Tujadili nyumba wanazojengewa Marais Wastaafu Tanzania

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
336
1,000
1. Naomba kujua nyumba Mwalimu aliyojengewa na serikali ilijengwa lini na wapi?

2. Naomba kujua Mkapa alijengewa nyumba yake wapi?

3. Naomba kujua kwa changamoto wananchi tulizonazo Hawa wazee wakitoa sadaka hizo pesa za nyumba zikajenga japo hospital haitakubalika?

4. Hawa viongozi wanaojengewa nyumba baada yakuondoka madarakani wakiwa wazee, awali walikua wanaishi wapi?

5. Natambua ni takwa la kisheria ila najiuliza kwanini sasa? Mwinyi kastaafu muda gani?

6. Kwa marais wa Zanzibar, je huu utaratibu unawahusu?

Ushauri
Haya mafao ya nyumba za marais yafutwe, sheria itamkwe atalipwa kiasi flani (thamani ya hiyo nyumba) na Mstaafu atawajibika kuchagua eneo ambapo fedha hizo zitatumika kujenga mradi wa wananchi Kama ukumbusho.
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
11,662
2,000
Punguani, mmeshindwa ofisi ya makao makuu ndo iwe nyumba za watanzania?. Labda Robert Amsterdam awajengee wake zake.
View attachment 1604263
SAWA PUNGUANI MKUBWA, CDM KAMA SIO KUTUMIA AKILI ZA KUWA WAMEHIFADHI FEDHA ZA KAMPENI SIJUI WANGELIFANYAJE MAANA SEREKALI IMENYIMA KABISA HELA ZA KAMPENI NA KUTOA KUDUCHU MNO KWA DHAMIRA VIFELI KWENYE KAMPENI KUMBE WENZAO WAKAWA NA AKILI KUBWA ZAIDI MPAKA WAMEKODI NA CHOPA KITU AMBACHO KINAWASHANGAZA SANA CCM "'mradi wa nyumba bora kwa watanzania wote wanyonge upo pale pale kila familia ya mtanzania na nyumba moja" ndio mkakati wa LISSU 2020-2025
 

MWANDENDEULE

JF-Expert Member
May 24, 2015
2,726
2,000
Hii ndio sheria ya hovyo kabisa kwa nchi masikini zaidi duniani. Inakuwaje mtu ambaye anajilipa mamilioni ya pesa tena pasipo kutozwa kodi na anayegharamikiwa na serikali kwa kila kitu ajengewe nyumba kwa jasho la masikini ambae hata akipiga tu miayo kwa njaa anatozwa kodi tena kandamizi?
 

Matrix19

JF-Expert Member
Feb 24, 2020
1,794
2,000
Suala sio kujengewa tu aina/ukubwa wa nyumba unafikirisha sana kitu kinachopelekea gharama ya nyumba kuwa kubwa kuliko idadi ya watu kwenye familia za wahusika! Halafu kuna mwananchi kule Kigoma anashuhudia haya huku akinywa Maji kwenye kisima ambacho mifugo hunywa maji pia!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom