Unajua concept ya ndoa nayo katika dunia ya utandawazi hii imekuwa ngumu sana kuijadili.
/QUOTE]
You are right aisee
Kwanza waliowafundisha mafunzo hayo ya uchumba ni watawa au watu wenye ndoa zao?? Nataka kupima uzoefu wao wa hali halisi. Mtu anayekufundisha theory ya kuogelea wakati si mwogeleaji ni ngumu sana kujua changamoto za swimming pool, bahari, mto na ziwani. Mengine ana-assume tu kumbe ndivyo sivyo. Hakuna kitu kilichokuwa naona muujiza kama 'alteration in rocks' lakini kiuhalisia ize tu, anyway. Changamoto ya kwanza.
You are right, mwalimu wetu wa dini alikuwa ni mtawa na frate pia. Lakini si mapadri wanao toa mafundisho ya ndoa ilhali wao hawana, na si ndio wanaosuluhisha mafarakano ya ndoa pia. So ilikuwa ni mafunzo kwenye context ya kikristu.
Pili, kuwa na marafiki wengi, afu mchumba mmoja, makusudio yake yalikuwa mchumba mkishindwana unateua rafiki mwingine kuwa mchumba?? Kama ndio, nafasi ya upendo iko wapi? Je, wana-assume kuwa upendo ni equally distributed kati ya marafiki au wachumba tofauti??? Changamoto ya pili.
Makusudio ya awali, ni kuwa mchumba apatikane kati ya marafiki ikiwezekana, na marafiki ni wa jinsia zote. But the main point was vingine vyote waweza kuwa navyo vingi lkn sio mchumba (yule mliyeahidiana kuoana). So obvious upendo hauwezi kuwa sawa.
Lakini pia, ishu ya kuwa na plan B katika dunia ya leo ambayo asilimia kubwa ni kuvuana kyupiz kabla ya ndoa inakuwaje? Nafasi ya uaminifu? Kama wakati wa uchumba tu ambapo bado unamhemuko wa mwenza wako, hamu haikuishi una Plan B, je mkiingia kwenye ndoa? Pale ambapo umeshajua mapungufu yake anakoroma usiku, akila anarusha chakula, labda ni insecure. he is no longer exciting, utakuwa mwaminifu?? Je wakati anashambuliwa na magonjwa kama kisukari, utakuwa mwaminifu?? Je ambapo hana uzazi, utakuwa mwaminifu??
Je wapenzi mtakuwa mnaaminiana wakati mnajua kila mmoja alikuwa na plan B wakati wa uchumba?? Changamoto ya tatu.
Exactly my point; kama umekuwa na nafasi ya kumchunguza na mkakubaliana kuwa wachumba, kwanini kuwe na umuhimu wa kuwa na potential hubby/wifey pembeni? Ina maana neno mchumba ni sawa tu na uBF na uGF? kwanini uwe na mashaka (kama yapo) kwamba akiniacha nitakuwa na mtu mwingine?
Lakini pia, unapokuwa na Plan B, wakati Plan A iko active, una uhakika kiasi gani Plan B itakuoa pale A mambo yanapokwenda mrama? Je Plan B nayo ikiingia mitini? Kutakuwa na haja ya kuwa na Plan C and D labda??
Good question
Aisee, ndoa na mapenzi hayana mahakama wala insurance kwa mtizamo wangu. Noana hapa Plan B inataka kutumika kama insurance hivi.
Good observation pia.