Tujadili Uhalali wa Tozo Daraja la Kigamboni

Tujadili Uhalali wa Tozo Daraja la Kigamboni

Watanzania tumezoea kuibiwa,ukienda mombasa kivuko cha likoni kinavusha 24/7 na haulipi hata shiringi moja,ghalama zote wanabeba wenye magari ya kuanzia ton3,wengine wote bure,watanzania tunaambiwa tupige mbizi kama kambale,nchi ya kina lugumi hii tuwaachie wenyewe.
 
Hivi mnaposema " daraja limejengwa na NSSF na Serikali " mnamaanisha nini?!

NSSF ni shirika la serikali
Wizara ya Ujenzi ni wizara ya serikali. Itoshe tu kusema Daraja la Kigamboni ni la Serikali....
 
Ok...lakini tunapishana kwa vipato.Je atakayeshindwa......itakuwaje ......na ni mstaafu anayelipwa pension na NSSF waliogharamia daraja kwa pesa zake.
Hii tabia ya kupenda vitu vya bure ndo maana nchi haindelei. Unawezaje kununua gari hala ushindwe kulipia tozo ya daraja, maana sasa huko unakoelekea ni kushindwa kununua mafuta ya hilo gari. Aidha, kama mtu atashindwa kulipa tozo ya daraja, anaweza kwenda kutumia ferry maana bado itakuwepo.
 
Tatizo tumechelewa kupata ivyo vitu ndio maana vinaonekana ni hatari unalipia daraja...kuna madaraja makubwa zaidi ya ilo kama Tete..msumbiji..Zambia na Namibia..Zambia na Zimbabwe Chirundu boarder..Botswana kuna madaraja makubwa sana maana kuna mito mikubwa ni bure..sema Bongo gari sijui linaonekana ni kitu gani..
 
Hivi mnaposema " daraja limejengwa na NSSF na Serikali " mnamaanisha nini?!

NSSF ni shirika la serikali
Wizara ya Ujenzi ni wizara ya serikali. Itoshe tu kusema Daraja la Kigamboni ni la Serikali....[/QUOT
USHURU DARAJA LA KIGAMBONI

Hongera kwa waliofanikisha mradi wa daraja la Kigamboni. Iwe ni serikali ama NSSF. Juhudi zote hizo lengo ni kumsaidia mtanzania. Kumpunguzia adha na bugdha mkazi wa Kigamboni. Kumhakikishia mwananchi usalama wa maisha yake haswa ukilinganisha na ule mchezo wa feri zetu zilizokuwa zikizima na kuharibika mara kwa mara.

Hongera Rais JPM kwa uzinduzi na hivyo kubariki matumizi yake. Lakini nitoe pole kwa kuibwa kwa security cameras 4! Hii ni aibu kwa vijana wa kitanzania. Hujaikomoa serikali bali umejikomoa wewe na sisi tusio husika na wizi wako. Pesa za kununua camera mpya hazitoki mfukoni mwa JPM, Majaliwa au Anne Kilango! Ni kodi itakayolipa. Ni sisi tunaokamuliwa PAYE ndio waathirika wa moja kwa moja na wizi huo. Shame!

Anyway, hoja yangu sio kujadili security cameras na wizi wake. Wala kufurahia uzinduzi wa daraja.. Ama kuzungumzia katumbuliwa kwa Bi. Anne Kilango Malecela. Hoja yangu ni malipo ya matumizi kwa daraja hilo. Labda tujiulize swali moja lakini yenye mantiki kidogo na linalobeba dhana nzima ya matumizi ya daraja.

Swali: Daraja limejengwa na Serikali au mtu binafsi?

Labda tuanze na mifano. Ukifika nchini India utakutana na madaraja, barabara na treni zenye uasili wa daraja la Kigamboni. Kwa maana ya kutoza watumiaji wake. Ukichukua barabara ya kutoka Nerhu Place mpaka ilipo Taj Mahal utakutana na vizuizi njiani. Kila baada ya kilometres kadhaa unalipia matumizi ya barabara. Malipo yote utakayoyafanya yatategemea umbali uendao. Kwa maana ya kwamba ukimua kuendesha gari lako hapa hadi Kibaha. Utalipia umbali wa Kibaha. Ukienda Mbeya au Kilimanjaro, utalipia vivyo hivyo.

Kadhalika kwenye njia za treni. Malipo yote hufanyika kwenye vituo vya treni (metro station). Ukitaka kulipa cash money utalipa. Ukitaka kutumia rechargeable card ni wewe tu. Lakini mifumo yote hii ni tofauti.

Wenzetu wana miuondo mbinu ya aina mbili. Private na Government infrastructure. Kwa miuondo msingi ambayo ni private lazima mtumiaji alipe. Achangie investment cost ili mwisho wa siku watu watengeneze faida. Upande wa pili ni wa serikali. Ambapo matumizi yake ni bure kabisa. Mwananchi halazimiki kulipia popote maana ni miradi ya serikali. Ni miradi inaonekana na kodi za wananchi. Ni miradi iliyoanzishwa kusaidia kizazi cha maskini na mtu wa daraja la kati ambaye hawezi nunua helicopter. Miradi kwaajili ya mtu asiyeweza kupewa tenda za polisi kama Lugumi.

Sasa unaweza shangaa. Kwanini watu wanatumia hiyo ya kulipia na kuacha ya bure ya serikali?! Jibu ni kwamba miuondo mbinu ya serikali ni chakavu na haijatunzwa. Road map yake ni ndevu kuelekea uendako. Hii ya private imetunzwa na humchukua muda mfupi mtumiaji kufika anakokwenda. Ina security cameras. In case unapata shida basi wahusika watakuja on the spot na kukusaidia.

Sasa daraja la Kigamboni linapaswa kulipiwa! Daraja la serikali. Mali ya wananchi wanailipia. Kuna utofauti gani kati ya daraja hili na lile la Salender, lile la Mkapa kule Kibiti, daraja la Wami n.k? Je hili limejengwa na Lugumi Investment Co. Ltd?! Hata kama limejengwa na NSSF. Je serikali haiwezi kurejesha deni hilo kwa NSSF na kuwaacha wananchi wakafaidi matunda ya kodi zao?! Kila mwaka deni la Taifa linapanda. Huyo mkopaji ni nani? Na hizo pesa huwa zinaenda wapi?

Rai yangu kwa JPM.
Mh. Rais wapo waliojenga imani kubwa na wewe. Wapo Watanzania ambao wamerejesha utamaduni wa kuwahi taarifa ya Habari ya saa mbili wakitaka kujua Rais wao kafanya nini leo. Utamaduni huu ulishatoweka na kurejea kwake ni imani ya wananchi waliyonayo kwako. Wapunguzie adha Watanzania kwa kutembea bure juu ya daraja Lao. Wapite bure maana mradi huu huenda ulikuwa ni deal la watu. Kama kweli makatibu wataenda Bungeni kwa mabasi na hivyo kuokoa kiasi hicho cha pesa. Basi pesa hiyo ikalipe deni la NSSF kama ilivyokuwa kwa pesa za sherehe za Uhuru.

Washawishi matajiri wa nchi hii kuungana na kuanzisha miradi ya treni za umeme, private roads, n.k Serikali haiwezi fanya kila kitu. Wapeni uwezo wa kuwekeza. Pawepo na monitoring and evaluation ya uendeshwaji miradi hiyo ili siku ya mwisho irudi na kuwa mali ya serikali (baada ya wao kutengeneza faida).

Daraja la Kigamboni liwe huru, lilindwe na litunze na wote. Liwe la BURE kama ilivyo TBC.

By Goodluck Mshana

WAKUU,

KUHUSU TOZO KAIKA DARAJA LA KIGAMBONI NI MUHIMU NA LAZIMA IWEPO KWA KIPINDI HIKI.

KWA SERIKALI ILITOA TAMKO AMBAYOP NI MOJA YA AHADI ZA MH. MAGUFULI KWA WANANCHI W KIGAMBONI WAKATI WA KAMPENI YA KWAMBA WANANCHI WAENDA WA MIGUU WATAVUKA BURE DARAJA LIKIKAMILIKA.

LAKINI KUHUSU TOZO HAIKWEPEKI KWA WATUMIAJI WENGINE WA DARAJA.

TUELEWE KUWA DARAJA LA KIGAMBONI LIMEJENGWA NA NSSF NA SIYO SERIKALI (WIZARA YA UJENZI) ILE NI PESA YA WANACHAMA WA MFUKO NA SIYO YA SERIKALI.

NIWAPE UFAFANUZI KIDGO KUHUSU DARAJA HILI:-

HAPO AWALI NI KWAMBA LILITAKIWA KUJENGWA PALE FERY NA SIYO HUKU VIJIBWENI. YAANI PALE FERY ILITAKIWA LIWE LA KUFUNGA NA KUFUNGUA.

NA MIMI NAKUMBUKA KUNA KAMPUNI NILIKUWA NAFANYIA KAZI, TULICHUKUA TENDA YA KUJENGA LILE DARAJA PALE FERY LA KUFUNGA NA KUFUNGUA; TATIZO TULISHINDWA KATIKA TARATIBU ZA MALIPO KWANI BAADAYE SERIKALI WALITOA MUONGOZO KUWA MKANDARASI ANATAKIWA KUJENGA KWA GHARAMA ZAKE NA KISHA KUCHUKUA TOZO KWA WATUMIAJI NA UKIMALIZA GHARAMA UNALIRUDISHA KWA SERIKALI (BUILD OPERATE and RETURN - BOR)

HIVYO KAMPUNI YETU TULISHINDWA KUTOKANA NA UTARATIBU HUU NA NDIO MAANA BAADAYE SERIKALI WAKAIOMBA NSSF KUJENGA LILE DARAJA KATIKA MFUMO ULEULE WA "BOR"

HIVYO KUTUMIA BURE ITACHUKUA MIAKA MINGI HADI NSSF WAMALIZE GHARAMA ZAO.

Wasalaaam

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
PRONDO.......yote uliyoyasema ni sahihi....lakini Ndugu elewa watu wanapigika kwelikweli.....Naishia hapo.[/Unachojiliza liza hakieleweki. Prondo ameshakukumbusha kuwa waendao kwa miguu na baiskeli hawalipi hata senti moja.Wenye vyombo vya moto kama magari ndio watakaolipia tozo tena kidogo.Wewe unatakaje sasa?kwamba nao watumie bure kwani wamekutuma?
 
Watu walikuwa wanalalamikia daraja kujengwa kutokana na hadha walizo kuwa wanapata pale kivukoni ambazo ni msongamano wa watu+magari, pili ni zile 200 walizokuwa wanalipia mpaka ikatoka kauli ya watu kupiga mbizi.Kwahyo kama kuna kulipia tena kwenye hili daraja basi hakuna msaada na utofauti wowote Bali ni kwamba badalaa ya kupanda kivuko unapita darajani kwa gharama zilezile au kwa ongezeko la gharama.
 
MADARAJA HAYA YOTE NI YA PUBLIC (Serikali).
1000px-Sydney_Harbour_Bridge_night.jpg
250px-Golden_Ears_Bridge_completed.jpg

Australia, Sydney habour bridge (Umbali: 1.1km) toll: $ 3 - one way. Canada: Golden Ear Bridge ; Toll $2.95 one way

%C3%96resundsbron.jpg

Denmark/Sweden: Oresund Bridge (Urefu: 8km); Toll: Euro 46
220px-Storeb%C3%A6ltsbroen_from_Sj%C3%A6lland.jpg

Denmark: The Great belt bridge (umbali -6km); Toll-$41
500px-Richmond-San_Rafeal_Bridge_wide.jpg

California: Richmond-San Rafael Bridge (Umbali 9km); Toll $5 one-way
 
m kara vipato vya USA au huko kwingine sawa na kwetu hapa..South Africa kuendesha katika zile bara bara zao unalipia kila umbali kuna road toll sasa vipato vya wale tupo nao sisi huku mbona mazuri ya wao mazuri hamtupii humu...
 
sijui unalinganisha nini hapo gari kufika hapa limefika kwa kodi na kila mwaka linapa motor vehicle ambazo still ni kodi kodi zenyewe milioni kumi mpaka 30 tena ulipie kupita katika road zilizojengwa kwa kodi izo..izo nchi hawana kodi ya mamilion katika magari ni kununua tuu na kulipeleka likachekiwe road worth tuu hata wakilipia bara bara sawa tuu..
 
USHURU DARAJA LA KIGAMBONI

Hongera kwa waliofanikisha mradi wa daraja la Kigamboni. Iwe ni serikali ama NSSF. Juhudi zote hizo lengo ni kumsaidia mtanzania. Kumpunguzia adha na bugdha mkazi wa Kigamboni. Kumhakikishia mwananchi usalama wa maisha yake haswa ukilinganisha na ule mchezo wa feri zetu zilizokuwa zikizima na kuharibika mara kwa mara.

Hongera Rais JPM kwa uzinduzi na hivyo kubariki matumizi yake.

Anyway, hoja yangu sio kufurahia uzinduzi wa daraja.. Ama kuzungumzia katumbuliwa kwa Bi. Anne Kilango Malecela. Hoja yangu ni malipo ya matumizi kwa daraja hilo. Labda tujiulize swali moja lakini yenye mantiki kidogo na linalobeba dhana nzima ya matumizi ya daraja.

Swali: Daraja limejengwa na Serikali au mtu binafsi?

Labda tuanze na mifano. Ukifika nchini India utakutana na madaraja, barabara na treni zenye uasili wa daraja la Kigamboni. Kwa maana ya kutoza watumiaji wake. Ukichukua barabara ya kutoka Nerhu Place mpaka ilipo Taj Mahal utakutana na vizuizi njiani. Kila baada ya kilometres kadhaa unalipia matumizi ya barabara. Malipo yote utakayoyafanya yatategemea umbali uendao. Kwa maana ya kwamba ukimua kuendesha gari lako hapa hadi Kibaha. Utalipia umbali wa Kibaha. Ukienda Mbeya au Kilimanjaro, utalipia vivyo hivyo.

Kadhalika kwenye njia za treni. Malipo yote hufanyika kwenye vituo vya treni (metro station). Ukitaka kulipa cash money utalipa. Ukitaka kutumia rechargeable card ni wewe tu. Lakini mifumo yote hii ni tofauti.

Wenzetu wana miuondo mbinu ya aina mbili. Private na Government infrastructure. Kwa miuondo msingi ambayo ni private lazima mtumiaji alipe. Achangie investment cost ili mwisho wa siku watu watengeneze faida. Upande wa pili ni wa serikali. Ambapo matumizi yake ni bure kabisa. Mwananchi halazimiki kulipia popote maana ni miradi ya serikali. Ni miradi inaonekana na kodi za wananchi. Ni miradi iliyoanzishwa kusaidia kizazi cha maskini na mtu wa daraja la kati ambaye hawezi nunua helicopter. Miradi kwaajili ya mtu asiyeweza kupewa tenda za polisi kama Lugumi.

Sasa unaweza shangaa. Kwanini watu wanatumia hiyo ya kulipia na kuacha ya bure ya serikali?! Jibu ni kwamba miuondo mbinu ya serikali ni chakavu na haijatunzwa. Road map yake ni ndevu kuelekea uendako. Hii ya private imetunzwa na humchukua muda mfupi mtumiaji kufika anakokwenda. Ina security cameras. In case unapata shida basi wahusika watakuja on the spot na kukusaidia.

Sasa daraja la Kigamboni linapaswa kulipiwa! Daraja la serikali. Mali ya wananchi wanailipia. Kuna utofauti gani kati ya daraja hili na lile la Salender, lile la Mkapa kule Kibiti, daraja la Wami n.k? Je hili limejengwa na Lugumi Investment Co. Ltd?! Hata kama limejengwa na NSSF. Je serikali haiwezi kurejesha deni hilo kwa NSSF na kuwaacha wananchi wakafaidi matunda ya kodi zao?! Kila mwaka deni la Taifa linapanda. Huyo mkopaji ni nani? Na hizo pesa huwa zinaenda wapi?

Rai yangu kwa JPM.
Mh. Rais wapo waliojenga imani kubwa na wewe. Wapo Watanzania ambao wamerejesha utamaduni wa kuwahi taarifa ya Habari ya saa mbili wakitaka kujua Rais wao kafanya nini leo. Utamaduni huu ulishatoweka na kurejea kwake ni imani ya wananchi waliyonayo kwako. Wapunguzie adha Watanzania kwa kutembea bure juu ya daraja Lao. Wapite bure maana mradi huu huenda ulikuwa ni deal la watu. Kama kweli makatibu wataenda Bungeni kwa mabasi na hivyo kuokoa kiasi hicho cha pesa. Basi pesa hiyo ikalipe deni la NSSF kama ilivyokuwa kwa pesa za sherehe za Uhuru.

Washawishi matajiri wa nchi hii kuungana na kuanzisha miradi ya treni za umeme, private roads, n.k Serikali haiwezi fanya kila kitu. Wapeni uwezo wa kuwekeza. Pawepo na monitoring and evaluation ya uendeshwaji miradi hiyo ili siku ya mwisho irudi na kuwa mali ya serikali (baada ya wao kutengeneza faida).

Daraja la Kigamboni liwe huru, lilindwe na litunze na wote. Liwe la BURE kama ilivyo TBC.

By Goodluck Mshana
Ngoja tusikilize maelezo ya kulipia kesho.. alafu tutajadili zaidi
 
Kama hutaki kulipa beba gari lako mgongoni na upige mbizi!
 
Kikubwa ni serikali kuweka tozo ndogo kumpunguzia mzigo mtumiaji,marejesho yaongezewe muda wa kutosha.
 
Tatizo tunachangia huduma nyingi saana:
Ulinzi shirikishi
Takataka
Madawati
Ujenzi wa mifereji
Ujenzi wa madarasa
Mafuta ya mwenge
nk...nk.
Halafu ona wanavyozitumbuwa wakubwa wetu huku wakitudharau.
 
Yani siku yule mtumbua majipu akatumbua huku akasema ni wizi sasa sijui nyie mnaosapoti tozo mtameza matapishi yenu kwa staili IPI, Nina wakariri hapa msije kuruka mita200 siku hiyo na nyie mkijidai eti ni wizi
 
Back
Top Bottom