Tujadili kuhusu mtandao wa Halotel

Tujadili kuhusu mtandao wa Halotel

Kwani unakimbizwa,au umeambiwa uwahi kutoa habari utapewa zawadi,unasema utakuwa rahisi kupita mitandao yote tueleze kivipi,kwa mfano ungesema kwa sekunde au dakika bei yake itakuwa hivi,kupiga kwenda mitandao fulani itakuwa kiasi hiki kwa muda wa sekundu au dakika,kifurushi cha data kituwa GB fulani kwa TZS halafu hapo ndio tuone huo utofauti,lasivyo subiri kuanza ,ukipata maelezo ya kina ndio uje utuhabarishe hapa kwa sasa hayo maelezo ni kama propanganda za uchaguzi wa raisi,wabunge na madiwani utakaofanyika mwezi huu

Subiri utaona,kabla hujajibu ni vizuri ukapitia taarifa fupi kutoka vyanzo vingine
 
Naona wazee wa marketing vietel mko kazini, nawatakia kazi njema!
 
Mtandao wa simu mpya toka Vietnam Halotel (vietel),utazinduliwa rasmi jumatano 14/10/2015.
Ni mtandao utakaotoa Huduma kwa bei ndogo kabisa kuliko mitandao yote nchi nzima na Huduma zao zitapatikana vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini,kila sehemu utayokua utakua hewani,
Watazindua na smart phones zao zenye ubora na garama nafuu kabisa,kwa kuzingatia kipato cha mtanzania Wa kawaida,
Mimi nitakuwa Wa kwanza kununua line ya halotel na smart phone ya halotel(vietel) sababu nimechoka unyonyaji Wa Vodacom na Airtel.

Ni maamuzi mazuri but kumbuka siku zote za maisha yako mtu yoyote ambaye ni capitalist lazima atakunyonya na anapenda zaidi ku-maxizime profits so tegemea baadae sana they gonna increase cost.
 
Kweli kabisa ndg, tunanyonywa sana, mawasiliano ni haki na kitu cha lazma lkn voda/tigo/airtel nk wanafanya kama anasa, angalia huduma ya data, watu tunatumia kwa kusoma wao wanatoa MB chache wakidhani tunaangalia porno (ngono video). Ghaaaaa tumechoka. Hebu nipe taarifa wapo wapi hawa?
 
Watanzania tusidanganywe na halotel, kampuni yoyote mpya ikitaka ingia kwenye soko lenye upinzani kamwe haiwezi anza na bei kubwa, wanaanza na bei ndogo ili kuvuta watu....
Tigo, Voda na Airtel hawatashusha bei maana wanajua ni nguvu ya soda wapi Sasatel na Zantel?
 
Ni maamuzi mazuri but kumbuka siku zote za maisha yako mtu yoyote ambaye ni capitalist lazima atakunyonya na anapenda zaidi ku-maxizime profits so tegemea baadae sana they gonna increase cost.

Baadae ila for the mean time tutafune gb5 hizo plus dakika kibao
 
Huo mtandao ni mkubwa kiasi gani kuweza kutoa huduma vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini?maana yake umewafikia watu wote nchi nzima?

Cable yao imepita kote huko,njiani na vijijini
 
Binafsi nimechukizwa na mwenendo wa mitandao yetu hii ikiongozwa na Voda,tigo na mwisho Airtel.Hawa jamaa hawajali afya ya mlaji na kama hii mamlaka ya TCRA ndio wanaoratibu huu unyonyaji basi walaaniwe.
Ni jambo la kushangaza kwa jinsi teknolojia ilivyo kua kwa kasi tofauti na zamani leo kila kitu kinachotuzunguka ni smart kuanzia simu,magari,kompyuta,t.v etc.Huwezi kuzitumia hizo nyenzo ki uhakika bila kuwa na matumizi makubwa ya data.Cha ajabu haya makampuni yametumia mwanya huo kutunyonya kwa dhahiri bila kujali na mamlaka ya kudhibiti hilo ipo,hata kwa wenye uelewa mdogo wa teknolojia ya mawasiliano unawezaje kuanzisha 4G kwa kujinadi halafu unamuuzia mteja mb1 kwa Tsh.500 kwa siku? Unawezaje kumuuzia mteja mb60 kwa wiki kwa Tsh.9999? Ni kituko ambacho kitauchekesha ulimwengu mzima."Its only possible in Tanzania."
Kiufupi,tunahitaji huduma bora zilizokuwa tailored to our needs na sio huduma fixed zilizopo ili kutunyonya.Cha kushangaza zaidi wanachokifanya wao ni kuturundikia ma SMS lukuki huku dakika zikiwekwa chache na bandwidth ndio loh aibu hata kuitaja.Wateja wengi hasa wa mijini tunahitaji data na dakika zaidi kuliko SMS ambazo zimekuwa overtaken na 3rd party applications kama whatsapp,facebook,imo,kik,tango,n.k.
Pendekezo,wenye mitandao yenu fanyeni upya review ya vifurushi vyenu jamani sio kutuhadaa na 4G LTE ambayo ni sawa na bure maana hatuwezi kunufaika nayo."We need more data at affordable prices."
La sivyo mabadiliko yatawahusu pia.
 
Watanzania tusidanganywe na halotel, kampuni yoyote mpya ikitaka ingia kwenye soko lenye upinzani kamwe haiwezi anza na bei kubwa, wanaanza na bei ndogo ili kuvuta watu....
Tigo, Voda na Airtel hawatashusha bei maana wanajua ni nguvu ya soda wapi Sasatel na Zantel?

Tena voda walivyosikia Halotel wanakuja kwa kiburi wamepunguza kale kaMB 8 hadi MB1 doh!
 
Kumbe voda inamuhusu Edo?Basi ngoja tumchangie kwanza ili aitoe mbio ccm kisha tutayamaliza baadae haya mambo yetu na raisi wetu.

Mwambie amrudishe mke kwanza ndo tutakuwa na imani nae vinginevyo haturudii makosa ya wale wanaotaka kuingi ikulu na wachumba!
 
kabla ya kusifia huo mtandao inakubidi ujiulize swali hili!

je, huo mtandao utaendeshwa kwa sheria na taratibu za nchi gani?
-maana kama na Tz Kampuni pekee inayoweza kutoa huduma kwa bei nafuu ni ile iliyo chini ya serikali (TTCL) haya mengine hawawezi kwani kufanya hivyo itakuwa hasara kwao.

Kitu itakua ile ya wazungu wanasemaga "under my roof, my rules"
 
Huo mtandao ni mkubwa kiasi gani kuweza kutoa huduma vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini?maana yake umewafikia watu wote nchi nzima?

Miundo mbinu Fiber Optics cable with direct connection from Minara paka Minara ingine
 
Nimesearch manually nimekuta: Hits Tz ..sijui ndio wenyewe?
 
Back
Top Bottom