Tujadili Sadaka kanisani kwa Mama Rwakatare

Assemblies of God, Assemblies of God, haya makanisa yamejaa kila mahali lakini cha ajabu wamiliki tofauti! Sasa jiulize kwa nini wasilifanye kanisa moja, na wao kusaidiana kueneza injili duniani kote (wafungue tu matawi)? Wizi mtupu kila mtu anataka amiliki sadaka za kwake pekeyake. Kuna wanaojiita manabii, wengine wazee wa upako, wanahubiri utajiri na miujiza kwa sababu wameona watanzania wengi ni masikini waliojawa na matatizo. ngoja nisiseme sana ila wajinga ndio waliwao!! Samahani kama kuna mtu nitakuwa nimemkwaza.
 
Jamani, waacheni wanaopeleka waendelee kupeleka, wamechagua wenyewe!...Msimkatie mama mrija wake!
 
Kumbe kanisa linalipa eeh? ngoja na mimi nianzishe kanisa langu POPOBAWA CHRISTIAN CHURCH.
 
hivi kwani ni nani aliyewatuma kwenda kusali huko,
kwani yale makanisa yenu ya awali yalikwenda wapi?
 
Akifa Kakobe, Rwakatare, Mwingira, Jo Devis and company, ndo kusema na makanisa yamekwisha !???
 
Kuna sadaka zaidi ya tano, tena hamna usiri, watu wanaambiwa wa elfu kumikumi njooni mbele, kisha anakuwekea mikono na kukuombea.
Mbona Biblia inasema tukiwa tunatoa sadaka hata mkono wako wa kushoto isijue?
Mama Rwakatare ana Roho wa Bwana au roho ya money?

watu makanisa kwa sasa ni ofisi zao, kitu hela ndo wanaweka mbele kwanza
ndio maana alimuogopa mchungaji mwenzie kwa kuhisi atamuibia waumini-kwangu hii hai-sound,

Mchungaji Rwakatare kuburuzwa kortini kwa udhalilishaji
MCHUNGAJI wa Kanisa la International Peacemaker, Alex Mavengero, anakusudia kumburuza kortini Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God la Mikocheni, Gertrude Lwakatare, kutokana na kutokubali kumuomba msamaha baada ya kumdhalilisha.

Akizungumza katika ofisi za Tanzania Daima jana, alisema tayari ameshawasiliana na mawakili wake na kesi hiyo inaweza kuanza siku yoyote.

Alisema kitendo cha Mchungaji Lwakatare kumtoa nje ya kanisa lake wakati misa ikiwa inaendelea ni cha udhalilishaji.
Akielezea tukio hilo, alidai Septemba 20 alipofika kwenye kanisa hilo kwa lengo la kusali kama waumini wengine, lakini wakati ibada ikiwa inaendelea Lwakatare alimwita mbele ya kanisa na kumtaka ajitambulishe kwa waumini kuwa yeye ni nani.

"Kwa kuwa sikuwa nikifikiria lolote baya kwa mama huyo, nilienda mbele na kushika kipaza sauti na kujitambulisha kwamba mimi ni mgeni kutoka Arusha, lakini baada ya kusema hivyo aliwaamuru walinzi wake wanikamate na kuniweka kizuizini kwa madai kwamba nimekuja kumuibia waumini wake mpaka pale alipomaliza ibada," alidai mchungaji huyo.
Source- Mchungaji Rwakatare kuburuzwa kortini kwa udhalilishaji
 
Back
Top Bottom