Tujadili nyumba wanazojengewa Marais Wastaafu Tanzania

Hakika mwenye nacho huongezewa. Hivi kulikuwa na haja gani kuwajengea hawa watu ambao bila shaka tayari walikuwa na utajiri na majumba ya kutosha tena nyumba?
Hizo pesa mbona kuna wengi tu wenye uhitaji nazo?
 
Hujasoma mahali imeandikwa kuwa;

".....kila mwenye nacho huongezewa na asiyekuwa nacho hunyang'anywa hata kile kidogo alichonacho....?"

Yes, sisi hatuna hata mfano tu wa nyumba, lakini hawa waliokuwa tunawalipa mishahara ya mamilioni kila mwezi, posho na marupurupu ya kila namna leo eti wanajengewa nyuma toka katika michango yetu kidogo dogo tunayolipa kama kodi..

Kama siyo kituko unadhani ni nini?
 
kama milioni 50 kila kijiji hazikupatikana,25 kwa kila mtz ni ndoto zile zile za kuongeza mishara maradufu huku ukiondoa kodi.
huwezi sema kila mtu atapewa 25ml haiwzekani kabisa suala hapa ni ujenzi wa sky screper unajua upo ujenzi fulani hivi kwa wenzetu jengo moja linaweza anzia posta mpaka mbagala nyumba 2000 nenda kanada uone nyumba nyingi kuliko idadi ya watu
 
Watumishi kura kwa Lissu zote.

Mmeteswa sana miaka 5

Walimu wamejengewa?
 
SAWA PUNGUANI MKUBWA, CDM KAMA SIO KUTUMIA AKILI ZA KUWA WAHIFADHI FEDHA KAMPENI HIZI WANGELIFANYAJE MAANA SEREKALI IMENYIMA KABISA HELA ZA KAMPENI NA KUTOA KUDUCHU MNO KWA DHAMIRA VIFELI KWENYE KAMPENI KUMBE WENZAO WAKAWA NA AKILI KUBWA ZAIDI MPAKA WAMEKODI NA CHOPA KITU AMBACHO KINAWASHANGAZA SANA CCM "'mradi wa nyumba bora kwa watanzania wote wanyonge upo pale pale kila familia ya mtanzania na nyumba moja" ndio mkakati wa LISSU 2020-2025
Huyo chizi muulize na yeye mbona ameshindwa kupanga chumba badala yake anaishi kwa shemeji yake
 
Haya yame toka wapi ,bado haujajibu Swali lililo Mezani Mkuu.
Wapo wapuuzi ambao wanaona hili jambo halituhusu. Hizi ni fedha za walipa kodi. Nimeiona hiyo nyumba ya Kikwete, utadhani ni nyumba ya familia ya watu 50. Huo, ni ufujaji wa fedha tu. Kwa vile wanajua HAWAWEZI KUFANYWA CHOCHOTE NA YEYOTE, basi twende tu. Tutafika!
28/10/2020 ni siku ya kuyabariki haya, au kuharamisha. Kazi kwetu!
 
Hizo nyumba zinajengwa kisheria. Marais wakistaafu wanatembelewa na viongozi mbali mbali kutoka nje mnafikiri hao viongozi wakiwatembelea watalala wapi? Former presidents hawawezi kuishi kama nyinyi malofa. Kila ndege huruka kwa mbawa zake. Tanzania tuna uwezo wa kuwajengea former presidents mahali pa kuishi kwa kufanya kazi waliyokuwa wamepewa.
 
Tafadhali sheikh ondoa neno lofa tafadhali sana
 
Hii ndio sheria ya hovyo kabisa kwa nchi masikini zaidi duniani. Inakuwaje mtu ambaye anajilipa mamilioni ya pesa tena pasipo kutozwa kodi na anayegharamikiwa na serikali kwa kila kitu ajengewe nyumba kwa jasho la masikini ambae hata akipiga tu miayo kwa njaa anatozwa kodi tena kandamizi?
Hapa ndipo wale wasioelewa vizuri wataelewa maana halisi ya neno UFISADI (kleptocracy) - yaani WIZI uliohalalishwa ndani ya serikali. Hii ni pamoja na malipo ya kufuru ya wabunge. Waliipisha wenyewe hizo sheria ili wakwibe. Ukilalamika wanakwambia ni matakwa ya sheria. Ndio maana nchi hii ya Tz inahitaji mabadiliko makubwa ya mfumo wa kiutawala. Huwezi kumsikia 'mzalendo' Magufuli akitaja hata kwa mbali!!! Hii imewafanya hata wananchi wanaobiwa, waone ni haki yao wezi kuiba na wao kuibiwa!!!!! Hapa panahitajika mabadiliko ya kifikira/kimtazamo (mindset). Fursa tuliyokuwa nayo ni hii tu ya TAL kuingia madarakani. Ameonyesha wazi kukerwa na huu mfumo-fisadi.
 
1. Naomba kujua nyumba Mwalimu aliyojengewa na serikali ilijengwa lini na wapi?

2. Naomba kujua Mkapa alijengewa nyumba yake wapi?

3. Naomba kujua kwa changamoto wananchi tulizonazo Hawa wazee wakitoa sadaka hizo pesa za nyumba zikajenga japo hospital haitakubalika?

4. Hawa viongozi wanaojengewa nyumba baada yakuondoka madarakani wakiwa wazee, awali walikua wanaishi wapi?

5. Natambua ni takwa la kisheria ila najiuliza kwanini sasa? Mwinyi kastaafu muda gani?

6. Kwa marais wa Zanzibar, je huu utaratibu unawahusu?

Ushauri
Haya mafao ya nyumba za marais yafutwe, sheria itamkwe atalipwa kiasi flani (thamani ya hiyo nyumba) na Mstaafu atawajibika kuchagua eneo ambapo fedha hizo zitatumika kujenga mradi wa wananchi Kama ukumbusho.
Nitajikita kwa number 5.
5. Natambua ni takwa la kisheria ila najiuliza kwanini sasa?
- Kuhamia Dodoma kwanini sasa?
- Umeme mto Rufiji kwanini sasa?
- Meli ya kuleplace Mv Bukoba, kwanini sasa?
- kulinda maliasili yetu, wanyama, madini kwanini sasa?
NK

Yote hayo yamewezekana kwasababu Ya Magufuli - ni mtekelezaji na mzalendo wa kweli - tumechelewa vya kutosha, nchi imeliwa vya kutosha na Magufuli amesema sasa basi.
Anatekeleza yaliyokuwa yamepuuzwa na waliomtamgulia
 
Ni upotevu wa pesa za walipa kodi kuwajengea MABILIONEA majumba ya kifahari wakati tayari wana majumba kibao walijenga wakati ni maraisi.
 
119976986_720875661975398_6178179625576337321_n.jpg

Oooh binadamu wote sawa...acheni ujinga 2020 ni Yeye
119976986_720875661975398_6178179625576337321_n.jpg
 
Hii nyumba ya Rais mstaafu Mzee Mwinyi iliyozinduliwa leo Karibu na Uchaguzi,huenda ikapunguza Kura nyingi sana za CCM Wakati huu wa uchaguzi.Maana kwa Wa-Tanzania walio WENGI hii kitu kichwa chenye aKili ya kawaida hakiwezi "ku-acomodate" hii kitu.Huyo ofisa aliyeshauri hii kitu ifanyike kipindi Hiki Amechemsha.Ni sawa na Unakula na kipofu sahani moja Halafu unamshika mkono kumuelekeza nyama zipo Hapa.
Ni jeuri tu linawasumbua
 
1. Naomba kujua nyumba Mwalimu aliyojengewa na serikali ilijengwa lini na wapi?

2. Naomba kujua Mkapa alijengewa nyumba yake wapi?

3. Naomba kujua kwa changamoto wananchi tulizonazo Hawa wazee wakitoa sadaka hizo pesa za nyumba zikajenga japo hospital haitakubalika?

4. Hawa viongozi wanaojengewa nyumba baada yakuondoka madarakani wakiwa wazee, awali walikua wanaishi wapi?

5. Natambua ni takwa la kisheria ila najiuliza kwanini sasa? Mwinyi kastaafu muda gani?

6. Kwa marais wa Zanzibar, je huu utaratibu unawahusu?

Ushauri
Haya mafao ya nyumba za marais yafutwe, sheria itamkwe atalipwa kiasi flani (thamani ya hiyo nyumba) na Mstaafu atawajibika kuchagua eneo ambapo fedha hizo zitatumika kujenga mradi wa wananchi Kama ukumbusho.
Nimejikuta nakutukana.

Maskini mnao siku zote.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom