoka NSSF ni mkopo tu. Kingeweza kutoka benki ya dunia, uchina, n.k.

Kwa maneno mengine, NSSF hawakupaswa kuomba ruhsa kwa wawekezaji (wafanyakazi) kuikopesha serikali 60% ya gharama za ujenzi wa daraja kwa sababu malipo yake hayana utata (not a risky investment).
 
Hii tabia ya kupenda vitu vya bure ndo maana nchi haindelei. Unawezaje kununua gari hala ushindwe kulipia tozo ya daraja, maana sasa huko unakoelekea ni kushindwa kununua mafuta ya hilo gari. Aidha, kama mtu atashindwa kulipa tozo ya daraja, anaweza kwenda kutumia ferry maana bado itakuwepo.
Mbona daraja la mkapa hawalipi? au kwakuwa lile lipo kijijini?
 
Tozo ni kwa ajili ya maintanance..tena ni jambo la kawaida sana. Tubadilikeni Watanzania.
 
Kesho mwanangu ataanza kulipa hela ya kura nyumbani, ili niendeshe maisha ya familia.
 
Hutaki kulipia daraja panda kivuko au piga mbizi.
 
Hiv majuz nimepita hapo darajani tukalipishwa 1500 kuvuka na wakati wa kurudi tukalipa tena 1500 ingine yaan jumla 3000!

Nikajiuliza mbona tozo hizi ni kubwa hivo kama daraja la utalii? llhali hilo daraja litakuwepo hapo kwa zaidi ya miaka 100 ijayo. Huo uharaka wa kurudisha pesa ya uwekezaji unatoka wapi? Naamini ilitakiwa waweke tozo ndogo ili kuvutia watu wavuke na kupunguza misongano kwenye barabara zingine.

Nachokiona hapo wahusika hawajatumia akili walichofanya ni kukopi na kupesti tozo za pale kivukoni na wakajitoa ufahamu kuwa vivuko vina mahesabu tofauti kabisa na daraja.

Ushauri; Tozo ziangaliwe upya na wananchi washirikishwe kikamilifu.
 
Back
Top Bottom