Tujadili nyumba wanazojengewa Marais Wastaafu Tanzania

1. Naomba kujua nyumba Mwalimu aliyojengewa na serikali ilijengwa lini na wapi?

2. Naomba kujua Mkapa alijengewa nyumba yake wapi?

3. Naomba kujua kwa changamoto wananchi tulizonazo Hawa wazee wakitoa sadaka hizo pesa za nyumba zikajenga japo hospital haitakubalika?

4. Hawa viongozi wanaojengewa nyumba baada yakuondoka madarakani wakiwa wazee, awali walikua wanaishi wapi?

5. Natambua ni takwa la kisheria ila najiuliza kwanini sasa? Mwinyi kastaafu muda gani?

6. Kwa marais wa Zanzibar, je huu utaratibu unawahusu?

Ushauri
Haya mafao ya nyumba za marais yafutwe, sheria itamkwe atalipwa kiasi flani (thamani ya hiyo nyumba) na Mstaafu atawajibika kuchagua eneo ambapo fedha hizo zitatumika kujenga mradi wa wananchi Kama ukumbusho.
Tuta jadili baada ya uchaguzi
 
Watanzania watu wa ajabu sana, wengi wanategemea former presidents walale kama popo.
 
Back
Top Bottom