mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 80,874
- 106,135
Umeeleweka vizuriHii ni hulka ya viongozi wote wa nchi masikini na hasa Afrika. Hujifikiria wao na kutaka kujikusanyia kila kitu.
Marais wote wanapokuwa madarakani nyumba zao hukarabatiwa kwa gharama ya serikali kwavile zinakuwa ni ''Ikulu'' wakati wowote. Hivyo, Rais Mwinyi na Kikwete wana nyumba zao.
Pili, viongozi wastaafu wanapewa asilimia 80% ya mshahara wao( Rejea mafao ya viongozi wa juu)
Wanapewa ulinzi na huduma zote kama zile walizopata wakiwa Ikulu.
Hawa si wanyonge
Nyumba wanazojengewa thamani zake ni kubwa kuliko vituo vya afya.
Lakini muhimu ni kuwatazama kama wana manufaa yoyote kwa Taifa baada ya uongozi.
Hawa kazi yao ni kupigia debe CCM na chama kingefanya taratibu za kuwahudumia si kodi za wananchi
Hawana kingine tunachoweza kujivunia kama walipa kodi. Hili ni hulka tu ya kujikusanyia na kujilimbikizia kwa gharama za wananchi. Tunahitaji vituo vya afya vya umma si nyumba binafsi
JokaKuu tindo Pascal Mayalla
Ova
Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app