Kwanini Padre hatoi sadaka kanisani?

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
7,091
13,790
Hili ni swali ambalo nimeulizwa na watu wengi sana huku wakitaka kujua, ni sababu zipi zinazomfanya Padre ashindwe kutoa sadaka Kanisani kama wanavyofanya Waamini wengine?

Maana wakati wa adhimisho la Misa Takatifu, mara nyingi tunamsikia Padre akisema: "๐’๐š๐ฅ๐ข๐ง๐ข ๐ง๐๐ฎ๐ ๐ฎ ๐ข๐ฅ๐ข ๐ฌ๐š๐๐š๐ค๐š ๐ฒ๐š๐ง๐ ๐ฎ ๐ง๐š ๐ฒ๐ž๐ง๐ฎ ๐ข๐ค๐ฎ๐›๐š๐ฅ๐ข๐ฐ๐ž ๐ง๐š ๐Œ๐ฎ๐ง๐ ๐ฎ ๐ฆ๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž๐ณ๐ข".

๐’๐–๐€๐‹๐ˆ: Sasa sadaka anayoitoa Padre hapo ni ipi wakati hatuioni?

๐‰๐ˆ๐๐”: Ni kweli kabisa kwa macho ya kawaida, ni vigumu kuiona sadaka anayoitoa Padre altareni kama vile wanavyofanya Waamini wengine, lakini nikuambie kwamba, sadaka ya Padre ni kubwa zaidi kuliko ya mtu yoyote yule.

Ngoja nikuulize swali: Hivi ushawahi kujiuliza kwanini wakati wa utoaji wa sakramenti ya daraja takatifu, Mapadre huwa wanalala chini kifudifudi huku akisaliwa sala maalumu pamoja na litania ya Watakatifu kabla hajawekwa wakfu na Askofu kwa kupakwa mafuta kwenye viganja vyake mikono na kuvalishwa rasmi mavazi ya kikuhani?

Hakika wengi wanadhani kitendo hicho cha kulala kifudifudi kwa Padre, basi anaweka nadhiri za utii kwa Askofu na kumuahidia kuishi maisha ya usafi wa moyo bila kufunga ndoa, ili aweze kumtumikia Mungu kwa uhuru zaidi.

Niseme tu kwamba, hayo yote yanaweza kuwa majibu ila sio kwa mantiki hiyo ya kulala kifudifudi. Kwani kitendo cha Padre kulala kifudifudi, inaashiria kujitoa sadaka kwa ajili ya kuutangaza Ufalme wa Mungu na kuufia ulimwengu kama Yesu alivyofanya.

Kwa sababu hiyo katika hatari yoyote ile ya kifo, ni rahisi sana kumuona Padre akiwa yuko radhi kutoa maisha yake kwa ajili ya Mungu na Kanisa ili kutetea imani iliyoachwa tangu zamani na Mitume wa Yesu.

Kadhalika ukiachana na sababu hiyo, pia hata maisha yake kwa ujumla ni sadaka tosha. Maana wakati wewe unalala usiku, Padre hutumia muda huo kuwaombea watu, yuko tayari kuacha chakula chake ili kumuwahi mgonjwa anayekaribia kufa na kumpa Sakramenti ya Upako. Wakati wote anashinda Kanisani ili kusikiliza shida za watu na kuwasaidia, daima aachi kutoa Sakramenti ya Kitubio hata kama afya yake haiko vizuri siku hiyo.

Maisha ya Padre kwa nje unaweza kuona ni mepesi, ila ukweli ni magumu sana, bila sala na moyo wa majitoleo huwezi. Kwa sababu kokote pale Padre akihitajika huwa anafika kwa wakati licha ya kuwa na kazi nyingi. Tena muda mwingine kwenye msiba utamkuta Padre anahuzunika na wale waliofiwa hata kama msiba huo haumuhusu, na wakati wa harusi hufurahi pamoja na wale waliofunga ndoa. Kwangu hiyo ni sadaka, sasa sijui muuliza swali alikuwa anataka sadaka ipi?

Maana Padre hawezi kutoa sadaka ya pesa, mazao au mnyama wa aina yoyote yule kama Wakristo wengine wanavyotoa. Ukweli nikuambie tu kuwa, muda mrefu Padre kashajisadaka tayari mwili na roho yake kwa lengo la kumtumikia Mungu na Kanisa. Na ndio sababu nasema, sadaka ya Padre ni kubwa zaidi kuliko zile tunazozitoa sisi kila siku.

Pia hata tukisema leo hii sheria ipitishwe rasmi, eti Padre naye atoe sadaka sawa na Waamini wengine. Je unafikiri sadaka hiyo Padre ataitoa wapi, wakati hana kazi wala kitega uchumi chochote kitachomuwezesha kufanya hayo yote?

Nadhani hapo ndio mwanzo wa Kanisa kuingia katika migogoro, kisa tu Padre ameanza tabia ya kuiba sadaka za watu ili apate pesa za kutoa Kanisani. Suala hili sio nzuri na halifai kabisa.

Kwani ukisoma vema Biblia, utakutana na kisa cha makabila 12 ya Waisraeli, ambayo makabila hayo yote yalipewa urithi katika sehemu yake ila kasoro kabila moja tu la Walawi, maana urithi wao ulikuwa kwa Bwana pekee na walipewa kibali cha kutumia sadaka zote zilizotolewa na Waisraeli wa wakati ule Hekaluni. (๐Œ๐ฐ๐š๐ง๐ณ๐จ 14:17-20).

Biblia inatuambia kabila hilo la Walawi ndilo lililowekwa wakfu kwa lengo la kutoa Makuhani kwa kazi ya Mungu tu, utaratibu ambao unatumika hadi sasa kwa Mapadre wetu. (๐–๐š๐ฅ๐š๐ฐ๐ข 22:1-33).

Kwahiyo nihitimishe kwa kusema kwamba, sote kama wanadamu tuna wajibu wa kutoa sadaka ingawa sadaka zetu zinatofautiana kidogo. Maana Padre hutoa sadaka yake ya mwili na roho kwa ajili ya Kanisa, na sisi basi tutoe sadaka za pesa na mali tulizonazo kwa ajili ya kujiombea wenyewe baraka na wale wote wanaotuzunguka.

๐“๐”๐Œ๐’๐ˆ๐…๐” ๐˜๐„๐’๐” ๐Š๐‘๐ˆ๐’๐“๐Ž
FB_IMG_1695785228284.jpg
 
Mkuu usiwatetee eti hawapaswi kutoa kwa kuwa hawana kazi siyo kweli nao wanapaswa kutoa maana wanalipwa hao kutokana na sadaka na zaka za waumini kwa kulipwa huko nao wanawajibika kutoa maana hata walawi uliowafananisha nao vilevile kwa vile vilivyotolewa na kupewa waliambiwa nao watoe zaka na sadaka sasa padri kwanini wasitoe?

Hebu tusome hapa halafu tujadili kwanini wao wasitoe.

Hesabu 18

25.Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

26 Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.

27 Na sadaka yenu ya kuinuliwa itahesabiwa kwenu, kama ndiyo nafaka ya sakafu ya kupuria, na kama kujaa kwake kinu cha kushindikia zabibu.

28 Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana.

29 Katika vipawa vyenu vyote mtasongeza kila sadaka ya kuinuliwa ya Bwana, ya wema wake wote, hiyo sehemu yake iliyowekwa takatifu.
 
Sasa hapo hauoni kuwa walawi huwa wanachukua zaka kutoka mikononi mwa waisrael?
 
Back
Top Bottom